Dodoma: Shirikisho la Walemavu laipongeza NEC

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,286
Reaction score
10,831
Shirikisho la Vyama vya Walemavu Mkoa wa Dodoma (SHIVYAWATA) limeishukuru Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kuwawezesha kuwaondolea vikwazo watu wenye ulemavu kwenye upigaji kura katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 28, mwaka huu.

Shukrani hizo zilitolewa na Katibu wa SHIVYAWATA Mkoa wa Dodoma, Jastus Ngw'antalima wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa, kuelezea furaha yao waliyopata kutokana na kushirikishwa kikamilifu katika kuchaguzi Rais, Wabunge na Madiwani ijapokuwa walipata changamoto kidogo.

Katibu huyo alisema, wakati wa upigaji kura, katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, vikwazo vingi vinavyokwamisha watu wenye ulemavu kupiga kura vilitatuliwa na kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika upigaji kura huo.

Alisema kutokana na urahisi huo wa kuhakikisha watu hao wenye ulemavu wanashiriki kwa wingi pia imechangia kuwawezesha watu wenye ulemavu kujitokeza kwa wingi kwenye vituo vya kupigia kura na kupiga kura kwa urahisi.

"Sisi kama Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Mkoa wa Dodoma, tuna kila sababu ya kuwapongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuturahisishia upigaji kura kuwa rahisi kwetu tofauti na uchaguzi za huko nyuma," alisema.

Katibu huyo alitaja baadhi ya vikwazo vilivyofaidika navyo kwenye upigaji kura huo kuwa ni pamoja na kuwepo kwa ongezeko la vituo vya kupigia kura, vifaa vingi vya kupigia kura, kuthaminiwa na kupewa ushauri wa kutosha wakati wa kupiga kura.

Hata hivyo katibu huyo alisema, pamoja na kuondolewa kwa changamoto hizo bado watu hao wenye ulemavu wamekutana na vikwazo vya miundombinu kwenye baadhi ya majengo ya shule na kulazimika kubebwa ili aweze kuvifikia vituo vya kupigia kura vilipokuwa vimewekwa.

Alisema kuwa baadhi ya majengo ya shule ya zamani hayajarekebishwa miundombinu yao, hali ambayo watu wenye ulemavu kukutana na changamoto hizo na kujikuta wakipewa msaada wa kubebwa.

Alitaja majengo hayo ambayo yalikuwa yamewekwa vituo vya kupigia kura ni kuwa ni pamoja na majengo ya shule ya msingi na sekondari na ofisi za serikali ambazo nyingi hazina miundombinu ya watu wenye ulemavu au hazijarekebishwa ili kuwapa nafuu watu wenye ulemavu.

Katibu huyo pia aliwataka watu wenye ulemavu mkoani Dodoma kutojihusisha na chokokocho yoyote ambayo inayoashiria kutaka kuharibu amani ya nchi kwani hakuna pa kukimbilia kama kutatokea vita na watu wenye ulemavu watakuwa waathirika wakubwa ikitokea vita hiyo.

Aidha, aliwataka kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika kufanya shughuli zinazowaingizia kipato ili kuiunga mkono serikali katika juhudi zake za kuleta kukuza uchumi ili kuleta maendeleo zaidi kwa watu wote wakiwemo na watu wenye ulemavu.
 
Jamii imeparanganyika na matokeo ya uchaguzi ya aina yake, kama viongozi wa dini nao wataanza kutoa matamko ya kupongeza ushindi huo itabidi hao viongozi watazamwe upya wanamtumikia nani Mungu au Shetani? Ni bora viongozi wa dini wajiepushe na matamko ya kupongeza, wataonekana wanashuhudia ushuhuda wa uongo, kuwa na viongozi wa dini waongo ni hatari kubwa kiroho. Hawataaminika kwa waumini wao
 
Jamii imeparanganyika na matokeo ya uchaguzi ya aina yake,kama viongozi wa dini nao wataanza kutoa matamko ya kupongeza ushindi huo itabidi hao viongozi watazamwe upya wanamtumikia nani Mungu au Shetani? Ni bora viongozi wa dini wajiepushe na matamko ya kupongeza,wataonekana wanashuhudia ushuhuda wa uongo,kuwa na viongozi wa dini waongo ni hatari kubwa kiroho.Hawataaminika kwa waumini wao
Kweli mkuu
 
Mwambie huyo mwakilishi wa walemavu dodoma kula zao zilikuwa maigizo tu, sisi tulishakuwa na kula zetu za kwenye mabegi yaliyotoka mikoani
 
Hawa siyo hata wa kubishana nao. Ni walemavu. Na humo wamo pia walemavu wa akili. Hawa ni wa kuwaonea huruma na kuwaombea.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ulemavu wao unahusika vp mitazamo au misimamo yao? Lowassa ni mgonjwa kabisa hata kuongea vizuri hawezi ila aligombea kutaka kuwa rais na mkampigia kura nyingi mkitaka awaongoze mtu ambaye yeye mwenyewe hajiwezi,sasa hao jamaa wametoa maoni yao unaanza kusema ulemavu wao.
 
Shirikisho la Vyama vya Walemavu Mkoa wa Dodoma (SHIVYAWATA) limeishukuru Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kuwawezesha kuwaondolea vikwazo watu wenye ulemavu kwenye upigaji kura katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 28, mwaka huu.

Shukrani hizo zilitolewa na Katibu wa SHIVYAWATA Mkoa wa Dodoma, Jastus Ngw'antalima wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa, kuelezea furaha yao waliyopata kutokana na kushirikishwa kikamilifu katika kuchaguzi Rais, Wabunge na Madiwani ijapokuwa walipata changamoto kidogo.

Katibu huyo alisema, wakati wa upigaji kura, katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, vikwazo vingi vinavyokwamisha watu wenye ulemavu kupiga kura vilitatuliwa na kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika upigaji kura huo.

Alisema kutokana na urahisi huo wa kuhakikisha watu hao wenye ulemavu wanashiriki kwa wingi pia imechangia kuwawezesha watu wenye ulemavu kujitokeza kwa wingi kwenye vituo vya kupigia kura na kupiga kura kwa urahisi.

"Sisi kama Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Mkoa wa Dodoma, tuna kila sababu ya kuwapongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuturahisishia upigaji kura kuwa rahisi kwetu tofauti na uchaguzi za huko nyuma," alisema.

Katibu huyo alitaja baadhi ya vikwazo vilivyofaidika navyo kwenye upigaji kura huo kuwa ni pamoja na kuwepo kwa ongezeko la vituo vya kupigia kura, vifaa vingi vya kupigia kura, kuthaminiwa na kupewa ushauri wa kutosha wakati wa kupiga kura.

Hata hivyo katibu huyo alisema, pamoja na kuondolewa kwa changamoto hizo bado watu hao wenye ulemavu wamekutana na vikwazo vya miundombinu kwenye baadhi ya majengo ya shule na kulazimika kubebwa ili aweze kuvifikia vituo vya kupigia kura vilipokuwa vimewekwa.

Alisema kuwa baadhi ya majengo ya shule ya zamani hayajarekebishwa miundombinu yao, hali ambayo watu wenye ulemavu kukutana na changamoto hizo na kujikuta wakipewa msaada wa kubebwa.

Alitaja majengo hayo ambayo yalikuwa yamewekwa vituo vya kupigia kura ni kuwa ni pamoja na majengo ya shule ya msingi na sekondari na ofisi za serikali ambazo nyingi hazina miundombinu ya watu wenye ulemavu au hazijarekebishwa ili kuwapa nafuu watu wenye ulemavu.

Katibu huyo pia aliwataka watu wenye ulemavu mkoani Dodoma kutojihusisha na chokokocho yoyote ambayo inayoashiria kutaka kuharibu amani ya nchi kwani hakuna pa kukimbilia kama kutatokea vita na watu wenye ulemavu watakuwa waathirika wakubwa ikitokea vita hiyo.

Aidha, aliwataka kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika kufanya shughuli zinazowaingizia kipato ili kuiunga mkono serikali katika juhudi zake za kuleta kukuza uchumi ili kuleta maendeleo zaidi kwa watu wote wakiwemo na watu wenye ulemavu.
Tatizo sio jinsi ya kupiga kura, tatizo liko kwenye kuheshimiwa hio kura yako
 
Hivyo ndivyo hali ilivyo huko mitaani,hiyo ndio hali inayonesha jinsi watu walivyochukulia hayo matokeo ya uchaguzi huu wenye utata mkubwa .
 
Hao watakua "Umoja Wa Walemavu Milembe".

Ni hasara kubwa mtu duniani kuishi kwa ulemavu, halafu mbinguni kuikosa pepo.
Masuala ya mbinguni kuikosa pepo yameingiaje tena hapa? Kuna wengine wao wana imani kuwa kupiga kura tu ni haramu na wengine hawaamini kabisa hayo masuala ya mbinguni. Sasa tofauti za mitazamo yetu ya kisiasa ziishie hivyo hivyo kisiasa.
 
Ni kweli kabisa mkuu uko sahihi sana. Kuna watu ni mabingwa wa kuhukumu wengine kisa ni utofauti wa mitazamo tu
 
Sidhani kama kuna kikao cho chote kimepitisha azimio hili bali ni maoni binafsi ya katibu.
 
Ulemavu wao unahusika vp mitazamo au misimamo yao? Lowassa ni mgonjwa kabisa hata kuongea vizuri hawezi ila aligombea kutaka kuwa rais na mkampigia kura nyingi mkitaka awaongoze mtu ambaye yeye mwenyewe hajiwezi,sasa hao jamaa wametoa maoni yao unaanza kusema ulemavu wao.
Tofautisha ulemavu na ugonjwa. Ulemavu ni hali ya kupungukiwa kitu fulani katika mwili. Inaweza kuwa ni akili, macho, masikio au kiungo kimojawapo katika mwili. Upungufu huu ni wa kudumu.

Lakini ugonjwa ni hali ya muda fulani tu. Karibu kila mtu, muda fulani amewahi kuwa mgonjwa. Ndugu zetu walemavu, wengine huzaliwa nao, wengine huupata ulemavu baadaye, lakini baada ya kuupata, linakuwa ni tatizo la maisha yake yote.

Wakati watu wote wenye akili timamu, kwa uthibitisho ulio dhahiri wanasema, uchaguzi uligubikwa na kila aina ya uchafu, halafu mlemavu (mwenye upungufu wa akili, asiyesikia, asiyeona, n.k.), anasema kila kitu kilikuwa safi. Kuna nini cha zaidi unachoweza kusema kwa hawa walemavu, zaidi ya:
1) kwa sababu wengine wana ulemavu wa akili, labda hawana uwezo wa kujua kilicho sahihi na kilicho batili
2) Labda kwa sababu wengine hawasikii, hawakuweza kusikia chochote kwa wakati kuhusiana na uchaguzi, wanaongea walicholishwa
3) Labda kwa sababu wengine ni walemavu wa macho, hawakuweza kuona chochote, pamoja na ule uchafu wa kura fake za CCM

Jumuisho: Hawa ni walemavu, wasamehewe, waonewe huruma, tusipoteze muda kuwajadili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumetoka kwenye kulaumu wapinzani na kupongeza awamu ya tano...
sasa...
Tumehamia kwenye kulaumu awamu zilizopita na kupongeza awamu ya tano...

Cc: mahondaw
 
Tofautisha ulemavu na ugonjwa. Ulemavu ni hali ya kupungukiwa kitu fulani katika mwili. Inaweza kuwa ni akili, macho, masikio au kiungo kimojawapo katika mwili. Upungufu huu ni wa kudumu.

Lakini ugonjwa ni hali ya muda fulani tu. Karibu kila mtu, muda fulani amewahi kuwa mgonjwa. Ndugu zetu walemavu, wengine huzaliwa nao, wengine huupata ulemavu baadaye, lakini baada ya kuupata, linakuwa ni tatizo la maisha yake yote.

Wakati watu wote wenye akili timamu, kwa uthibitisho ulio dhahiri wanasema, uchaguzi uligubikwa na kila aina ya uchafu, halafu mlemavu (mwenye upungufu wa akili, asiyesikia, asiyeona, n.k.), anasema kila kitu kilikuwa safi. Kuna nini cha zaidi unachoweza kusema kwa hawa walemavu, zaidi ya:
1) kwa sababu wengine wana ulemavu wa akili, labda hawana uwezo wa kujua kilicho sahihi na kilicho batili
2) Labda kwa sababu wengine hawasikii, hawakuweza kusikia chochote kwa wakati kuhusiana na uchaguzi, wanaongea walicholishwa
3) Labda kwa sababu wengine ni walemavu wa macho, hawakuweza kuona chochote, pamoja na ule uchafu wa kura fake za CCM

Jumuisho: Hawa ni walemavu, wasamehewe, waonewe huruma, tusipoteze muda kuwajadili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hao ni watu wenye shughuli zao na familia zao hivyo wana akili zao sawa kabisa na ndio maana wanashiriki katika uchaguzi wakijua ni haki yao ya msingi ya kupiga kura,hivyo hatuzungumzii watu wenye ulemavu wa akili.

Na pia wapo watu ambao sio walemavu ambao nao wameelezea mtazamo wao wa uchaguzi sawa na hao walemavu,ila wewe unataka kuhusisha maoni yao na ulemavu wao kana kwamba hakuna watu wengine waliyotoa maoni sawa na ya kwao.
 
Madai ya shivyawata kwamba Nec imetatuwa changamoto za watu wenye ulemavu sii za kweli
Kwanza nawapongeza kwa ushindi
Hoja yangu nii watu wenye ulemavu kundi la viziwi hakuna changamoto iliyo tatuliwa tangu kampen zianze viziwi walikosa kusikiliza sera za wagombea hili lilikuwa ni jukumu la nec kuweka wakaliman katika mikutano ya kampen ili wasikilize sera za wagombe sasa viziwi walio wengi wamechagua tu kwakuangalia sura au yanayosemwa na weng hivo shivyawata hawana sababu ya kuudanganya uma kuwa changamoto za walemavu zimetatuliwa ili khali kwa upande wa viziwi hakuna jipya tuiombe serikali kupitia nec ione umuhimu wa watu wenye ulemavu kuwa na jimbo lao ili tuchague viongoz kutokana na sera zetu wenyewe watakao beba ajenda zetu vikamilifu
 
Back
Top Bottom