Dodoma: Wabunge wapinga kunyanyaswa na polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dodoma: Wabunge wapinga kunyanyaswa na polisi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Nov 10, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Nov 10, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Wabunge wang’aka
  Wabunge jana waligeuka mbogo wakiitaka Ofisi ya Spika, kuchukua hatua kukomesha kile walichokiita unyanyasaji unaofanywa dhidi yao na polisi katika matukio ya kuwakamata wanapohusishwa na uvunjaji wa sheria.

  Habari kutoka ndani ya kikao cha kutoa mwongozo kwa wabunge kuhusu Mkutano wa Tano wa Bunge kilichofanyika jana katika ukumbi wa Pius Msekwa, Dodoma zinasema kuwa wabunge waliochangia hoja hiyo walisema ukamataji unaofanywa na polisi kwa wabunge unaonekana kudhamiria kuwadhalilisha badala ya kusimamia sheria.

  Kwa mujibu wa habari hizo, Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Pauline Gekul ndiye aliyeibua hoja hiyo huku akiitaka Ofisi ya Spika kuchukua hatua za kuwaondolea wabunge adha hiyo na kadri mjadala ulivyoendelea, suala hilo liliungwa mkono na wabunge wa kambi zote.

  “Aliposimama Gekul kuzungumza baadhi ya wabunge walidhani kwamba pengine ni hoja ya wapinzani kuwatetea wabunge wa Chadema waliokamatwa Arusha, kwa hiyo baadhi yetu walikuwa kama wanaguna vile, lakini baadaye ilibainika kwamba kamatakatama hiyo imewakumba wabunge wote wa upinzani na wa CCM,” alisema mbunge mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe.

  Wabunge wengine waliotajwa kuzungumzia hoja hiyo ni Livingstone Lusinde wa Mtera (CCM), Murtaza Mangungu- Kilwa Kaskazini (CCM), Israel Natse- Karatu (Chadema) na Christopher Akunaay- Mbulu (Chadema).Kwa mujibu wa taarifa hizo, wabunge hao walisema kwa nyakati tofauti kwamba mbunge anapotenda kosa anaweza kuarifiwa kwamba anahitajika kituo cha polisi na yeye kwenda bila kushurutishwa.

  “Mbunge hawezi kutoroka au kuwakimbia polisi, dhamana aliyonayo ni kubwa kwanza wapigakura waliomchagua, Bunge kama taasisi na hata chama chake cha siasa, sasa huwezi kusema unamtafuta mbunge kama anavyoweza kumsaka mhalifu mwingine ambaye hatambuliki. Huu ni udhalilishaji,” alisema mbunge mwingine ambaye pia aliomba jina lake lihifadhiwe.Spika Anne Makinda aliahidi kuwasiliana na vyombo vya usalama ili vifuate utaratibu wakati wanapotaka kuwakamata wabunge kutokana na makosa mbalimbali wanayofanywa.

  Miongoni mwa taratibu ambazo wabunge wamekuwa wakitaka zifuatwe ni Ofisi ya Spika kuarifiwa kabla ya kukamatwa na kuitwa kwenda polisi wenyewe badala yakufuatwa na idadi kubwa ya askari.

  Hata hivyo, Spika aliwataka wabunge kwa upande wao kuwa makini kwa kuzingatia sheria na uhusiano mwema na vyombo vya dola ili kuepusha misuguano baina ya mihimili ya Bunge na Serikali.
  Habari hii imeandikwa na Peter Saramba, Arusha, Hussein Issa, Dar na Neville Meena, Dodoma.

  Mwananchi
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Nov 10, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  KATIKA MFUMO WA UTAWALA WA SHERIA POLISI WALA HANA MADARAKA YA KUAMULIA HATIMA YA MIKUSANYIKO ILA TU KAZI YAO NI KUTOA ULINZI IMARA WAKATI WOTE

  Kwa kawaida, katika mfumo wa utawala wa kisheria kokote duniani Polisi haina Mamlaka yoyote kisheria Kupiga MARUFUKU Mikutano, Mijumuiko wala Maandamano yoyote ya kuonyesha hisia z KUTOKUAFIKI JAMBO lolote bali tu lao ni kutoa ulinzi ili kusitokee uvunjifu wa amani.

  Mabadiliko Tanzania hayazuiliki tena sana sana ni watu wachache tu kujichagulia tu kujipotezea wakati. Change is here and NOW; kuendelea kuzuia mtokoto wa chungu cha ugali mwishowe mpishi fedhuli hujiunguza mwenyewe bila kujielewa tena!!

  Nguvu ya Umma sasa kutikisa kila kona ya nchi na maafisadi wengi kutondoka huku akaunti na mali nyinginezo kuwekewa barafu huko Ughaibuni si kipindi kirefu sana.

  Na wale wenye ubize kutafuta makao nje ya nchi hivi sasa tutawaumbueni si kipindi kirefu sana tu. A de jure one-political party system of police to oversee the smooth running of a pluralistic political system - what a paradox!!!

  Indeed, a sweeping police force systems overhaul is long overdue in our country in order to keep pace with changing times and tastes.
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Nov 10, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Sheria zilizopo Tanzania haziwapi polisi mamlaka ya kuruhusu au kukataza mikutano au maandamano. Sheria zinaelekeza polisi kujulishwa juu ya mikusanyiko au maandamano kwa ajili ya ulinzi. Hivi hawa polisi wanajiongezea vipengere vyao visivyohakikiwa na bunge?
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Nov 10, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  UTETEZI WA UBINADAMU, HAKI NA UTU WA MTANZANIA WALA SI LELEMAMA; WAVUJAJASHO TUSONGE MBELE ZAIDI LEO ILI TUISHI KAMA WATU KESHO.

  Sheria za nchi zinapoanza kutekelezwa kwa KUBAGUANA hapo ndiopo wenye akili wanapogutuka na kugundua kwamba tayari Mfumo wa UTAWALA WA SHERIA umeshawekwa kando kupisha Mfumo wa Utawala wa MTU.

  Na matokeo ya utaratibu kama huu ndio haswa unaofungulia milango giza nene la taifa linaloitwa UDHALILISHAJI WA UTU wa Wa-Tanzania na ubinadamu ule wa Mwalimu Nyerere kubakia tu ka-msamiati wa kale.

  Nguvu ya Umma tayari tunapinga hayo yote bila kurudi nyuma hata chembe.  [​IMG]

  Remand prisoners from Kisongo Prison on March 13 refused to disembark from their truck "Black Maria" to attend court proceedings. They were protesting the delay of in hearing their cases. Their anger was fueled by the recent release on bail of former Regional
  Commissioner for Tabora whose prosecutors have lowered his charge from murder to manslaughter. Some of the remandees claimed to have been remand jail for more than 10 years.

  (Photo by Edward Selasini)
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Nov 10, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Watu wametulia katika mikusanyiko yao halafu polisi kuvizia na mabomu hii sheria iliwekwa lini? Uharibifu gani katika mkusanyiko wa viongozi wa Chadema na wananchi uliofanyika hadi polisi kutumia silaha kuwatawanya?
   
 6. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #6
  Nov 10, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  KAMANDA LEMA TOKA KIJANA MHANGAIKAJI TU MITAANI ARUSHA HADI KUJAZA PENGO KUU LA 'MWANA NA NGUZO IMARA KWENYE SIASA ZA KITAIFA'

  Miongoni mwa mafanikio makubwa sana kupatikana chadema ni kule kuwajema viongozi wengi vijana lakini wenye mitazamo na siasa za kitaifa zaidi huku tukiwakumbuka baadhi ya wanasiasa wetu ambao wao kwao taifa lina maana sawa na kijiji alikozaliwa tu.

  Na ni shida kubwamno kwamba viongozi wa aina hii, ambao hasa ndio walioangusha utawala wa Mwalimu Nyerere kutoweza kufanikiwa licha ya ni njema aliokua nayo, bado wako wengi mno nchini japo katika umri ule wa kusinzia tu.

  Inashangaza sana jinsi Dr Slaa alivyowajenga Kamanda Lema kutoka kwa ukada wa mbunge kwa mara ya kwanza hadi kuwa mmoja kati ya watu gumzo ya taifa kule siasa za kitaifa zinapozungumzwa na watu kutulia kumsikiliza.

  Viongozi wengine nyota hivi sasa chini huyu kocha mahiri ni pamoja na Mhe Halima Mde, Freeman Mbowe, Zitto Kabwe, John Mnyika, Chiku Abwao, Mchungaji Msigwa, Tundu Lissu, Heche, Wenje, ...

  Udhalimu na ukandamizaji wa haki za binadamu hokomaza zaidi wanasiasa na pia huwafanya kusaidia kuzaliwa kwa KATIBA MPYA iliyo bora zaidi; na ndio maana tunaongeza umakini wetu zaidi Bungeni Dodoma tangu sasa kumulika kiundani zaidi swala la Muswada wa Katiba Mpya inayopelekwa huko hivi sasa.
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Nov 10, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Ukitaka kumjua kiongozi mwenye uchungu wa kweli na nia njema kwa nchi yake, utamtambua kataika kujitoa kwake bila hofu kwa ajili ya ukombozi wa watu wake. Mchumia juani hulia kivunili. Tuwe pamoja nduguzangu, maana hata hizi key board nazo ni silaha madhubuti sana ya kuhamasisha, kuelimisha na kujenga mshikamano katika jamii.
   
 8. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #8
  Nov 10, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,335
  Likes Received: 22,187
  Trophy Points: 280
  Wenye taarifa za maandamano anijulishe, mi nipo hapa Manzese nayangoja kwa hamu.
   
 9. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #9
  Nov 10, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  UJASIRI KATIKA KUTETEA HAKI NA UTU WA MTANZANIA KWA GHARAMA YA KUSWEKWA NA 'WAOKOLONI WEUSI WA CCM YA LEO' KIZUIZINI KISONGO

  Kamanda Lema, Mbunge kijana mdogo aliyeshangaza taifa zima kwa ujasiri wake wa ajabu kule katika kutetea KILE ANACHOKIAMINI sana na kuthamini mno moyoni; UTETEZI WA HAKI, UBINADAMU NA UTU wa Watanzania kwa ujumla wetu bila kujali tofauti zetu za kiitikadi.

  [​IMG]

  Gharama wanazolipa kule kizuizini Kisongo kule Arusha ni kwa faida ya Watanzania wote kuondokana na Wakoloni weusi wachache waliomo ndani ya CCM hii ya kileo.
   
 10. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #10
  Nov 10, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,575
  Likes Received: 1,942
  Trophy Points: 280
  Mbona hawazungumzii kuhusu wananchi kunyanyaswa na polisi?Wai kila siku maslahi yao tuu!Mishahara,marupurupu nk basi.

  Kwa kutetea maslahi yao wakishachaguliwa ndo kazi yao.Wengi wao at least.
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  Nov 10, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nasema kilichokua ni JAMBO TU KWA JIJI LA ARUSHA hivi sasa kulipuka kila pembe ya nchi kutokana na mkondo waliouchukua hivi sasa watawala wetu.

  Safari ya mbali ndio hivyo imeanza kwa hatua ya kwanza na ya uhakika mno. Sasa baada ya Kisongo ni madai ya KATIBA MPYA nchi nzima na kupinga kulipwa kwa kampuni hewa ya DOWANS.
   
 12. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #12
  Nov 10, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0


  Taratibu mkuu.mambo makubwa yanaandaliwa.mbuyu ulianza kama mchicha.
   
 13. e

  evoddy JF-Expert Member

  #13
  Nov 10, 2011
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 302
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Utetezi juu ya wabunge kutokamatwa na polisi ni kwamba kwa sheria za tanzania uwezi kumkamata mtu kama hajatenda jinai au mada tatizo kubwa la polisi Tanzania ni kushindwa kufuata sheria badala yake wanatekeleza matakwa ya viongozi waliomadarakani.

  Ukiangalia kesi nyingi za Mh Lema hazina mantiki,mara katoka mahakamani kasindikizwa na wafuasi wake polisi wanasema walikuwa wanaandamana na kuwahutubia bila kibali lakini polisi hao hao wanasaua walivyokuwa wakitoa ulinzi kwa Mh Sendeka alipokuwa na kesi na Emiliya umati wa watu kutoka Simanjiro walikuwa wanajaaa Mahakamani na wanatembea kwa miguu kuelekea Simanjiro,hapo polisi hawakuona kama maandamano bali matembezi tu .Watanzania tunajua mkakati wa kuidhoofisha CHADEMA na Wabunge wake pamoja na viongozi wake ,polisi kama CCM B hawatashinda kamwe ila nguvu ya UMMA ndiyo itashinda
   
 14. k

  kilolambwani JF-Expert Member

  #14
  Nov 10, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sisi wachunguzi wa mambo ya KISAIKOLOJIA tunajua uadui uliopo baina ya polisi na wabunge ni tofauti ya kipato na hawa wabunge linapokuja suala la kudai maslahi nje na ya kwao hawawi SERIOUS na matokeo yake watu wanajenga chuki juu yao. Kwahiyo inapotokea nafasi ya kuwashughulikia watu wanamalizia hasira zao hapo. Mishahara mikubwa, marupurupu kibao, mikopo ya magari, lakini polisi na 130,000.= unategemea nini. Maoni yangu nawasilisha.
   
 15. t

  tumpale JF-Expert Member

  #15
  Nov 10, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 201
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  polisi inajidhalilisha
   
 16. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #16
  Nov 10, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Lakini iweje wanaonyanyaswa ni wa upande wa upinzani? kwani wao ndo wana maslahi zaidi ya wabunge wa CCM. Katika hili ni kwamba polisi wameishajitolea kutokuwa na utu; utaratibu wao wa kazi ni mbovu - kitendo cha kutii sheria / amri ya mkuu wako wa kazi pasipo kupewa mwanya wa kutafakali ni kudharirishwa. Wao wanafanya kazi kama maroboti tu! Siku wakipata kiongozi mwenye kichaa ndo tutawajua - hizi ni rasharasha ndg zanguni. Tujipange sawasawa kulifumua jeshi la polisi na kulijenga upya.
   
 17. thereitis

  thereitis JF-Expert Member

  #17
  Nov 10, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 297
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  hawa polisi wakiendelea kutudhalilisha dawa yao ni kuwapiga mawe huku mtaani ambapo hawatakuwa na bunduki.
   
Loading...