Dodoma: Tumaini linalodidimia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dodoma: Tumaini linalodidimia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAKOLE, Feb 14, 2012.

 1. MAKOLE

  MAKOLE JF-Expert Member

  #1
  Feb 14, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 601
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Nilibahatika kuwepo hapa Dodoma kwa muda wa majuma manne. Kwa kipindi nilichokuwepo katika mji huu wa Dodoma yapo mambo mengi ambayo kwa namna moja ama nyingine na pamoja na kuwa yanajulikanwa na baadhi ya wenye mamlaka katika nchi hii lakini bado iko haja ya Watanzania wayafahamu.

  Hakika mji huu na wakazi wake wanashuhudia historia yenye kuuma na kutia uchungu mkubwa. Inawezekana pia Labda kwa sababu hii ndio maana Serikali bado kwa yakini haijaamua kuhamia rasmi Dodoma kama makao makuu yake. Kwa hili naomba kuwaalika watafiti wa masuala ya kisiasa kulitafiti hili la uhusiano kati ya nitakayoyaeleza na dhamira ya serikali ya kuhamishia makao yake makuu hapa Dodoma.

  Nimeshaondoka Dodoma, walakini, bado kila nukta niwapo safarini naikumbuka hali ya aibu niliyoiona Dodoma, hakika yataka moyo mgumu kuweza kuvumilia yaliyopo mjini hapa.

  Dodoma yapo haya yafuatayo:-

  1. Asilimia kubwa sana ya wakazi wake ni MASIKINI wa kutupa, nadhani kila mtanzania analifahamu hili. Sio lengo langu kuwafahamisha suala hili. LAKINI


  2. Asilimia kubwa ya ombaomba wa Dodoma ni watoto wadogo sana ambao kwa umri wao walitakiwa wawepo shuleni.

  3. Watu hawa hawana makazi ya kudumu, hali hii hata katika mji wa Dar es Salaam pia ipo, kwani ifikapo usiku wengi wao hulala pale jua linapowachwea.

  Nimepata fursa ya kutembelea sehemu inayoitwa Ng'ong'ona. Hapa ni jirani sana na kilipo kitivo cha Elimu Chuo kikuu cha Dodoma. Wanachuo wengi hufika kijijini hapo kupata mahitaji yao, hasa vyakula kwani kuna mlundikano wa migahawa mingi sana. Hapa ndipo nilipopata hisia za uchungu ambazo kwazo, nimeamua kuzitupa kwa Watanzania wenzangu:

  1. Wengi wa wahudumu hapa ni watoto ambao pia ni wanafunzi wa Shule ya Msingi ama Sekondari ya Ng'ong'ona. Hawa huwa wanapanga siku za kunda shule na siku za kwenda kazini kutoa huduma kwa wanachuo kama vibarua..

  2. Watoto wengine, kwa kukata tama ya hali ya maisha nyumbani huwa wanafika hapo ili kupata riziki zao. HAKIKA watanzania : Hawa hujitolea kuosha vyombo vinavyotumiwa kwa chakula na wateja kwa malipo ya AMA kula MABAKI YA VYAKULA VILIVYOBAKIZWA NA WATEJA au KUKWANGUA SUFURIA ambazo hupikia na kuloekewa maji ili zilainike, hivyo wao ndio wanapata ujira wao.

  3. Kundi kubwa la watoto na wazee wao, hujongea maeneo ya mikahawa iliyopo ndani ya chuo mida ya chakula na husubiri hapo hadi pale watakapoitwa kwenda kuchukuwa mgao wao. Mgao huo aghalabu huwa ni "MAKOMBO" yaani mabaki ambayo yastahili wapewe mifugo kama mbwa, kuku nk. Wao hupewa huku wakiwa katika foleni.

  4. Kwa watoto watukutu utawakuta badala ya kufikisha chakula nyumbani kwa kuwa kinasubiriwa na jamaa zao, wao huanza kutafuna mifupa njiani kwani wanajua fika kuwa watakapoifikisha nyumbani hawatapata mgao wa mfupa (kwa wao huo ndio mnofu).

  5. Nimejaribu kumhoji kijana wa darasa la 3 hapa Ng'ong'ona p/r anasema kuwa wao wamezoea kula mara moja tu kwa siku, hivyo inawalazimu kuacha kwenda shule na kuranda randa ili apate riziki.

  Hawa ndio watanzania ambao wakifeli mitihani tunalalamika, na pengine tunawalalamikia walimu.

  Hawa ndio tunawaandaa waje kushika madaraka ya nchi baada ya sisi, waje kupambana na changamoto za mabadiliko ya dunia ya sasa.
  Hii ni sehemu ndogo ya watanzania walioko msambweni, hapa ni eneo moja tu - Dodoma.

  Tunawaandaa hawa wanafunzi katika mifumo dhaifu, Halafu tunaweka vikwazo katika elimu ya juu kuwa MIKOPO ITATOLEWA KULINGANA NA VIPAUMBELE, SAYANSI 100%. SIO HALALI, SIO HALALI.

  Yatupasa kwa pamoja tupige kelele kwa vyombo husika, Jamii hii isaidiwe!

  NAWASILISHA.
   
 2. m

  msambaru JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Wana JF na yeyote mwenye uelewa au aliyewahi kupita dodoma, ni aibu kubwa kwa mji ambao tunauita makao makuu ya nchi kuwa na kituo cha mabasi ya kwenda mikoani kama njia ya kupita ng'ombe kikwetu tunaita ifanda, mi nadhani tungekubaliana kuwa ni mji mkuu wa ccm ili walishane hilo vumbi mpaka washibe. Plz plz plz sirikali ya ya mkoa wa idodomia ondoeni aibu hio, nendeni mkalie hata kwa waziri mkubwa.
   
 3. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #3
  Feb 14, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 453
  Trophy Points: 180
  One day nilikaribishwa na vumbi jekundu pale, sina hamu!!, ikabidi nijibanze pale petrol station round about kusubiri ndugu yangu anipokee!! lol
   
 4. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #4
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Umesema ukweli, lakini kimsingi chama kinachotawala Dodoma ndiyo chanzo cha umasikini. Inawezekanaje makao makuu ya thithiem iwe ndiyo mahali pa kulaza vijana omba omba? We nenda pale kwenye jengo lao utawakuta wakati wa usiku wamejazana wamelala.
  Hata hivyo, Kenyata aliposema, "Ukimkuta mtu amezubaa, nyonya mpaka aanguke." Nadhani msemo huu thithiemu wanautumia hapa Dodoma. Watu wa hapa wamelala na hivyo thithiemu wanawanyonya. Na sasa wameshaanguka. Kimsingi Dodoma itabaki hivi mpaka pale hawa watu watakapoacha uzubaifu wao. Kuna kabila mbili kubwa hapa, Wagogo na Warangi. Wagogo si watu wa kupenda kazi, kilimo chao si cha kisasa na pia si watu wenye bidii hata hivyo kuna baadhi yao wana bidii. Warangi wao hufikiri ni waarabu. Wanafuata uislamu kama vile wapo maka, kazi yao ni kufungua madrasa na kushinda huko. Wazazi wa vijana hawana msukumo kabisa kwa vijana wao kukazana kusoma, ila hukazania elimu ya dini na wangine huthubutu hata kusema kwamba kosoma elimu dunia ni dhambi. Wingi wao huamini uchawi na ni washirikina wa kutupwa. Ukifuatilia wengi wao wana majini na hayo majini yanawasumbua kila siku. Ndiyo maana ukipita barabara za Chamwino, Chinangali, Chang'ombe ambapo Warangi wengi huishi mara nyingi utakutana na matakataka yaliyotupwa kwenye njia panda. Kwa upande mmoja Warangi hujishughulisha, lakini kutokana na kukosa elimu fedha zao huishia kwa waganga au huwekeza katika mambo ambayo hayawaletei ustawi wa maisha yao. Pia Warangi hupenda sana kuoa wake wengi ambao huzaa watoto wengi. Mara nyingi wazazi hasa baba hushindwa kuwa karibu na watoto. Hii hufanya wasichana wengi wa Kirangi kuingia katika tabia hatarishi hasa umalaya.
  Katika jamii ya namna hii huwezi kukuta maendeleo. Na taifa hili lisipofanyiwa marekebisho, ni matumaini yangu kwamba ipo siku litakufa kabisa.
  Sasa ukiangalia hali ya umasikini wa kupindukia kwa Wagogo ambao ndiyo wengi sana hapa Dodoma umekuwa ndiyo mtaji wa thithiemu. Kwani wao huwapa kanga moja moja na tisheti na kofia na kwa hakika huwapa kura wagombea wa thithiem. Na kwa vile Warangi hupenda sana kujitambulisha kama waarabu, thithiemu hutumia njia ya dini kupata kura zao. Utasikia kiongozi amekuja Dodoma na ametoa mikeka kadhaa kule Chamwino na Chinangali, huyo tayari ameshapata kura za Warangi. Jambo ambalo sasa watafanikiwa zaidi ni huu udini walioupandikiza hasa kwa vyama pinzania. Mwaka 2005 kurudi nyuma cuf iliambatanishwa na uislamu na sasa Chaema imeambatanishwa na Ukristo.
  Kwa hali hii Dodoma itabaki nyuma zaidi.
   
 5. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #5
  Feb 14, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Kinachohitajika hivi sasa katika nchi yetu ni kubadili kabisa mfumo wa kuandaa bajeti na utekelezaji wa miradi ya maendeleo!
  1. Lazima serikali isitishe mara moja kuanzisha miradi mipya ili kuepuka utaratibu wa sasa ambapo miradi mipya inaanzishwa lakini inashindikana kukamilika kwa wakati kutokana na ukosefu wa fedha.
  2. Bajeti ya serikali iwe inatokana na makusanyo ya ndani na fedha ambazo serikali ina hakika za kuzipata kupitia mikopo ya ndani na kuacha au kupunguza kabisa fedha za wahisani katika bajeti hata kama zitapatikana kwa mikopo. Uzoefu unaonyesha kuwa wahisani wanatoa fedha zao kwa kuchelewa sana na wakati fulani wanatoa pungufu ya ahadi zao.
  3. Serikali ijikite katika kutatua matatizo ya wananchi maskini na kuwasaidia katika kujiwezesha.
  4. Serikali idhamirie kwa dhati kupunguza matumizi yake kwa kuondoa matumizi yasiyo kipaumbele cha taifa na pia kupunguza shughuli za kianasa kama maadhimisho mbalimbali, posho za watumishi wake na wa mashirika yake ambazo hazina tija kama posho za makalio, safari za viongozi nje ya nchi, ukubwa wa serikali nk.
  5. Serikali iwape watumishi wake vitendea kazi na fedha za kutosha ili waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu na kurudisha ari ya utendaji kazi kwa watumishi.
  Haya ni baadhi ya mabo ambayo nafikiri yakifanyiwa kazi mabadiliko kuelekea maisha bora kwa wananchi maskini yataanza kuonekana.
   
 6. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Mzee kama vipi naomba nikuulize kaswali kadogo tu.

  Umeshazunguka ktk vijiji vya mikoa na wilaya za nchii hii? Kama bado hujafanya hivyo, nakushauri usifanye hivyo maana nna uhakika inaweza ikawa ndo mwisho wa maisha yako hasa kama una BP. Mbona hiyo ya dodoma ni nafuu, zunguka mkuu nchi hii ni kubwa utalia, kweli nakwambia. Tatizo la hawa viongozi wetu wengi hawana uelewa wa kutosha wa matatizo ya watz, hasa maeneo ya vijijini, na bahati mbaya wenye hizo shida nao wanaona kama ni utaratibu wa kawaida tu wa maisha.

  Mkuu watu wanateseka ktk nchii, zunguka tu vijijini, ndo utajua kuna watz wengine wanaishi kama sio binadamu, utazimia nakwambia. hiyo ya dodoma ni chamtoto sana, tena wewe umetembelea maeneo ya mjini.

  Hofu yangu mimi na namna wanavyoendelea kuwaweka watoto wao madarakani ndo shida zitendelea kuwepo milelel maana hao watoto wao nao hawana uelewa wa shida za watz, hivyo hata ktk plans zao mambo yataendelea kuwa yaleyale................like father like son. Nchi imekwisha hii, waliokamatia hawataki kuachia na wakiachia wanawapa watoto wao...........!
   
 7. MAKOLE

  MAKOLE JF-Expert Member

  #7
  Feb 14, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 601
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mkuu kwa bahati nzuri nimepata kuzunguka vijiji vingi katika nchi hii, hii ya Dodoma yenyewe nilikuwa natokea Iringa kupitia njia ya mkato. Huko nako nashindwa kuelewa kwamba kwa miaka yote 50 iliyopita leo ndio kunajengwa barabara ya lami katika eneo muhimu la nchi. Kuna vituko vingi sana na sijajua hasa mbunge wa maeneo ya Mtera alikuwa anafanya nini pamoja na kushika nyadhfa kubwa serikalini. Lakini ushauri wako ni mzuri, tembea uone!
   
 8. mwanamapinduko

  mwanamapinduko Senior Member

  #8
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 174
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Tamisemi kuwa dodoma naona wamepata upofu hawaoni hiyo manispaa/cda wanavyotafuna mapato kwa maposho ya aina zote, badala ya kutenga hata kiduchu kukarabati huo mfano wa stand.
   
 9. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #9
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  mgogo ukishampa debe la mahindi na kimbo 3 za maharage umemaliza kazi
   
 10. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #10
  Feb 14, 2012
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,491
  Trophy Points: 280
  ... Hali ya dodoma kwa sasa ni nzuri. Kwa miaka ya karibuni, serikali iwewekeza sana ktk ujenzi wa taasisi mbali mbali. Ni mji wenye tumaini kubwa kwa siku za usoni. Laiti kama ungekuja hapa mwaka 2007, ungeandika kitabu kuhusiana na masahibu ya Dodoma. Kwa kifupi ni kwamba uwepo wa taasisi za elimu ya juu kama CBE, Mipango, St. John, Chuo cha serikali za mitaa Hombolo-ambavyo vinakuwa kwa kasi na uwepo wa UDOM, umeongeza mzunguko wa pesa na hivyo maisha ni afadhali kuliko ilivyokuwa zamani.

  Kwahiyo sio kweli kwamba dodoma inakatisha tamaa, kwa sie tuliokuwepo hapo awali, tunajua watu wa dodoma wana matumaini makubwa sasa kuliko ilivyokuwa awali.
   
 11. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #11
  Feb 14, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu ndyoko. Nimezunguka ktk nchi hii lakini Dodoma na baadhi ya maeneo ya mkoa wa Singida kuna umasikini wa kutupwa. Siku zote tunazungumzia umasikini uliopo ktk mikoa ya kusini mwa Tanzania,mimi naona huko kuna nafuu sana. Hawa jamaa bado wanalala ktk nyumba za tembe,kuna matatizo makubwa ya kupata maji na utapiamlo. Mkuu usione watu wakifika mijini hawataki kurudi kwao,wengine hali huko vijijini panatisha!
   
 12. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #12
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Chezea ccm wewe.
   

  Attached Files:

  • Acc.jpg
   Acc.jpg
   File size:
   9 KB
   Views:
   198
 13. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #13
  Feb 14, 2012
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,966
  Likes Received: 222
  Trophy Points: 160
  soga la kahawa ni zuri kwa bahati mbaya linadhalilisha jm kuwa a home of great thinkers wengi wa wachangiaji ni watu wenye aidha upeo mdogo wa mambo yalivyo au chuki dhiidi ya serikali bila sababu
   
 14. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #14
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wakazi (wenyeji) wa dom wanaishi maisha ya tabu.

  Even mailimbili pale mipango,nyumba za pembeni wanatumia maji ya kuchimba chini (kisimani),hao wapo karibu na chuo na ni wakazi wa mjini.

  Je umefika mkonze wewe?
  Chidachi?
  Mpungudzi?
  Mlowa?

  Wacha siasa hazitakusaidia,jk katajwa wapi hapo?
   
 15. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #15
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Kwa jinsi niavyoifahamu Dodoma, Mkonze kuna maendeleo sana, nenda Noli, Chididimo, Chifutuka, ... utajionea. Dodoma ni masikini kweli. Unajua wale wanaosema kwamba kuna maendeleo yanayoonekana naamini wanaangalia matumbo yao tu. Kimsingi kipato cha wenye nacho kimeongezeka, lakini the mass, yaani watu wa kawaida, hali ni ngumu sana. Hii inatokana na serikali kutofanya chochote kuwawezesha. Miradi kwa mfano ya zabibu ingeweza kuwasaidia sana wananchi lakini utasikia viongozi tu ndo wanaochukua mashamba na miradi hii. Kwao ni dili. Wanakuja kuchuma tu hapa Dodoma.
   
 16. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #16
  Feb 14, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Teh!Unautani na akina AGWE!
   
Loading...