DODOSO ni Bomu lingine kwa Elimu ya Juu

DODOSO ni Bomu lingine kwa Elimu ya Juu

mkuu wa vilaza

Senior Member
Joined
Apr 25, 2015
Posts
192
Reaction score
85
Bomu la kwanza liliwekewa pause litaendelezwa second semester (MEANS TEST) Bomu lingine limeletwa nalo ni DODOSO kwa wanufaika wa mikopo ya Elimu ya Juu.

Ikiwa ni mwaka sasa tangu ulipoingia utawala wa awamu ya tano, tumeshuhudia mabadiliko mbalimbali katika kila wizara na taasisi zake yakiwa yanafanywa mengine bila hata ya kuwepo kwa ushirikishwaji wa walengwa. Mwaka wa masomo 2016/2017 tumeshuhudia aina ya kipekee kabisa ya utoaji mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu kutoka bodi ya mikopo kwa system inayoitwa *Means Test* ambayo tumeona jinsi ilivyokuwa mwiba kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza kwa kujikuta wanapewa hadi 1300 kwa siku kutoka 8500 iliyokuwepo awali.

Baada ya siku kadhaa kupita hao hao bodi ya mikopo wamekuja na jinamizi lingine linaloitwa DODOSO ambalo wanafunzi wanaondelea na chuo na niwanufaika wa mikopo (continuous) wanatakiwa wajaze taarifa zao.

Katika hilo DODOSO kuna mambo ya ajabu sana ambayo kwangu mimi baada ya kutafakari kwa kina nimegundua ni moja ya njia ya kupunguza wanufaika wa mikopo ya Elimu ya juu. Kwa nini nasema hivyo?

1.Kwenye DODOSO unatakiwa ujaze taarifa za wazazi ikiwemo nyumba anayoishi hali yake je tofali au udongo,
2. Kama mzazi ni mwajiriwa uambatanishe risiti za malipo ya mzazi (bank statement ), pia uambatanishe level ya Elimu ya mzazi (vyeti)
3. Kama mzazi ni mfanyabishara pia uweke kiasi cha pato lake baada ya kulipa kodi TRA.
4. Kuna sehemu ya kuambatanisha mali za wazazi (mifugo,mashamba )
5. Pia ipo sehemu ya kujaza Parents/guardian life styles

Ukisoma vyote hivi unafikia katika mawazo ya kwamba serikali haina pesa za kugharamia Elimu ya juu na njia pekee ni kupunguza wanufaika. Na hili watafanikiwa kwa asilimia kubwa kama wamedhamiria.

Baada ya kuandika hizo paragraph hapo juu ilibidi nijiulize kama bodi wanayo mandate ya kuvunja mkataba tuliokuwa tumeingia nao awali nikakutana na kipengele kinachosema bodi wanayomamlaka ya kusitisha mkopo kwa sababu wanazozijua wao, ukiondoa mambo mengine kama kudisco, kuacha chuo, mwanafunzi mwenyewe kusitisha, na pia kufukuzwa chuo.

Hivyo basi hii ndio Rai yangu kwa serikali za wanafunzi za vyuo vyote nchini wafanye juu chini kukutana na bodi na kujiridhisha kwamba baada ya kujaza DODOSO hakutakuwa na wanafunzi watakaopunguziwa mkopo. Hilo liwe lengo kuu la kikao. Kama hili litawashinda basi ni muda wao wa kuachia ngazi kwa kuwa wameshindwa kuwatumikia waliowachagua.

Pia kwa serikali ya Mh Magufuli itimize kwa vitendo ahadi aliyoiweka akiwa Tabora kwenye kampeni kwamba wanafunzi watapewa mkopo bila ya ubaguzi. (Sio mategemeo yetu kuona wanafunzi wanaacha chuo kisa serikali imeshindwa kuwahudumia)

*Mpekuzi* nimemaliza sasa ni zamu ya viongozi wenu mliowachagua kuwatetea.

[emoji767] Ole-Mpekuzi
UDSM
 
Kwa mtu aliye makini ataelewa kwamba kinachofanyika sio tuu kupunguza wanafunzi wasio na sifa bali pia kubana matumizi kwa kuwa lipo tatizo la ukata wa fedha.nashindwa kuelewa how cimes mtu amesoma mpaka sasa yuko mwaka wa mwisho then unakuja kuterminate mkataba wake kwa vigezo vya mwaka huu wakati vigezo vilivyotumika kumkopesha ni vingine kabis???bodi ingekuwa na hekima na busara wangedeal na hao wanaoingia na wala sio hao wanaoendelea kwa sababu sio kwamba watapata loss kwa continuous students since nao wakimaliza na kuajiriwa watakuwa wanakatwa mishahara kurudisha mikopo yao waliyokopa na bodi will only get benefit itakayowawezesha kukopesha wanafunzi wengi zaidi kwa miaka ya masomo ijayo.ninachojiuliza ni kuwa wakishaterminate then hizo hela watarudishiwaje na mnufaika??au hawajui sheria za kuvunja mkataba??aliyeleta hii plan sio siri ni jipu lingine!
 
yani nimeishangaa sana hiyo dodoso mpaka nimeishiwa pozi mmmmmmmmh!!!!
 
Maagizo yanatoka juu,ukihoji tu hauna kazi. Ndio maana unaona kuna vitu vinafanywa vya kijinga sana
 
Kwa mtu aliye makini ataelewa kwamba kinachofanyika sio tuu kupunguza wanafunzi wasio na sifa bali pia kubana matumizi kwa kuwa lipo tatizo la ukata wa fedha.nashindwa kuelewa how cimes mtu amesoma mpaka sasa yuko mwaka wa mwisho then unakuja kuterminate mkataba wake kwa vigezo vya mwaka huu wakati vigezo vilivyotumika kumkopesha ni vingine kabis???bodi ingekuwa na hekima na busara wangedeal na hao wanaoingia na wala sio hao wanaoendelea kwa sababu sio kwamba watapata loss kwa continuous students since nao wakimaliza na kuajiriwa watakuwa wanakatwa mishahara kurudisha mikopo yao waliyokopa na bodi will only get benefit itakayowawezesha kukopesha wanafunzi wengi zaidi kwa miaka ya masomo ijayo.ninachojiuliza ni kuwa wakishaterminate then hizo hela watarudishiwaje na mnufaika??au hawajui sheria za kuvunja mkataba??aliyeleta hii plan sio siri ni jipu lingine!
Utaifa ndio sifa ya kwanza ikifuatiwa na ufaulu.

Ikitokea nyingine ni ubaguzi wa wazi wazi. KATAENI.
 
Back
Top Bottom