Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 1,114
- 2,154
Kwani walikuwa awajui kwamba kuna wanachama wao wameanza kampeni? Lakini mbona kama njia zao maana tumeshuhudia baadhi ya viongozi wakubwa nao wakijipigia kampeni mapema!
================
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa kimepiga marufuku Wanachama wanaoanza kufanya kampeni mapema, kwani watakaokiuka na kuanza mapema watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa kanuni za chama hicho.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Daudi Yassin, katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Iringa, ambacho kimefanyika katika Ukumbi wa CCM Mkoa.
"Tukawaeleze Wanaccm tuache tabia ya kuanza kampeni kabla ya Wakati tuheshimu katiba na kanuni" amesema Yassin
Yassin ameongeza kwa kuwataka Viongozi wa CCM kutanguliza masilahi ya chama mbele na siyo masilahi binafsi jambo ambalo litapelekea kukivuruga Chama.
Aidha kupitia Kikao hicho Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa kimemtunuku zawadi Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (MNEC), Asas, kwa mchango wake mkubwa katika kujenga chama na kufanikisha ushindi wa kihistoria wa asilimia 99.99 kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024.
"Sisi sote ni mashahidi, ambao tumekuwa tukishuhudia jitihada za makusudi zinazochukuliwa na Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa za kuhakikisha CCM inaendelea kushika hatamu kwa Mkoa wetu wa Iringa, kwa kutambua mchango na jitihada hizo kikao hiki Cha Halmashauri kuu kinamtunuku Tuzo maalum ya kumpongeza na kumshukuru kwa moyo wake wa uzalendo wa kuipigania CCM" amesema Yassin