Dodoma: Zaidi ya bilioni 11 zatumika kulipa wanufaika TASAF

Dodoma: Zaidi ya bilioni 11 zatumika kulipa wanufaika TASAF

Nipe Maji

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2025
Posts
335
Reaction score
190
Billion 11,123,585,402.18 zimetumika kuwalipa wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini (TASAF) kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Takwimu hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mhe. Rosemary Senyamule wakati akifungua kikao kazi cha tathmini ya utekelezaji ya mpango huo.

‘’Serikali ya awamu ya 6 kwa kushirikiana na wadau wengine inaendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya TASAF ambapo katika kipindi cha Julai 2024 hadi April 2025, Mkoa umepokea Tsh. 11,123,585,402.18 kwaajili ya kulipa walengwa, usimizi na ufuatiliaji wa Mpango.

Kadhalika, Senyamule amesema Serikali inaanda mpango mzuri wa kuzitambua kaya hizo ‘’Ni matarajio ya Serikali kuwa katika tathmin ijayo walengwa wengi watakuwa wamekidhi vigezo ili kutoa nafasi kwa walengwa wengine kunufaika na mpango huu katika awamu nyingine zinazokuja’’, Mhe. Senyamule

Hatahivyo Mkuu wa Mkoa huyo amewaagiza wataalam wa Halmashauri kuendelea kutoa elimu ya ujasiriamali na usimamizi wa miradi kwa walengwa wanaonufaika na fedha hizo ili zitumike kuanzisha miradi ya kiuchumi itakayowaongezea kipato.

Kwa upande wake Mratibu wa Tasaf Mkoa Bi. Josephine Paschal ametaja njia zinazotumika kuwalipa fedha wanufaika hao,ambapo kuanzia Julai hadi Aprili 2025 kaya 45,771 zimenufaika. Kati ya hizo, kaya 26,275 sawa na 57% zimelipwa fedha mkononi, na kaya 19,474 sawa na 43% zimelipwa kwa njia ya benki na simu ( E- pay) lakini Msisitizo wa TASAF ni kuhakikisha kaya zote zinalipwa kwa E- Payment”, Amesema Bi. Josephine

Aidha Bi. Josephine amesema kupitia Mpango huo kaya 45,771 za Walengwa, wamepatiwa mafunzo ya Ujasiriamali yanayotolewa na wataalam katika kila dirisha la Uhaulishaji huku lengo likiwa ni kusaidia kaya hizo kuibua miradi midogo itakayowawezesha kuongeza kipato chao.
1747372678177.png
Screenshot 2025-05-16 081710.png
 

Attachments

  • Screenshot 2025-05-16 081710.png
    Screenshot 2025-05-16 081710.png
    311.7 KB · Views: 16

Similar Discussions

Back
Top Bottom