Dodoma: Sita wafariki dunia kwa ajali ya gari

Dodoma: Sita wafariki dunia kwa ajali ya gari

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
24,883
Reaction score
60,915
Watu sita wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa kwenye ajali iliyohusisha gari ndogo kugonga na mkokoteni uliokuwa unavutwa na ng’ombe katika Kijiji cha Lugala Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma leo Jumapili Julai 3, 2022..

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno amethibitisha kutokea ajali hiyo huku akiahidi kutoa taarifa kamili baadaye.

Kamanda amesema yuko njiani kuelekea kwenye eneo la tukio.

Akizungumza kuhusu ajali hiyo Diwani wa kata ya Manzase mkoani Dodoma, John Mika amesema gari ndogo liligonga mkokoteni uliokuwa umebeba watu 12.

“Watu hao walikuwa wanakwenda kwenye mlima wa Lugala kwa ajili ya kuchimba udongo wanaotumia kufinyanga vyungu ndipo gari hilo likawagonga, ambapo watu sita walifariki hapohapo na ng’ombe wawili waliokuwa wakivuta mkokoteni walikufa,” amesema Mika.

Mika amesema majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa hospitali ya Mkoa wa Dodoma.

20220703092206_-535536842_5235250335893045903_572_425_85_webp.jpg
 
Sijui ajali imetokea muda gani ila barabara ya Morogoro Dodoma hasa kuanzia Gairo mpaka Dodoma ni hatari sana kuendesha usiku kuna power tiller hiyo mikokoteni au matrekta yanatembeaga usiku kwa usiku na huwa haya sign yeyote kama vile reflector na hata yakiharibika huwa wanayaacha njiani bila alama yoyote sasa kama utakuwa speed au gari yako haina taa nzuri ni rahisi kupata ajali
 
Sijui ajali imetokea muda gani ila barabara ya Morogoro Dodoma hasa kuanzia Gairo mpaka Dodoma ni hatari sana kuendesha usiku kuna power tiller hiyo mikokoteni au matrekta yanatembeaga usiku kwa usiku na huwa haya sign yeyote kama vile reflector na hata yakiharibika huwa wanayaacha njiani bila alama yeyote sasa kama utakuwa speed au gari yako haina taa nzuri ni rahisi kupata ajali
Asante kwa tahadhari. Njia hio naikumbuka Kwa kupiga tuta lisilo na alama nikiwa zaidi ya 100kph
 
Mwanzo nliona land cruise, nikambiwa tena mkokoteni , ila hapa naona toyota hais ... bado najiuliza kwani mkokoteni wa kuvutwa na ng'ombe inaweza beba watu 12?
 
Sijui ajali imetokea muda gani ila barabara ya Morogoro Dodoma hasa kuanzia Gairo mpaka Dodoma ni hatari sana kuendesha usiku kuna power tiller hiyo mikokoteni au matrekta yanatembeaga usiku kwa usiku na huwa haya sign yeyote kama vile reflector na hata yakiharibika huwa wanayaacha njiani bila alama yoyote sasa kama utakuwa speed au gari yako haina taa nzuri ni rahisi kupata ajali
Nadhani Manzase ni barabara ya Iringa. Halafu huwa wala haipo busy as compared to ile ya Dar, sasa sijui tatizo ilikuwa nini
 
Back
Top Bottom