Dodoma: Kofia mbili kuchomoza mabadiliko CCM

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,795
21,392
CCM imeitisha mkutano mkuu maalumu kufanya marekebisho ya katiba yake kwa kuwapa majukumu wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), kuwarejesha kwenye NEC makatibu wa mikoa na kofia mbili kwa nafasi za uongozi wa juu.

Haya ni mabadiliko ya 17 kufanyika ndani ya chama hicho kilichoanzishwa mwaka 1977 baada ya kuunganishwa kwa vyama vya Tanganyika African National Union (Tanu) cha iliyokuwa Tanganyika, na Afro-Shiraz cha Zanzibar.

Mabadiliko ya mwisho yalifanyika mwaka 2017 yaliyoendana na kuwapunguza wajumbe wengi kwenye vikao vya juu vya chama sababu kubwa ikitajwa ni gharama ingawa kulikuwa na nyingine zilizotajwa nyuma ya pazia.

Hata hivyo, mkutano huu unaotarajiwa kufanyika Aprili mosi pia kuna wana-CCM watatu wenye kesi ya ukosefu wa maadili mbele ya chama na Kamati Kuu imeagiza waitwe kujieleza, akiwamo Humphrey Polepole aliyekuwa mbunge wa kuteuliwa na Rais na sasa ameteuliwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi.

Mkutano mkuu maalumu wa mwaka 2017 uliowafukuza uanachama wana-CCM 12 na wengine kuonywa, pia ulimpa onyo Dk Emmanuel Nchimbi ambaye baadaye aliteuliwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Brazil, wengine ni wabunge Josephat Gwajima (Kawe) na Jerry Silaa (Ukonga). Huenda mkutano huu unakuzungumzia hatma ya wana-CCM hao.

Taarifa ya mwisho ya CCM iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka ilisema Kamati Kuu iliagiza wabunge hao waitwe kujieleza kutokana na dosari na mienendo yao.

Mabadiliko ya katiba
Mabadiliko ya katiba ya mwisho yaliwaondoa ujumbe wa Nec makatibu wa CCM wa mikoa waliokuwa wakiingia kwa nafasi zao na kuwaacha wenyeviti wa CCM wa mikoa kuendela kuwa wa-NEC.

Hata hivyo, taarifa za ndani za CCM zilisema kuondolewa kwa makatibu hao kumetengeneza udhaifu wa utekelezaji wa maagizo yanayotolewa na Nec, kwa kuwa baadhi ya wenyeviti hawayafikishi kwa makatibu wao, huyafikisha kwa kuchelewa au kwa tafsiri isiyo sahihi.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, makatibu wa mikoa ambao ndio watendaji wa chama kwenye maeneo yao, mara kadhaa wameshindwa kutekeleza maagizo ya NEC na kudhoofisha shughuli za chama kwa kuwa hawakuyapata kwa usahihi au hayakufika kabisa.

Kuondolewa NEC
Chanzo chetu kilisema makatibu hao waliondolewa baada ya wajumbe wa NEC ya kumtafuta mgombea urais wa CCM iliyofanyika Septemba 21, 2015, kuimba “tuna imani na Lowassa” wakati Mwenyekiti wa CCM kwa wakati huo Jakaya Kikwete akiingia ukumbini.

Kipindi hicho kilikuwa cha mchakato ndani ya CCM wa kumtafuta mgombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na jina la Edward Lowassa lilikuwa limekatwa na vikao vya mwanzo.

Chanzo chetu kilisema makatibu wa mikoa wanahesabika ni watumishi wa chama, lakini kwa wakati huo hakuna aliyesimama kumtetea mwenyekiti kwa kuupinga wimbo huo.

Wa-NEC kupewa majukumu
Kwa mujibu wa chanzo chetu, wajumbe wa Nec hasa wa wanaowakilisha mikoa wamekuwa wakilalamika hawana majukumu ya kufanya baada ya vikao wanavyohudhuria vya Nec na kamati za siasa za mikoa yao.

Mabadiliko haya yanakwenda kuwapa majukumu wa-Nec kwa kuwanganisha na wajumbe wa mitaa ili waongeze nguvu kuratibu kazi za chama kwenye mashina ya maeneo yao.

Kofia mbili
Kwa mujibu wa chanzo chetu CCM inatarajia kurejesha mfumo wa uongozi wa kofia mbili kwa zile nafasi nyeti, ili wahusika waingie kwa nafasi zao.

Mfano, Rais anapochaguliwa kushika uongozi wa nchi vile vile awe mwenyekiti wa chama kwa nafasi yake badala ya kwenda kuchaguliwa tena ndani ya chama.

Hali ilivyo sasa, uchaguzi ndani ya CCM na ule wa nchi unafanyika tofauti, hivyo, kiongozi anayeondoka kwenye nafasi ya urais anabaki kuwa mwenyekiti wa chama hadi uchaguzi utakapofanyika mwaka mmoja baadaye.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, hiyo imekuwa ikiwalazimu wenyeviti hao kujiuzulu nyadhifa hizo ili kumpa nafasi aliye madarakani kuongoza Serikali na chama.

Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa (marehemu) alijiuzulu uenyekiti wa chama na kumuachia Jakaya Kikwete aliyekuwa amechukua uongozi wa nchi na Kikwete alipoondoka madarakani alijiuzulu uenyekiti na kumuchia John Magufuli (marehemu).

Kwa mujibu wa chanzo chetu hilo linategemea na hiari ya mtu na wakati mwingine imekuwa ngumu katika utendaji wa kazi za Rais pale anapoingia kwenye vikao vya chama kama mwalikwa akisubiri muda wa uchaguzi.

Kauli ya Shaka
Katibu mwenezi wa CCM, Shaka alisema sababu ya kufanya marekebisho ya katiba ni kuongeza kasi ya ufanisi wa kazi za chama na utekelezaji wa maamuzi ya vikao vya chama.

Shaka alisema pia lengo lingine ni kuongeza na kuimarisha udhibiti wa chama na viongozi wake wanaochaguliwa na kuongoza kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM kupiti Serikali za mitaa.

Mabadiliko yapunguza ajira
Mabadiliko hayo yaliondoka na ajira zaidi ya 170, hasa makatibu wasaidizi wa mikoa na wilaya na wenye vyeo visivyotambulika katika katiba waliokuwa wakilipwa mishahara, huku ikiondoa mzigo wa posho, ikielezwa kuwa kazi zao zitafanywa na makatibu wa jumuiya. Katika mlolongo huo, wamo makatibu wasaidizi wa mikoa ambao idadi yake ni 32 na wilaya 139, walipoteza ajira zao.

Mabadiliko mengine ni kupunguza wajumbe waliokuwa na kofia mbili kama vile wabunge na wajumbe wa Nec, isipokuwa tu pale ambapo wanalazimika kwa mujibu wa nafasi zao.

Chanzo: Mwananchi
 
Kofia mbili tuseme kuanzia Mwenyekiti wa CCM Taifa asiwe pia Rais wa nchi siyo !! ama ?

Kama hivi ndivyo basi haya yatakuwa mabadiliko makubwa mno ndani ya chama chetu, sijui yamesukumwa na nini? yaani why now ?
 
Haiwezi kuwa Mkuu, Rais kutokuwa Mwenyekiti wa Chama maana yake unajenga chama ndani ya Chama, unajenga kundi lenye nguvu ndani ya chama, unajenga mazingira ya watu kukosa 'heshima na hofu' juu ya Rais maana wanajua hana 'meno' kwenye chama.

Hii ndiyo ilileta changamoto pale South Africa, Zuma alikosa power na akaacha kuogopwa na hatimaye akina Rampho wakamtumia Chairperson ku'push agenda ya kumuondoa Zuma.

Ndani ya Chama, Mwenyekiti anayo nguvu kubwa sana. I bet CCM hawatofanya hili kosa.
 
Ushauri wa bure kwa uongozi wa CCM Taifa.
1. Lipeni mabalozi posho au mshahara unaokubalika ili kukijenga chima ngazi ya shina kuliko kupeana posho na ajira huko juu wakati kwrnye ngazi ya shina mnsua chama na mmebaki na wazee tu hakuna vijana wa kuwa balozi kwa kaxi ya bure.
2. Walipeni makatibu wa matawi posho au mshahara badsla ya utani na ujinga uliopo sasa wa kuwalipa Tsh 5,000 kwa mwezi na posho yenyewe wanalipwa kwa mikono badala ya kuwalipwa kwa mfumo wa simu zao kutokea makao makuu moja kwa moja na zilipwe kwa wakati.
3.walipeni posho au mishahara ya kutosha makatibu kata ambao ni watumishi wa chamanngazi ya kata, kwa sasa mnawalipa Tsh 10,000 kwa mwezi.
4. Walipeni wenyeviti wa ccm mkoa, wilaya na kata posho au mishahara kuliko ilivyo sasa hawalipwi chochote anathema Wewe majambazi au wako wapi au wan Isije?
5. UVCCM inapumulia mashine ngazi ya Matawi, kata, wilay na mikoani kwenye katiba mpya Angalia a bora ya Kuboresha jumuia hiyo kimapato.
6. Mtaji mkubwa wa ccm ni wazee Kwa sasa ambao wengi wao wameendelea kufa na kukosa uwezo wa kukimbia kuhusu mambo ya chama. Sasa katiba ibadili hali mtaji wa ccm uwe vijana walio wengi.
7. Uongozi au kiongozi ndani ya ccm achaguliwe kulingana na sifa Za elimu na Sio kusema kujua kusoma na kuandika imepitwa na wakati. Au sifa ya kuvaa awe kila siku Ndio awe kiongozi.
8. CCM ihakikishe inakuwa na Ofisi Za chama Za kudumu kuanzia ngazi ya shina, Tawi na kata Kwa sasa Ofisi zote zipo wilaya na mikoani tu.
9. Makatibu wa ccm wilaya Wewe viongozi ambao ni vijana kwa umri kuliko ilivyo sasa ni wazee unakuta ni Katibu wa ccm wa vijana wilaya au Mkoa.
9. Habari ya kofia mbili muwe makini na hilo, mnarudi tulikotoka mtu Ana kofia hadi sita na nafasi hizo Haitink anakwenda kusaini posho na kuondoka au rafiki kabisa ila posho anatengewa na kupelekewa au inachukuliwa na wengine.
 
Haiwezi kuwa Mkuu, Rais kutokuwa Mwenyekiti wa Chama maana yake unajenga chama ndani ya Chama, unajenga kundi lenye nguvu ndani ya chama, unajenga mazingira ya watu kukosa 'heshima na hofu' juu ya Rais maana wanajua hana 'meno' kwenye chama.

Hii ndiyo ilileta changamoto pale South Africa, Zuma alikosa power na akaacha kuogopwa na hatimaye akina Rampho wakamtumia Chairperson ku'push agenda ya kumuondoa Zuma.

Ndani ya Chama, Mwenyekiti anayo nguvu kubwa sana. I bet CCM hawatofanya hili kosa.
Hiyo Kwa Tanzania haiwezekani,
Chama kikileta ujuaji juu ya raisi,amiri jeshi mkuu,JWTZ wanapelekwa kuwanyoosha😂
 
"
8. CCM ihakikishe inakuwa na Ofisi Za chama Za kudumu kuanzia ngazi ya shina, Tawi na kata Kwa sasa Ofisi zote zipo wilaya na mikoani tu."

Siyo kweli. Ukweli ni kwamba CCM ina ofisi za kudumu kuanzia shina hadi Taifa.

Kwenye mashina, Ofisi ya CCM ni nyumbani kwa Balozi/Mjumbe. Na kama tunavyojua, ukipita mtaani ukakuta bendera nyumbani kwa mtu basi tunajua huyo ni Mjumbe wa Nyumba 50.

Matawi, Kata, na Vijijini kuna ofisi za kudumu za CCM.
 
Hapo mchonga hakuuweka kiujanja ujanja hiyo kweli,ili amfukuze mtu urais kipindi yeye mwenyekiti,nasikia alikua mwenyekiti Hadi 1990s hapa,Kama ni kweli..Basi alipenda Sana madaraka
 
"
8. CCM ihakikishe inakuwa na Ofisi Za chama Za kudumu kuanzia ngazi ya shina, Tawi na kata Kwa sasa Ofisi zote zipo wilaya na mikoani tu."

Siyo kweli. Ukweli ni kwamba CCM ina ofisi za kudumu kuanzia shina hadi Taifa.

Kwenye mashina, Ofisi ya CCM ni nyumbani kwa Balozi/Mjumbe. Na kama tunavyojua, ukipita mtaani ukakuta bendera nyumbani kwa mtu basi tunajua huyo ni Mjumbe wa Nyumba 50.

Matawi, Kata, na Vijijini kuna ofisi za kudumu za CCM.
Matawi, Kata, na Vijijini hakuna ofisi za kudumu za CCM.
Kwenu ni wapi au ni wale wale mnaomdanganya samia kuwa agombee Urais 2025?
 
Waondoe kitu inasema Ujamaa

Socialist countries are non existent

Wakiondoa socialism, na kofia 2 zitaondoka
 
CCM imeitisha mkutano mkuu maalumu kufanya marekebisho ya katiba yake kwa kuwapa majukumu wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), kuwarejesha kwenye NEC makatibu wa mikoa na kofia mbili kwa nafasi za uongozi wa juu.

Haya ni mabadiliko ya 17 kufanyika ndani ya chama hicho kilichoanzishwa mwaka 1977 baada ya kuunganishwa kwa vyama vya Tanganyika African National Union (Tanu) cha iliyokuwa Tanganyika, na Afro-Shiraz cha Zanzibar.

Mabadiliko ya mwisho yalifanyika mwaka 2017 yaliyoendana na kuwapunguza wajumbe wengi kwenye vikao vya juu vya chama sababu kubwa ikitajwa ni gharama ingawa kulikuwa na nyingine zilizotajwa nyuma ya pazia.

Hata hivyo, mkutano huu unaotarajiwa kufanyika Aprili mosi pia kuna wana-CCM watatu wenye kesi ya ukosefu wa maadili mbele ya chama na Kamati Kuu imeagiza waitwe kujieleza, akiwamo Humphrey Polepole aliyekuwa mbunge wa kuteuliwa na Rais na sasa ameteuliwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi.

Mkutano mkuu maalumu wa mwaka 2017 uliowafukuza uanachama wana-CCM 12 na wengine kuonywa, pia ulimpa onyo Dk Emmanuel Nchimbi ambaye baadaye aliteuliwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Brazil, wengine ni wabunge Josephat Gwajima (Kawe) na Jerry Silaa (Ukonga). Huenda mkutano huu unakuzungumzia hatma ya wana-CCM hao.

Taarifa ya mwisho ya CCM iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka ilisema Kamati Kuu iliagiza wabunge hao waitwe kujieleza kutokana na dosari na mienendo yao.

Mabadiliko ya katiba
Mabadiliko ya katiba ya mwisho yaliwaondoa ujumbe wa Nec makatibu wa CCM wa mikoa waliokuwa wakiingia kwa nafasi zao na kuwaacha wenyeviti wa CCM wa mikoa kuendela kuwa wa-NEC.

Hata hivyo, taarifa za ndani za CCM zilisema kuondolewa kwa makatibu hao kumetengeneza udhaifu wa utekelezaji wa maagizo yanayotolewa na Nec, kwa kuwa baadhi ya wenyeviti hawayafikishi kwa makatibu wao, huyafikisha kwa kuchelewa au kwa tafsiri isiyo sahihi.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, makatibu wa mikoa ambao ndio watendaji wa chama kwenye maeneo yao, mara kadhaa wameshindwa kutekeleza maagizo ya NEC na kudhoofisha shughuli za chama kwa kuwa hawakuyapata kwa usahihi au hayakufika kabisa.

Kuondolewa NEC
Chanzo chetu kilisema makatibu hao waliondolewa baada ya wajumbe wa NEC ya kumtafuta mgombea urais wa CCM iliyofanyika Septemba 21, 2015, kuimba “tuna imani na Lowassa” wakati Mwenyekiti wa CCM kwa wakati huo Jakaya Kikwete akiingia ukumbini.

Kipindi hicho kilikuwa cha mchakato ndani ya CCM wa kumtafuta mgombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na jina la Edward Lowassa lilikuwa limekatwa na vikao vya mwanzo.

Chanzo chetu kilisema makatibu wa mikoa wanahesabika ni watumishi wa chama, lakini kwa wakati huo hakuna aliyesimama kumtetea mwenyekiti kwa kuupinga wimbo huo.

Wa-NEC kupewa majukumu
Kwa mujibu wa chanzo chetu, wajumbe wa Nec hasa wa wanaowakilisha mikoa wamekuwa wakilalamika hawana majukumu ya kufanya baada ya vikao wanavyohudhuria vya Nec na kamati za siasa za mikoa yao.

Mabadiliko haya yanakwenda kuwapa majukumu wa-Nec kwa kuwanganisha na wajumbe wa mitaa ili waongeze nguvu kuratibu kazi za chama kwenye mashina ya maeneo yao.

Kofia mbili
Kwa mujibu wa chanzo chetu CCM inatarajia kurejesha mfumo wa uongozi wa kofia mbili kwa zile nafasi nyeti, ili wahusika waingie kwa nafasi zao.

Mfano, Rais anapochaguliwa kushika uongozi wa nchi vile vile awe mwenyekiti wa chama kwa nafasi yake badala ya kwenda kuchaguliwa tena ndani ya chama.

Hali ilivyo sasa, uchaguzi ndani ya CCM na ule wa nchi unafanyika tofauti, hivyo, kiongozi anayeondoka kwenye nafasi ya urais anabaki kuwa mwenyekiti wa chama hadi uchaguzi utakapofanyika mwaka mmoja baadaye.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, hiyo imekuwa ikiwalazimu wenyeviti hao kujiuzulu nyadhifa hizo ili kumpa nafasi aliye madarakani kuongoza Serikali na chama.

Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa (marehemu) alijiuzulu uenyekiti wa chama na kumuachia Jakaya Kikwete aliyekuwa amechukua uongozi wa nchi na Kikwete alipoondoka madarakani alijiuzulu uenyekiti na kumuchia John Magufuli (marehemu).

Kwa mujibu wa chanzo chetu hilo linategemea na hiari ya mtu na wakati mwingine imekuwa ngumu katika utendaji wa kazi za Rais pale anapoingia kwenye vikao vya chama kama mwalikwa akisubiri muda wa uchaguzi.

Kauli ya Shaka
Katibu mwenezi wa CCM, Shaka alisema sababu ya kufanya marekebisho ya katiba ni kuongeza kasi ya ufanisi wa kazi za chama na utekelezaji wa maamuzi ya vikao vya chama.

Shaka alisema pia lengo lingine ni kuongeza na kuimarisha udhibiti wa chama na viongozi wake wanaochaguliwa na kuongoza kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM kupiti Serikali za mitaa.

Mabadiliko yapunguza ajira
Mabadiliko hayo yaliondoka na ajira zaidi ya 170, hasa makatibu wasaidizi wa mikoa na wilaya na wenye vyeo visivyotambulika katika katiba waliokuwa wakilipwa mishahara, huku ikiondoa mzigo wa posho, ikielezwa kuwa kazi zao zitafanywa na makatibu wa jumuiya. Katika mlolongo huo, wamo makatibu wasaidizi wa mikoa ambao idadi yake ni 32 na wilaya 139, walipoteza ajira zao.

Mabadiliko mengine ni kupunguza wajumbe waliokuwa na kofia mbili kama vile wabunge na wajumbe wa Nec, isipokuwa tu pale ambapo wanalazimika kwa mujibu wa nafasi zao.

Chanzo: Mwananchi

CCM wanabadilisha katiba yao ya 1977 iendane na wakati, kwanini hawataki tubadili Katiba ya JMT ya 1977?​

Matawi, Kata, na Vijijini hakuna ofisi za kudumu za CCM.
Kwenu ni wapi au ni wale wale mnaomdanganya samia kuwa agombee Urais 2025?
Nikuulize wewe kwenu ni wapi.

Mfano, Kilimanjaro, ofisi ya Mkoa ipo Moshi Mjini.

Wilaya ya Moshi, ofisi ipo Moshi Mjini, Arusha Road

Kata ya Kibosho Magharibi, ofisi ipo Mawaleni, Kibosho

Tawi la Manushi Sinde,ofisi ipo Manushi Sinde.

Balozi/Mjumbe kwake kuna bendera na hapo ndipo ilipo ofisi ya shina.

Upo?
 
CCM wanabadilisha katiba yao ya 1977 iendane na wakati, kwanini hawataki tubadili Katiba ya JMT ya 1977​

Chanzo: Mwana

Nikuulize wewe kwenu ni wapi.

Mfano, Kilimanjaro, ofisi ya Mkoa ipo Moshi Mjini.

Wilaya ya Moshi, ofisi ipo Moshi Mjini, Arusha Road

Kata ya Kibosho Magharibi, ofisi ipo Mawaleni, Kibosho

Tawi la Manushi Sinde,ofisi ipo Manushi Sinde.

Balozi/Mjumbe kwake kuna bendera na hapo ndipo ilipo ofisi ya shina.

Upo?
Nikuulize wewe kwenu ni wapi.

Mfano, Kilimanjaro, ofisi ya Mkoa ipo Moshi Mjini.

Wilaya ya Moshi, ofisi ipo Moshi Mjini, Arusha Road

Kata ya Kibosho Magharibi, ofisi ipo Mawaleni, Kibosho

Tawi la Manushi Sinde,ofisi ipo Manushi Sinde.

Balozi/Mjumbe kwake kuna bendera na hapo ndipo ilipo ofisi ya shina.

Upo?
Niambie ipo Ofisi ya ccm Kata mji mpya dodoma? Weka picha
 
Nikuulize wewe kwenu ni wapi.

Mfano, Kilimanjaro, ofisi ya Mkoa ipo Moshi Mjini.

Wilaya ya Moshi, ofisi ipo Moshi Mjini, Arusha Road

Kata ya Kibosho Magharibi, ofisi ipo Mawaleni, Kibosho

Tawi la Manushi Sinde,ofisi ipo Manushi Sinde.

Balozi/Mjumbe kwake kuna bendera na hapo ndipo ilipo ofisi ya shina.

Upo?
Weka picha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom