VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Katika kile kinachoonekana kama upofu wa viongozi wa kitaifa katika kufanya yawapasayo kuyafanya kwa ajili ya wananchi wote,Ofisi ya Spika wa Bunge imetamba kuwa itahakikisha kuwa Bunge la Bajeti halioneshwi luningani. Afisa mmoja Mwandamizi wa Bunge,leo asubuhi ya saa tatu na nusu, alituambia kuwa Ofisi ya Bunge itasimamia uamuzi wake wa awali wa kutorusha moja kwa moja vikao vya Bunge ili kulinda hadhi ya Bunge hilo.
'Katibu Mkuu wa Bunge(Dr.Kashililla) alishasema kuwa Bunge halitaoneshwa 'live'. Watu wakamzongazonga sana kimaneno. Lakini,mwisho wa siku yeye ameibuka mshindi. Si mnaona mpango wa kutolionesha 'live' umeshaanza? ' alisema Afisa huyo wa Bunge
'Watanzania ni rahisi sana kuwaongoza mtu atakavyo. Unasema kwanza. Wakibisha,unawadanganya kuwa umekubaliana nao. Halafu,unafanya utakavyo.Hawabishi tena. Ndivyo Ofisi ya Spika ilivyofanya. Spika na Naibu wake wameubariki uamuzi huu,nani hapa nchini ataupinga?' aliuliza kwa kejeli Afisa huyo aliyekuwa akificha kitambulisho chake ingawa jina la kwanza ni Frank.
Watanzania mpo? Taarifa ni kuwa,mtapata 'edited version' ya Bunge la luningani. Wa kubisha na abishe. Ofisi ya Spika wa Bunge imeapa kusimamia uamuzi wake wa kuzuia kuoneshwa moja kwa moja kwa Bunge.
Tafakari na uchukue hatua!
VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam(sasa Dodoma)
Mkuu betlehem,yawezekana huo ni mpango utakaotekelezwa kwa hatua. Yawezekana ikawa ni taarifa tu hii.Ngoja tusubiri.Mkuu VUTA-NKUVUTE kwa kipindi kirefu nimekuwa sikuamini kulingana na taarifa zako za namna yake unazoweka humu jukwaani ila jana nimeanza kukuamini kidogo baada ya kufanyia utafiti wa kina taarifa yako fulani.Hii ya leo ni kipimo cha mwisho kwangu. Ikitokea kuanzia kesho bunge likawa halirushwi tena mimi ntakuamini sasa.Mpaka kufikia leo bunge bado lilikuwa linakenda live.
hakuna jipya kwako wewe vuta nikusukume
umekosa weledi.. mbona tunaangalia bunge hapa....
kuliko kuonyesha udhaifu wako hapa ni bora ukalale
bungeni unahesabiwa idadi ya post nini? haiwezekani post nne zote zikijibu post moja tu. Unatia mashaka jaribu kutulia na kandika majibu yako sio kukurupuka unatujazia jamvi.silense is gold...vuta nkuvute u better keep quiete
bungeni unahesabiwa idadi ya post nini? haiwezekani post nne zote zikijibu post moja tu. Unatia mashaka jaribu kutulia na kandika majibu yako sio kukurupuka unatujazia jamvi.

Mkuu betlehem,yawezekana huo ni mpango utakaotekelezwa kwa hatua. Yawezekana ikawa ni taarifa tu hii.Ngoja tusubiri.