Dogo Janja na Kinyozi.

sir Ganto G

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2013
Posts
573
Reaction score
114
Wakiwa saloon kinyozi akamwambia rafiki yake " kuna dogo mmoja ni mjinga mjinga sana,sijawahi ona dogo mjinga kama yeye, na muda si mrefu atakuja na ntakuthibitishia ujinga wake.
Dogo akaangia saloon, Kinyozi akachukua noti ya elfu mbili akaweka mkono wa kulia na coins za mia mia mbili mkono wa kushoto, Dogo akachagua coins na akaondoka zake.
"si umeona nilichokuwa nakisema Dogo ni mjinga ni mjinga wa mwisho, utadhani katoka kijijini leo" Kinyozi akapiga kelele.

Siku ya pili Rafiki wa kinyozi akamwona Dogo kwa mbali akiwa analamba Chostik baada tu ya kutoka kwa kinyozi kama kawaida yake, rafiki wa kinyozi " wee Dogo mbona kila ukipewa uchague hela unachukua coins badala ya noti?".

Dogo akajibu "siku nitakapo chukua ile noti tu ndo utakuwa mwisho wa kamchezo"
 
Janja ya toto, akili anayo huyo...polepole ndiyo mwendo!
 
Haha ana akili sana dogo haba na haba hujaza kibaba!!

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Kinyozi anajifanya anajua kumbe Dogo anamwinjoi tu.....
 
ndo maana yake dogo anajitambua bwana haaa chezea akili weye
 
Hiyo inaitwa kula kwa kijiko cha chai hushtukiwi!
 

kuna watu mnapenda sana kutembea juu ya ganda la ndizi, yani mnamwaga povu la sabuni ya unga kwenye tiles halafu mnatelezea

Hamjisumbui hata kidogo kutumia akili zenu, kutwa kucha mnaangalia ni vipi mtatembelea juu ya bamia
 

Mwisho wa mchezo kivipi? cjaelewa flani hivi
 
Mkuu shine dogo kakusudia siku atayochukua noti kinyozi hatompa tena nafasi ya kuchagua hela. So bora achague coin ili mchezo uendelee kila siku
 
Hahahahaha sasa hapo Jamaa siku akija kujumlisha coins zote alizozitoa atajuta kumfahamu dogo.
 
Mkuu shine dogo kakusudia siku atayochukua noti kinyozi hatompa tena nafasi ya kuchagua hela. So bora achague coin ili mchezo uendelee kila siku

MM NADHANI MAKUBALIANO KATI YA DOGO NA MGANGA WAKE NI KWAMBA ASICHUKUWE HELA YA NOTI SIKU AKICHUKUWA MCHEZO UNAISHIA HAPO!! AU VP? TEHTEH!teeee.NOMA SANA
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…