Nipo Kiongozi wetu,ni kweli kabisa huku bila kitunguu swaumu mchuzi haujapikika wala samaki/kuku hajakaangika,ila makaburu wa RSA kwa hapa Maputo wanaingiza sana vitunguu na wenyeji na wao wanalima pia,kitunguu kimoja kinachambuliwa au kinauzwa kizima kwa 5 au 10mt. Na exchange rate US$ 1 =27mt. Hiyo ni bei ya kitunguu jijini Maputo.
hivi jamani mozambique ni sehemu nzuri ya kusoma vyuo au bora nibaki humuhumu bongo? Nisaidieni jamani...
nadhan bora ubaki nyumban coz wenyewe kwenye upande wa elimu wako nyuma
Mi niko Maputo Cidade,kama unataka kusoma basi soma huko huko Tz.Wewe upo maputo au wapi?
mkuu LAT sisi huku Nampula tuna kaumoja ketu sio mbaya wakati wa shida tunasaidiana japo wabongo tunauzito fulani.lakn tunasonga!
mkuu LAT sisi huku Nampula tuna kaumoja ketu sio mbaya wakati wa shida tunasaidiana japo wabongo tunauzito fulani.lakn tunasonga!
Mkuu Speedy! Nataka kuja pemba na Coaster yangu nijuze biashara ya daladala ikoje huko? Barabara zinaeleweka? Foleni vipi kama bongo?
Jamani mlioko huko Moza hasa Maputo, gharama za kufika huko toka Dar zikoje kwa kupitia Mtwara? Na plan kuja huko kuona nini cha kufanya miaka michache ijayo. Ulaya nimechemsha,ubavu wa kufanya vitu Ulaya kwa sasa sina,ila Moza naweza kumudu.
Mi naomba kujua zaidi kuhusu nguo na accessories na cosmetic ni mji gani inalipa na je ni njia gani nzuri ya kufanya. Asante
ila lugha ni issue speedy,lizzard. Full kireno.na hela nazo ni changamoto nyingine. Namba iliyoandikwa sio thamani yake kama huku tz unavyotafsiri hela kirahisi. Mfano noti ya 200 thamani yake sina hakika ni kama elfu kumi ya tz na ni kama elfu arobaini mitkash..ila watu wengi wanatoka kimaisha huko mi niko mtwara naona.kama unataka fanya kwa rejareja ili uvune faida kubwa njoo pemba ila kama unataka jumla nenda nampula. Karibu