Petro Proshenko
Member
- Feb 25, 2015
- 67
- 127
Hili ni wazo langu pekee mimi siyo mjumbe wa Kamati Kuu wala NEC wala mwanachama wa chama chochote cha siasa ni raia mzalendo wa kawaida tu niliyezaliwa miezi michache kabla ya uhuru wa nchi hii.
Baada ya kukubali kuwa Dodoma yawe Makao Makuu ya Serikali, nimetafakari kwa kina sana kwanini tusiupe heshima ya jina la Rais wetu wa kwanza kama ilivyo jiji la Washington DC na majiji mengine ulimwenguni?
Nimejiridhisha kwa sababu kuu zifuatazo;
1) Mwalimu JK Nyerere ni muasisi wa kwanza wa Taifa hili
2) Ndiye aliyesimamia na kupitisha wazo la Dodoma kuwa Makao Makuu
3) Ili kumuenzi kwa uzuri kabisa licha ya kutumia jina lake kwa majina ya Kiwanja cha Ndege, Barabara, mitaa, shule na Majengo basi tukajumuisha yote kabisa na kuuita Jiji lijalo la Dodoma kwa jina NYERERE JK CITY. Hii itatoa nafasi kwa vizazi vijavyo kutokuipoteza historia ya Mwalimu JK Nyerere muasisi wa Taifa.
4.) Ni mtanzania pekee wa kwanza kuweza kuwaunganisha watanzania wa kabila zote na kujenga utaifa.
Naelewa kuwa mji wa Dodoma una historia ya uasili wake, Nia yangu siyo kuipora hiyo historia bali ni kuiongezea thamani zaidi na kuinganisha katika historia ya nchi hii kikamilifu.
Dhamira yangu si kisiasa bali ni maono niliyoyapata baada ya kutathimini kwa kina mengi mema Mwalimu JK Nyerere aliyoifanyia nchi hii.Mbali ya wachangiaji mbali mbali wa safu hii naamini pia wanasiasa wetu wenye nia njema na nchi hii wataafiki wazo hili na kukaribisha mjadala wa kitaifa kuhusu wazo hili.Tusiingize malumbano ya kisiasa katika kujadili mustakabali wa wazo hili.