Dodoma-CHADEMA wapambane hadi mwisho!

Dodoma-CHADEMA wapambane hadi mwisho!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Hapa Dodoma,mambo yanazidi kupamba moto. CHADEMA ikiwakilishwa na Wabunge wasiofikia 50 Bungeni kati ya karibu Wabunge 300 wa Bunge zima,inachachafya Bunge,inatoa hoja nzito,inasema kweli daima hata kama ukweli unaumiza 'Wakubwa'. CHADEMA wanalichangamsha Bunge kihoja na kimjadala. Ni kweli.

Kama nilivyoripoti katika uzi wangu wa "Dodoma-Mambo ni moto!",hapa Bungeni kuna mkakati wa makusudi wa kuwadhibiti Wabunge wa upinzani hasa CHADEMA na wafananao na hao ili kufanikisha mpango madhubuti wa kuilinda Serikali na CCM kwa namna yoyote ile.

Kutokana na yanayoendelea,mtakubaliana nami kuwa CCM wanabebwa Bungeni. Sina haja ya kurudia matusi na lugha za kuudhi za Mwigulu Nchemba,Juma Nkamia na Peter Serukamba. Na hata kilichotokea jana cha kutolewa nje ya Bunge kwa Mbunge na Wakili Msomi Tundu A.M.Lissu.

Kimsingi,Naibu Spika Job Ndugai na Lissu hawaivi. 'Wana bifu'.Tegemeeni mabishano zaidi mbeleni pale ambapo Ndugai ataongoza Bunge na Lissu akiwemo Bungeni. Ni wazi pia kuwa si Makinda wala Ndugai wanaoliweza Bunge hili.Sababu kuu ni moja:wanawachukulia Wabunge wa CHADEMA kama wakorofi na wanaharakati.

Hapa Dodoma,Mawaziri,Wabunge wa CCM na wale wa upinzani(si wa CHADEMA) wanamimina nyaraka za pongezi kwa kiti cha Spika kwa kuwadhibiti CHADEMA.Pia Mwigulu Nchemba na Livingstone Lusinde aka Kibajaji wanapongezwa kwa kuongoza mashambulizi ya kupoteza malengo ya CHADEMA kihoja na 'kuwaweza'.

Kimsingi,mipango yote hapa Bungeni Dodoma si kujadili hasa Bajeti;ni kuwadhibiti CHADEMA.So amazing! Sijui itakuwaje mwaka huu katika Bajeti na mjadala wake kwakweli!?

Sasa, CHADEMA wasirudi nyuma. Waendelee kupambana.Waeendelee kuwa tegemeo pekee kwa watanzania hapa Bungeni Dodoma. Wasiogope kutolewa nje. Watakaobaki ndani waendeleze mapambano. Kwa mipango yetu hii haramu ya kichama,CCM inafikia mwisho wa kutuongoza hapa Tanzania.

Wewe unasemaje?
VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam(sasa Dodoma)
 
Last edited by a moderator:
Pengo la Samweli Sitta linaonekana wazi wazi.
 
Ahsante..makamanda hawarudi nyuma,SERUKAMBA ALIETUKANA ANAPETA,LISSU kutaka sheria ifuatwe anaadhibiwa..naisubiri 2015.
 
HUO NDIO UKWELI WENYEWE MKUU, BUNGE HASA KITI CHA SPIKA KIPO KISISIEMU ZAIDI SIO KIHOJA ZA KUWATETEA WANANCHI. LAKINI UZURI WANANCHI WANAONA.. TAYARI LUSHOTO VIJIJINI HUKO HALI IMESHAKUWA ABRAKALABDA KWA SISIEMU, MPAKA DC ANATIISHIA KUWAFUTA WATU KAZI KWA KUTOA ELIMU YA URAIA.

SASA NGOJA WANALUMUMBA WENZAKO WAJE WAKU SERUKAMBA, MAAANA HAWANA HATA PESA YA KULA MJINI. SASA HIVI WANALIPWA 7000 PER THREAD WAKICHANGIA...

Cc. CHAMA, RITZ, REJAO, TASWIRA, WINGU, KATIBA MPYA, SUMU, STROKE, FAIZA FOX......
 
Mkuu commited,hao wote uliwaorodhesha wamenikuta chamani. Hawanitishi kwa lolote.
 
Last edited by a moderator:
makinda na ndukai uelewa ni mdogo wanafikiri hicho kiti ni cha milele .
 
Mkuu commited,hao wote uliwaorodhesha wamenikuta chamani. Hawanitishi kwa lolote.

hahhaaaa safi sana mkuu, HONGERA SANA kuna wakati lazima tuweke uchama pembeni, kama vyama vyetu havifanyi kazi yao sawasawa lazima TUSEME. NAKUUUNGA MKONO, BASI HAO VIJANA WAFUNDISHE SIASA ZA KIMAENDELEO SIO SIASA ZA KUTUKANA WATU BILA SABABU ZA MSINGI. WAO ISHU ZINAZOGUSA MASLAHI YA TAIFA HAWAJADILI, BALI WAKIONA ISHU INAYOIGUSA CHADEMA HAPO WATEKESHA. WAFUNDISHE KUJADILI MAMBO YA MSINGI, ILI NCHI YETU IENDELEE. HONGERA SANA MKUU KWA UJASIRI WAKO;
 
Mimi na nashauri kungekupo pia sheria ya kuwatoa wote wanaosinzia , wasiochangia chochote wanapasha viti moto tu. Wengine hawana la maana wanalolifanya kulaposho za kodize pasipo kuzitendea haki. Hukumu inakuja 2015,tutapima mgombea kwa uchangiaji wahoja zinazolenga maslahi ya nchi na watu wake.
 
Hongera CDM Mnaonyesha ukomavu wa kisiasa kwa kuwakaba koo magamba kwa hoja pevu bila kujali wingi wao magamba bungeni.!
 
Chadema wabadili mbinu bungeni, waamue kujenga hoja nzito na wapunguze munkari, panic itawaharibia tu haiwezi kuwasaidia, wako wachache kulingana na ccm kama nao watataka kupambana kimabavu na kujibishana kwa maneno ya mipasho na vurugu basi wajue wanafunika pua na mdomo mchangani, wanakiumiza chama
 
Kwa vile wao wanategemea DOLA na nyie mnamtegemea MUNGU lazima mtawashinda!! Kazeni buti makamanda.
 
Chadema wabadili mbinu bungeni, waamue kujenga hoja nzito na wapunguze munkari, panic itawaharibia tu haiwezi kuwasaidia, wako wachache kulingana na ccm kama nao watataka kupambana kimabavu na kujibishana kwa maneno ya mipasho na vurugu basi wajue wanafunika pua na mdomo mchangani, wanakiumiza chama
well said ndugu yangu.
lakini bahati mbaya hapa jf watu hawaishauri chadema vizuri, hawaoni kama ndo inaporomoka.
muda mwingine inabidi watu wabadilike na wabadilishe strategies.
wabunge wa chadema wameanza kuonekana kama watu wenye nia mbaya
.
 
Hapa Dodoma,mambo yanazidi kupamba moto. CHADEMA ikiwakilishwa na Wabunge wasiofikia 50 Bungeni kati ya karibu Wabunge 300 wa Bunge zima,inachachafya Bunge,inatoa hoja nzito,inasema kweli daima hata kama ukweli unaumiza 'Wakubwa'. CHADEMA wanalichangamsha Bunge kihoja na kimjadala. Ni kweli.

Kama nilivyoripoti katika uzi wangu wa "Dodoma-Mambo ni moto!",hapa Bungeni kuna mkakati wa makusudi wa kuwadhibiti Wabunge wa upinzani hasa CHADEMA na wafananao na hao ili kufanikisha mpango madhubuti wa kuilinda Serikali na CCM kwa namna yoyote ile.

Kutokana na yanayoendelea,mtakubaliana nami kuwa CCM wanabebwa Bungeni. Sina haja ya kurudia matusi na lugha za kuudhi za Mwigulu Nchemba,Juma Nkamia na Peter Serukamba. Na hata kilichotokea jana cha kutolewa nje ya Bunge kwa Mbunge na Wakili Msomi Tundu A.M.Lissu.

Kimsingi,Naibu Spika Job Ndugai na Lissu hawaivi. 'Wana bifu'.Tegemeeni mabishano zaidi mbeleni pale ambapo Ndugai ataongoza Bunge na Lissu akiwemo Bungeni. Ni wazi pia kuwa si Makinda wala Ndugai wanaoliweza Bunge hili.Sababu kuu ni moja:wanawachukulia Wabunge wa CHADEMA kama wakorofi na wanaharakati.

Hapa Dodoma,Mawaziri,Wabunge wa CCM na wale wa upinzani(si wa CHADEMA) wanamimina nyaraka za pongezi kwa kiti cha Spika kwa kuwadhibiti CHADEMA.Pia Mwigulu Nchemba na Livingstone Lusinde aka Kibajaji wanapongezwa kwa kuongoza mashambulizi ya kupoteza malengo ya CHADEMA kihoja na 'kuwaweza'.

Kimsingi,mipango yote hapa Bungeni Dodoma si kujadili hasa Bajeti;ni kuwadhibiti CHADEMA.So amazing! Sijui itakuwaje mwaka huu katika Bajeti na mjadala wake kwakweli!?

Sasa, CHADEMA wasirudi nyuma. Waendelee kupambana.Waeendelee kuwa tegemeo pekee kwa watanzania hapa Bungeni Dodoma. Wasiogope kutolewa nje. Watakaobaki ndani waendeleze mapambano. Kwa mipango yetu hii haramu ya kichama,CCM inafikia mwisho wa kutuongoza hapa Tanzania.

Wewe unasemaje?
VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam(sasa Dodoma)
VUTA-NKUVUTE ,
Mimi nilitegemea mtu kama umesomea sheria ni lazima kufahamu kabisa kuwa msingi wa sheria ni ukweli.

Kama waliosomea sheria wanakuwa waongo, wazandiki na wapiga chapuo, watengeneza stories za kufikirika basi sifahamu wale wasiosomea sheria wana hali gani katika jamii.

Anyway, tutafika tu.
 
Last edited by a moderator:
Ha ha The entire govenment is on defensive, kwenye caucus yao wameambiwa wabaki kuitetea serikali kwa nguvu zote na kupiga vita chadema hawazungumzii kitu kinachojenga nchi ni majisifu,kusifu raisi kusifu CCm,kusifu usalama wa taifa what else do have ,vry frustrating
 
Back
Top Bottom