DODOMA: Prof. Kabudi amuonya Lema awe na adabu. Amnyooshea kidole

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,627
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema) Godbless Lema leo jioni Mei 4, 2018 bungeni mjini Dodoma amevutana na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi baada ya kutamka neno lililomkera mteule huyo wa Rais.

Mvutano baina ya wawili hao umetokea wakati Profesa Kabudi akijibu hoja za wabunge zilizoibuka katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2018/19, ikiwemo ya masheikh wa Uamsho ambao wapo mahabusu kwa muda mrefu ikielezwa kuwa uchunguzi wa mashtaka yao bado haujakamilika.

Wakati waziri huyo akitoa ufafanuzi kuhusu masheikh hao, Lema alitamka neno ambalo halikusikika katika vipaza sauti lakini Profesa Kabudi alilisikia na kuonyesha kukerwa.

“Wewe Lema uwe na adabu,” amesema Profesa Kabudi akimyooshea kidole Lema huku akiwa amekunja uso mithili ya mtu aliyepandwa na jazba hali iliyomfanya Lema kusimama na kutaka kuomba utaratibu lakini Mwenyekiti wa Bunge, Azzan Zungu alimkatalia na kumtaka aketi.

“Lema nakuheshimu,” amesema Kabudi huku Lema naye akimjibu licha ya sauti yake kutosikika jambo ambalo lilimlazimu Zungu kuingilia kati na kumtaka Profesa Kabudi kuzungumza na kiti kutokana na kila mara wabunge wa upinzani kumrushia maneno waziri huyo.

Katika ufafanuzi wake Zungu amesema,
“waheshimiwa wabunge tangu jana mnataka majibu ya Serikali, majibu yanawaingia.” Huku akisisitiza kwamba hatatoa ruhusa ya kutoa mwongozo wala taarifa kutoka kwa wabunge hadi hapo Serikali watakapomaliza kujibu hoja bungeni kuhusu wizara hiyo.
 
Sasa hao masheikh waliwakamata wa nini kama walikua hawajawachunguza na kujiridhisha kama wana kesi za kujibu?na mahakama nayo kwa nini haitoi onyo kuifuta kesi kwa serikali juu ya kuchelewesha upelelezi?hakika hii ni dhulma kubwa
 
Alizoea kutishia watoto na Supplimentary,kila akiingia darasana na vile vimisemo vyake kuwa,Tangu UDSM imeenza tuliopata first class ya sheria tunahesabika.

Sasa huko bungeni hakuna wa kumpa supp..,Hakuna wa kunyenyekea,ni mwendo wa kunyooshwa tu.Ameshindwa kuwa na adabu yeye,leo anayakana yale yooote aliyoongea kwenye tume ya katiba mpaka akawa anatoa mapovu na mate kama bomba la mvua.

Wasomi wanafiki hawa wa Tz,
 
profesa wa hovyo sana huyu Kalamaganda Kabudi.... maprofesa wengine wa hovyo ni Ndalitako, profesa Haruna Mapumba , Profesa Kitila Utumbo, Prof. Mwongo na yule mama Tibaijuka. taifa limejaliwa maforofesa hewa.
 
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema) Godbless Lema leo jioni Mei 4, 2018 bungeni mjini Dodoma amevutana na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi baada ya kutamka neno lililomkera mteule huyo wa Rais.

Mvutano baina ya wawili hao umetokea wakati Profesa Kabudi akijibu hoja za wabunge zilizoibuka katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2018/19, ikiwemo ya masheikh wa Uamsho ambao wapo mahabusu kwa muda mrefu ikielezwa kuwa uchunguzi wa mashtaka yao bado haujakamilika.

Wakati waziri huyo akitoa ufafanuzi kuhusu masheikh hao, Lema alitamka neno ambalo halikusikika katika vipaza sauti lakini Profesa Kabudi alilisikia na kuonyesha kukerwa.

“Wewe Lema uwe na adabu,” amesema Profesa Kabudi akimyooshea kidole Lema huku akiwa amekunja uso mithili ya mtu aliyepandwa na jazba hali iliyomfanya Lema kusimama na kutaka kuomba utaratibu lakini Mwenyekiti wa Bunge, Azzan Zungu alimkatalia na kumtaka aketi.

“Lema nakuheshimu,” amesema Kabudi huku Lema naye akimjibu licha ya sauti yake kutosikika jambo ambalo lilimlazimu Zungu kuingilia kati na kumtaka Profesa Kabudi kuzungumza na kiti kutokana na kila mara wabunge wa upinzani kumrushia maneno waziri huyo.

Katika ufafanuzi wake Zungu amesema,
“waheshimiwa wabunge tangu jana mnataka majibu ya Serikali, majibu yanawaingia.” Huku akisisitiza kwamba hatatoa ruhusa ya kutoa mwongozo wala taarifa kutoka kwa wabunge hadi hapo Serikali watakapomaliza kujibu hoja bungeni kuhusu wizara hiyo.
Kabudi atakimbia bunge kupitia mlango uleule alioingilia , hii ishu ya uamsho si ya kitoto
 
Back
Top Bottom