Ni kitu kilicho wazi kabisa, hata kwa mtoto mdogo, kuwa CCM wanafanya kila njia kuwadhibiti wabunge wa CHADEMA katika kutoa hoja zao. Wananchi wote wameliona hilo na wanalizungumzia. Uzuri wa hoja za wabunge wa CHADEMA ni kuwa hoja zao zipo katika kutetea maslahi ya wananchi na Tanzania kwa ujumla. Sasa kwa sababu CCM wao wanaoliona ni kuitetea serikali kwa kila hali, wanashindwa kuona kwamba kwa kupinga hoja za CHADEMA, wanapinga matakwa ya wananchi, na hivyo kuwa kinyume na wananchi. Jambo hili ndilo litakaloiangusha CCM.