Magazetini
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 593
- 1,712
Habari waungwana,
Leo habari kubwa ni mkutano mkuu 'Maalum' wa chama cha mapinduzi ambao cheche zake zilianza jana kwa makada kadhaa kupewa adhabu ikiwemo kuondolewa chamani. Tuwe sote pamoja nikujuze yanayojiri katika mkutano mkuu maalum wa chama cha mapinduzi.
=======
Akizungumza mbunge wa Nzega, Hussein Bashe amegoma kuzungumzia yeye kushikiliwa na polisi hapo jana na kusema suala hilo kamuachia katibu mkuu wa chama hicho, Abdurahman Kinana. Alipoulizwa kama ana hofu ya kutimuliwa chamani, amedai hana hofu hiyo kwani hayo mambo hufanyika kwa utaratibu.
Katibu wa uenezi wa chama cha mapinduzi, Humphrey Polepole amesema CCM inatarajia kujenga chuo kikuu kwa ajili ya kufundisha makada wa chama hicho.
Kinachoendelea kwa sasa ni utambulisho wa wageni mbalimbali waliohudhuria hasa mabalozi wa nchi mbalimbali waliofanikiwa kufika katika mkutano huo, pia mwakilishi wa msajili wa vyama vya siasa nchi.
Pia wametambulishwa wadhamini wa chama cha mapinduzi, wake za wake wa viongozi ikiwemo Karume, Kawawa, Ali Juma, Salma Kikwete na wake wa viongozi wa sasa ikiwemo Mary Majaliwa, Mwanamwema Shein, Janet Magufuli.
Yupo pia Pandu Kificho, Anna Makinda, manaibu makatibu wakuu wastaafu.
Wajumbe wote wanaotakiwa kuhudhuria ni 2380, watano wametoa taarifa na wengine 19 kwa sababu nyingine, waliohudhuria ni wajumbe 2,356 sawa na asilimia 99.8.
Anaeongea kwa sasa ni mwenyekiti wa CCM, Dkt Magufuli
Magufuli: Kabla sijaanza hotuba yangu, aje kwanza mzee Kikwete. Nilitaka nizungumze neno moja, najua wote tumekaa hapa kwenye ukumbi mzuri, kuna watu walifanya kazi kufanikisha na moja ya wato ni mheshimiwa Jakaya Kikwete. Ukumbi huu pamoja na kuwa alishiriki kuujenga alikuja na kuufungua, naomba wajumbe wa mkutano mkuu ukumbi tuuite Kikwete Hall.
Tumekutana hapa kwa kazi maalum ya kufanya marekebisho madogo kwenye katiba ya chama chetu.
Tumeeendelea kudumisha amani nchini, vitendo vya kutishia usalama tumedhibiti, tumezidisha mapambano dhidi ya madawa ya kulevya, navipongeza vyombo vya ulinzi na usalama. Muungano wetu unazidi kuimarika, viongozi mbalimbali wa nje wametembelea nchi yetu na sisi tumetembelea nchi mbalimbali pia tumefungua balozi mpya sita kwenye nchi mbalimbali.
Uchumi tunaendelea vizuri na nchi yetu inashika nafasi ya pili kwa ukuaji wa uchumi barani Afrika. Tunataka angalau tukusanye trilioni 1.8 na naamini tutafikia huko kwa kudhibiti mianya yote ya ukwepaji kodi.
Tumeanzisha kitengo maalum cha mahakama na kilianza kazi November kushughulikia rushwa kubwa, wakti wa kuanzisha kitengo hiki, wale wenzetu walitoka nje, nawapongeza sana wabunge wa CCM kwa kusimama Imara mpaka kuanzishwa.
Barabara zimekamilika na nyingine zinaendelea kujengwa na kuhakikisha makandarasi wanalipwa, wakati wa kampeni tuliahidi kushughulikia foleni, tumeanza TAZARA na tutafata ubungo kwa kuweka interchange Ubungo.
========
Mafufuli: Kama mjuavyo, chama chetu kina utamaduni wa kujitathmini. Tunahitaji mpitie mabadiliko ya katiba yanayopendekezwa na ikiwezekana myapitishe.
Mabadiliko yanalenga kuboresha mfumo na muundo wa chama chetu, wa sasa una mapungufu jama umetuletea mafanikio kwa miaka 40. Kuna watendaji wanafanya majukumu yanayofanana na kugongana kimaamuzi. Pia kuna watu wanafanya maamuzi lakini nafasi zao hazipo kikatiba.
Lengo la kuongeza ufanisi na utandaji wa chama kwano ufanisi hushuka sana hasa baada ya uchaguzi pia hata wakati wa uchugu kuna watu wanakosa heshima kwa viongozi, kuna watu waliimba wana imani na nani nani..
Watumishi mamluki wasiruhusiwe ndani ya chama chetu, asubuhi CCM, jioni chama kingine.
=>Watu walikuwa wanawapiga vita wanaofaa kuwa viongozi kwa kuwa hawana pesa! Tunataka wanachama wenye uwezo ndo waongoze chama.
=> Licha ya utajiri wa rasilimali tulio nao CCM, tumeendelea kuwa ombaomba. Hata wengine tunaowaomba hawana hata hadhi hiyo!
=> Nafahamu wamo wengine wataguswa na mabadiliko haya na wengine wameguswa jana lakini ni maslahi ya chama.
=>Tunataka kujenga uwezo wetu wa kitaasisi. Yeyote atakayejaribu kujinufaisha na rasilimali za chama atawajibishwa mara moja
- Napenda kuwahakikishia kuwa Serikali inahamia Dodoma kweli na tumedhamiria, utekelezaji umeshaanza!
- Nami najipanga kuhamia Dodoma. Lengo letu la kuhamia Dodoma ifikapo 2020 litatimia kwakuwa tumeshaamua kufanya hivyo
- Naomba ndani ya CCM naomba tuchague Viongozi waadilifu, si kwa uwezo wao kifedha. Kwenye uongozi wangu rushwa haina nafasi!
Anayeongea kwa sasa ni katibu mkuu wa chama cha mapinduzi, AbdulRahman Kinana,
- Sina shaka hata kidogo, watanzania wataendelea kuiamini CCM. Tathmini hii ilifanywa chini ya Rais Mstaafu, Jakaya M. Kikwete
- Mabadiliko haya yanatokana na Wana CCM, hayajatoka kwa mtu wala kikundi cha watu flani. Ni uamuzi wa chama!
- Mabadiliko haya ndani ya @ccm_tanzania hayalengi mtu wala kikundi cha watu. Kuna watu wanafanya upotoshaji wa makusudi!
- Mabadiliko ya Katiba ya CCM haya ya sasa ni ya 16. Tunataka kuongeza ufanisi na kutoa fursa zaidi ya kuwa karibu na wananchi
- Mwenyekiti ameshatupa uhakika; wana CCM msisite kuzisimamia Serikali zote mbili. Hatuko peke yetu, vyama vinauza sera!
- Tunataka kupunguza urasimu na umangi meza ndani ya CCM. Viongozi wawajibike kwa wananchi, wasikae ofisini tu!
- Tunataka vikao vichache vya chama(CCM) na vyenye tija kwetu. Hili si jambo jipya! Wingi si hoja, tunatafuta tija
- Katika CCM, Ilifika wakati kunakuwa na vikao vinakaa nje kushughulikia vikao vya ndani
- Tunataka kupunguza utitiri wa vyeo kwa mtu ndani ya CCM. Wengine watabaki na vyeo vyao kutokana na nafasi zao!
- Kikwete: Nashukuru kwa heshima kubwa niliyopewa na Mhe. Rais Magufuli (kwa Ukumbi kupewa jina lake)
- Katika upinzani wa sasa, CCM tusingekuwa na Katibu Mkuu kama Kinana sijui ingekuwaje! Amekuwa akiongoza Kampeni za Urais
- Kinana ni mtu mtambuzi sana! Naamini atapewa heshima anayostahili na chama!
- Mabadiliko yanayofanywa sasa yanalenga kuboresha ufanisi ktk chama(CCM). Kulikuwa na changamoto kubwa kuendesha chama hiki
- Kama wanachama wote milioni 8.4 wangekuwa wanalipa ada kila mwaka tungepata Bil 12. Ila, tulikuwa tunapata milioni 500 tu
- Lazima tukubali, mabadiliko na kupunguza idadi ya vikao haikwepeki. Nilimkabidhi tathmini ya chama tuliyoifanya Mwenyekiti