Dodoma kuna mgawo wa umeme kimya kimya

wakimataifa.

JF-Expert Member
Jun 7, 2015
1,625
554
tuseme kwa sababu ya mkurugenzi kutumbuliwa au vipi kuna rafiki yangu anaishi nkuhungu juzi aliniambia jana yake walikatiwa umeme saa kumi jioni mpaka saa nne usiku nikambisha jana kuna mtu anaishi aliniambia walikatiwa umeme saa kumi mpaka saa nne na dk kumi usiku leo maeneo ya mjini yote umekatika mpaka naleta habari hizi hatuna umeme.
sasa tujue mgomo au ujeuri wa TANESCO au sababu ya nini tunaomba majibu kwa watu wa Tanesco
 
Na ukisema umeme maana yake na maji, jana huku hakukuwa na umeme na maji hakuna hadi leo. hiyo ni Kikuyu
 
Ndugu yangu mchwa hujaribu kulila jiwe. Utakuta wametanda jiwe, wameweka na "lines" zao kama wafanyavyo kwenye nyasi ama mti katika maandalizi ya kuula. Hufanya hayo kwa jeuri, wakitegemea nguvu ya turufu waliyopewa kuharibu kila kitu watakavyo wao, wakijua wazi kuwa jiwe haliwezekaniki, lakini wao wanalijaribu.
Nimetoa mfano wa mchwa na jiwe nikilinganisha na staff wa Tanesco wanavyotutesa na mgao usiokuwa ba taarifa hivi sasa. Wanatuonesha jeuri ya kutumbuliwa Mramba, kwamba hawakupenda na wapo naye!
Baada ya Mramba kufukuzwa, wamebakishwa masalia yake waliokuwa ndani ya chaka,kivulini. Chaka limefyekwa. Sasahivi wanaomboleza maumivu ya nyundo aliyobondwa nayo boss wao.
Wanataka kutuaminisha huyo jamaa kaonelewa.
Mimi nadhani katika figisufigisu hii ya utendaji mbovu wa Tanesco, Magufuli afukuze ikiwezekana staff wote na alisuke shirika upya.
Tutavumilia kutumia koroboi tukisubiri neema ya kudumu itakayoletwa na safu mpya, kuliko mumiani waliopo Tanesco waliovaa ngozi ya kondoo kumbe ni chui wararuao bila huruma wala mswalie mtume.
 
Back
Top Bottom