Dodoma: Jina la Mbunge Halima Mdee, moja ya sababu kufutwa kwa hotuba nzima ya upinzani kuhusu Wizara ya Fedha na Mipango Bungeni

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amezuia Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kusoma maoni yao kuhusu bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa madai imejaa makosa.

Ametoa zuio hilo bungeni leo Jumatatu Juni 3, 2019, Spika Ndugai amesema sababu mojawapo ni jina la mbunge wa Kawe (Chadema) Halima ambaye ametajwa kwenye kitabu cha hotuba hiyo ukurasa wa mbele.

Amesema hotuba nzima kuanzia ukurasa wa kwanza hadi mwisho imejaa maneno yasiyo faa wakati wanajua maandishi hayo yatadumu hata miaka 100 ijayo.

Msemaji wa upinzani wa Wizara ya Fedha Halima Mdee amesimamishwa na Bunge kuhudhuria mikutano mwili ya Bunge kuanzia huu unaoendelea wa 15 wa Bunge la Bajeti kwa kosa la kuunga mkono kauli ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad kwamba Bunge ni dhaifu.

"Hapa tunatoka sisi lakini kuna vizazi vyetu na wajuu na vitukuu wetu watasoma vitabu hivi, haiwezekani mtu umesimamishwa halafu unashiriki kufanya kazi za Bunge," amesema Ndugai.

Hivi karibu Ndugai aliwaambia wapinzani bungeni kuwa hotuba zao zitaruhusiwa kusomwa isipokuwa aliwatahadharisha kuwa makini na uandishi usioleta mgongano.

Hotuba hiyo iliyozuiwa ilikuwa isomwe na Mbunge wa Momba (Chadema), David Silinde ambaye ni Naibu Waziri kivuli katika Wizara ya fedha na ndiye aliyesoma hotuba hizo kwa miaka miwili kutokana na Mdee kuwa nje kwa adhabu mbalimbali.

View attachment 1116087
Kweli Ndugai ni dhaifu, na Bunge linaloongozwa na Ndugai na Bi.Betina nalo ni dhaifu!
 
Chadema nao wanaudhi.hotuba ya Bajeti ya upinzani inatakiwa ijae mamba sio majina ya watu na porojo. Bajeti ilitakiwa ijikite kusema Sisi upinzani. Bajeti yetu ingekuwa hivi vyanzo vya mapato vingekuwa hivi kila kimoja kingeingiza shilingi kadhaa jumla ya mapato ingekuwa hii. Matumizi yangekuwa haya wakaweka break down na vipaumbele vya bajeti yetu vingekuwa hivi ambavyo vingegharimu kiasi cha shilingi hizi. Wao kazi yao ni. Kutoa bajeti mbadala ya upinzani sio porojo za halima mdee. Hongera spika kuikataa hiyo waliyoleta sio Bajeti ya upinzani
Umeisoma hiyo hotuba? au kama kawaida wakisema wao inatosha
 
Kweli Ndugai ni dhaifu, na Bunge linaloongozwa na Ndugai na Bi.Betina nalo ni dhaifu!
Nakuhakikishia kwa hili la bajeti ya Upinzani kukosekana Upinzani ndio dhaifu hasa.Leteni bajeti yenu kuwa mngeshika nchi bajeti yenu ingekuwa hivi.Leteni bajeti porojo wananchi hatutaki.Where is your budget? Waziri wa fedha wa serikali kaleta bajeti ninyi mnaketa porojo za halima mdee na kelele za people's power leteni budget.Ndugai Yuko sahihi yeye anatakiwa apokee budget yenu Sio porojo zenu
 
Bunge DHAIFU linahofia kusikia jina la Halima Mdee maana wakilisikia Wabunge wote DHAIFU wa maccm watakufa.
This is double standard, hajui afanyalo.
Alikataa kufanya kazi na CAG Assad but still akapokea report yenye jina lake.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amezuia Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kusoma maoni yao kuhusu bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa madai imejaa makosa.

Ametoa zuio hilo bungeni leo Jumatatu Juni 3, 2019, Spika Ndugai amesema sababu mojawapo ni jina la mbunge wa Kawe (Chadema) Halima ambaye ametajwa kwenye kitabu cha hotuba hiyo ukurasa wa mbele.

Amesema hotuba nzima kuanzia ukurasa wa kwanza hadi mwisho imejaa maneno yasiyo faa wakati wanajua maandishi hayo yatadumu hata miaka 100 ijayo.

Msemaji wa upinzani wa Wizara ya Fedha Halima Mdee amesimamishwa na Bunge kuhudhuria mikutano mwili ya Bunge kuanzia huu unaoendelea wa 15 wa Bunge la Bajeti kwa kosa la kuunga mkono kauli ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad kwamba Bunge ni dhaifu.

"Hapa tunatoka sisi lakini kuna vizazi vyetu na wajuu na vitukuu wetu watasoma vitabu hivi, haiwezekani mtu umesimamishwa halafu unashiriki kufanya kazi za Bunge," amesema Ndugai.

Hivi karibu Ndugai aliwaambia wapinzani bungeni kuwa hotuba zao zitaruhusiwa kusomwa isipokuwa aliwatahadharisha kuwa makini na uandishi usioleta mgongano.

Hotuba hiyo iliyozuiwa ilikuwa isomwe na Mbunge wa Momba (Chadema), David Silinde ambaye ni Naibu Waziri kivuli katika Wizara ya fedha na ndiye aliyesoma hotuba hizo kwa miaka miwili kutokana na Mdee kuwa nje kwa adhabu mbalimbali.

View attachment 1116087
Upinzani wa nchi hii mambo yao ni ya kitoto kitoto tuu as if hawakwenda shule!
 
Nakuhakikishia kwa hili la bajeti ya Upinzani kukosekana Upinzani ndio dhaifu hasa.Leteni bajeti yenu kuwa mngeshika nchi bajeti yenu ingekuwa hivi.Leteni bajeti porojo wananchi hatutaki.Where is your budget? Waziri wa fedha wa serikali kaleta bajeti ninyi mnaketa porojo za halima mdee na kelele za people's power leteni budget.Ndugai Yuko sahihi yeye anatakiwa apokee budget yenu Sio porojo zenu
Hoija isiyo mashiko,unataka hotuba wakati babako hataki kuipokea?

Ndiyo sababu uvutaji wa ndumu haukubaliwi na jamii yetu kwa mambo kama haya
 
Chadema nao wanaudhi.hotuba ya Bajeti ya upinzani inatakiwa ijae namba sio majina ya watu na porojo. Bajeti ilitakiwa ijikite kusema Sisi upinzani. Bajeti yetu ingekuwa hivi vyanzo vya mapato vingekuwa hivi kila kimoja kingeingiza shilingi kadhaa jumla ya mapato ingekuwa hii. Matumizi yangekuwa haya wakaweka break down na vipaumbele vya bajeti yetu vingekuwa hivi ambavyo vingegharimu kiasi cha shilingi hizi. Wao kazi yao ni Kutoa bajeti mbadala ya upinzani sio porojo za halima mdee. Hongera spika kuikataa hiyo waliyoleta sio Bajeti ya upinzani
Kama unajua hayo yote kwanini usiende upinzani? Badala yake umekazana kuwafundisha wapinzani wa kweli nyuma ya keynoard. Hovyo kabisa!
 
Miaka 100 ijayo pia vizazi watasoma kuwa kulikuwa na bunge lililoongozwa na Spika Ndugai ambaye alikuwa akisikia neno dhaifu anafungia na kumkataa kila aliyelitamka! Lakini mienendo na matendo yalionyesha kuwa kulikuwa na udhaifu wa kweli.
 
Back
Top Bottom