Dodoma: Msalato International Airport yawekwa kapuni? kwanini wakarabati Uwanja mdogo wa Dodoma?

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,185
18,513
Jana nimeona serikali kwa kupitia waziri wa ujenzi na uchukuzi wakizindua ukarabati wa uwanja wa ndege wa dodoma wakidai wanataka uwe na uwezo wa kupokea ndege kubwa.

Uwanja huu wa ndege upo mjini kabisa hata upanuzi wake sujui wataufanyaje maana lazima kutakua na gharama kubwa pia ni eneo ambalo lipo na makazi ya watu.

Nilidhani pengine wanafanya hivyo ili uwe uwanja wa muda kwa kuwa serikali iliyo pita ilisha pendekeza kujenga uwanja wa kimataifa huko msalato ambko kuna eneo kubwa la kutosha na design ilisha fanyika.

Sijaelewa kwa nini serikali imeamua kupoteza fedha kwenye uwanja mdogo kama ule ambapo ndio makao makuu ya nchi?

Kwa nini wasinge amua kuuhamisha moja kwa moja uwanja huo huko msalato wakajenga uwanja wenye hadhi ya Makao makuu ya nchi?

Naanza kupata wasiwasi na dhana ya hapa kazi tuu nadhani ni hapa kasi tuu kama ile ya vodacom.

b629e645a926971bc80cf87cdc737387.jpg
 
UDOM International Airport ndo mbadala wa Msalato Int. Airport.
Msalato ilishapigwa chini kitambo
 
ha ha ha watanzania kwa mapicha picha tu tunatisha..

nakumbuka tulioneshwaga picha za treni la umeme kutokea airport dar kwenda posta sijui limepotelea wapi tena
 
Hili jambo la kushangaza kweli, wangeanza hata na ujenzi was runway tu, sijui mipango yao ikojeikoje
 
Back
Top Bottom