Dodoma CCM itaweza kujisafisha?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,098
Jitihada za CCM kujisafisha hazitafanikiwa ikiwa fisadi Mkapa hatawekwa kiti moto na kama kuna ushahidi kwamba alivunja sheria za nchi kujipatia mali kwa njia za haramu basi afikishwe mahakamani.

Dodoma CCM itaweza kujisafisha?

Lula wa Ndali-Mwananzela Februari 6, 2008
Raia Mwema

KAMA kuna wakati ambao Chama cha Mapinduzi (CCM) kinatakiwa kionyeshe uwezo wa uongozi basi ni wakati huu.

Kama kuna saa na dakika ambayo wananchi wanaangalia kwa karibu kila hatua inayochukuliwa na CCM basi wakati huo ni sasa.

Macho ya wengi yameelekezwa kwa CCM kuona kama dhidi ya kashfa kubwa ya Benki Kuu (BoT) na nyingine zilizotangulia, chama hicho kinaweza kuyakata mawimbi ya bahari waliyoichafua wana CCM wenyewe.

Ni matumaini yangu kuwa nchi yetu imefikia kilele cha ufisadi na ya kuwa kila kitendo cha kifisadi ambacho tungeweza kukiona tutakuwa tumeshakiona hadi hivi sasa.

Tumeona: Viongozi kutumia madaraka vibaya; upotevu wa mabilioni ya fedha ambayo Serikali ikaamua kuyafuta tu kinyemela tumeona; ununuzi wa ndege kubwa na watu kuapishwa kula majani ili ndege hiyo inunuliwe tumeona; na Ikulu kugeuzwa genge la biashara na kutumiwa mtu kupata mkopo, hilo nalo tumeliona.

Sijui ni kitu gani kingine ambacho kinaweza kutushtua tena. Je, Watanzania watashtuka wakisikia kiongozi amemtwanga mtu risasi mtaani kisa ati "kamtukana"? Je watashtuka wakisikia kuwa waziri fulani na raia walianzisha kampuni wakiwa madarakani na wakitumia ofisi zao? Je tutashtuka huko mbele tukisikia kuwa Gavana wa Benki Kuu hakuwa mwajiriwa wa serikali bali aliingia mkataba (msiniulize na nani na kwa nini) kusimamia idara nyeti kama Benki Kuu halafu leo tunashangaa hakuwa na uchungu nayo?

Ama kweli sabuni ambayo CCM wanataka kutumia kujiosha lazima iwe ni ya aina yake, vinginevyo wasije kuwa wanapojisafisha ndivyo wanavyojichafua. Kwani, hukushangaa pale Spika wa Bunge tukufu anayevalia Joho lililofumwa toka Uingereza aliposema Naibu wake "Asikurupuke" kujadili mambo yenye umuhimu kwa Taifa kwa vile yeye "mwenyewe" hayupo? Au ulielewaje pale ambapo Kigogo huyo wa CCM alipoamua kuweka mijadala ya Bunge kiporo ili aende kwenye ziara ambayo yeye ndiye alialikwa binafsi na si mtu mwingine?

Baada ya watu kupiga kelele na kushangazwa jinsi gani Spika Samuel Sitta anaujasiri wa kuliteka Taifa zima kwa vile tu yeye ni Spika na Katiba inampa nguvu hizo akaamua kuahirisha safari yenyewe!

Kilichonitiba mimi ni kuwa Spika alikuwa anamaanisha kwamba Naibu Spika yuko pale kama picha tu na haruhusiwi kusimamia masuala nyeti na magumu kwa Taifa. Kwa maneno mengine, kusipokuwapo na kashfa kama ya Richmond na BoT Bunge letu linajadili vitu vya kawaida tu na visivyo na umuhimu kwa Taifa.

Binafsi natoa hoja kuwa Spika Sitta ambaye amekuwa akisahihisha watu wengine kwa kutumia lugha mbaya bungeni, awaombe radhi wabunge na Taifa kwa ujumla kwa kumshushia hadhi Naibu Spika (Asisahau kumuomba radhi na Bi. Makinda) hasa kwa kutumia neno "kukurupuka".

Kauli yake ya "Naibu Spika asije kukurupuka" ni kauli ya kibabe, isiyo na chembe ya uungwana na nikiangalia kwa mbali imejaa unyanyasaji wa mfumo dume. Aombe radhi bila kukawia, vinginevyo tutaanza kumuweka kwenye kundi la mafisadi wanaotumia madaraka yao vibaya.

Hata hivyo, tukiacha hilo la Spika Sitta, ni wazi kuwa kama kuna wakati mgumu kisiasa kwa CCM basi ni wakati huu. Inaonekana Rais Jakaya Kikwete ameanza kuona dalili mbaya, na kama si yeye tu bila ya shaka hata viongozi wengine wa ngazi za juu wa chama hicho. Vitendo vya viongozi wa CCM kuzomewa na kupokewa kwa mabango, bila ya shaka, ilikuwa ni kama wito wa kuwaamsha toka usingizini.

Je, hatua ya Rais Kikwete kutangaza "makusudio" ya kuanzisha utaratibu wa kuhakikisha kuwa viongozi wabunge hawajishughulishi na biashara ndiyo hatua muafaka ya CCM kuanza kujisafisha? Je, kuwachukulia hatua za kinidhamu au za kisheria waliohusika na mikataba ya BoT na Richmond na wadogo zao, ndio mwanzo wa kujisafisha?

Naamini kuwa kuna mambo ambayo Serikali ya CCM haina budi kuyafanya kwa sababu ni wajibu wake na ni ya lazima. Lakini kama kweli inataka kujisafisha kuna mambo ya msingi ambayo ni lazima iyasimamie na kuanza kuyatenda ili wananchi warudishe imani kwake. Haitoshi kutoa maneno matamu au ahadi nzuri, ni vitendo tu vinavyoangaliwa. Si ahadi za wakati wa uchaguzi bali ni vitendo baada ya uchaguzi.

Kuhusu ufisadi nchini CCM lazima ikae chini na kusema "imetosha". Wao wawe wa kwanza kuuchukia ufisadi na wasikubali kuwa marafiki na ufisadi. Yaani waukatae ufisadi kama ukoma. Na watafanya hivyo si kwa kukemea majukwaani au bungeni. Haitoshi kuukana ufisadi mbele ya waandishi wa habari.

CCM lazima itengeneze mazingira yatakayofunua ufisadi. Kuna mabadiliko kadhaa ya kisheria ambayo Serikali ya CCM haina budi kuyaangalia kwani ni ya msingi. La kwanza, ni kwenye manunuzi ya Serikali. Hadi sasa mtu anayepoteza shilingi laki moja wizarani na kukosa maelezo yuko sawa na aliyepoteza shilingi milioni moja na akakosa maelezo. Hivi majuzi kwenye kikao cha Bunge tumeambiwa kuwa Serikali imesamehe deni la zaidi ya shilingi bilioni nne ambazo zimepotea kinyemela.

Sasa hatuwezi kuendesha Serikali na utumishi wa umma namna hiyo. Bunge litunge sheria ambayo italazimisha kiongozi au mtumishi wa umma asimamishwe kazi mara moja pindi kiasi fulani kinapopotea au kukosa maelezo na ndani ya siku kadhaa baada ya kufuatia uchunguzi kama hakuna maelezo basi mtu huyo anafikishwa mahakamani kwa ubadhirifu.

Mtindo huu upo kwenye nchi zilizoendelea na ambazo hazina mzaha na fedha za walipa kodi wao. Mtumishi wa umma ambaye anapoteza hata dola moja na haina maelezo anachukuliwa hatua za kinidhamu. Ukifanya kazi kwenye vihoteli vya MacDonald mwisho wa siku droo yako ya fedha haitakiwi kupungua dola mbili. Ukipoteza mara ya kwanza unapewa onyo la mdomo, mara ya pili la maandishi na mara ya tatu mtu anatimuliwa.

Kwenye fedha za Watanzania kusiwe na mswalia Mtume. Afisa wa Serikali ambaye ni mkuu wa idara au kitengo na anawajibika kusimamia fedha, akishindwa kutoa maelezo ya ziliko shilingi elfu 10 za wananchi, hakuna kubembelezana, atakiwa arudishe ndani ya siku kadhaa na anapewa onyo la maandishi. Akipoteza tena anatimuliwa. Yule ambaye chini yake shilingi zaidi ya milioni moja zinatoweka hapewi onyo la maandishi, anatimuliwa kazi.

Ambaye anapoteza zaidi ya shilingi milioni tano zilizokuwa chini yake huyo siyo tu anatimuliwa bali pia anafikishwa mahakamani kwa wizi wa mali ya umma, matumizi mabaya ya ofisi, na ubadhirifu. Hili litakuwa fundisho na onyo kwa watu kuchezea fedha za Watanzania. Sasa hivi wanaotafuna fedha za Watanzania hawana wasiwasi kwani hakuna jinsi ya kuwawajibisha mara moja na badala yake kuna mchakato usio wa lazima wa kuwawajibisha.

La pili na kubwa pia ni kuwa Serikali ya CCM kwa kutumia wabunge wake lazima isimame kweli kuisimamia Serikali. Matatizo mengi kwenye vyombo vingi vya Serikali yanatokana na wabunge wa CCM kutokuwa makini na kuwa goi goi na kusubiri hadi waambiwe nini cha kufanya. Wengi wanaogopa au hawapendi kuonekana wako "kimbelembele" na hivyo wengi wanasubiri kuona nani atakuwa wa kwanza kunyosha kidole.

Imekuwaje leo ATC inanunua ndege mbovu na kutumia zaidi ya shilingi milioni 400 kuifanyika matengenezo na hilo lionekane jambo la kawaida na hakuna mbunge anayepiga kelele? Inakuwaje viongozi wa shirika hilo wajipongeze kwa magari ya kifahahari na hakuna anayesema "imekuwaje"?

Wabunge wa CCM ambao ndio wengi bungeni wangeweza kuliepusha Taifa katika kashfa na viongozi wengi wabovu. Ni ukimya wao na woga wao ndio umeligharimu Taifa. Hata hivyo, kama habari za siku hizi mbili tatu zina ukweli wowote basi kuna mwanga walau kidogo mbele.

Wakati umefika kwa wabunge wa CCM watumie nafasi yao kuanza kukisafisha chama chao kwa kuwatosa viongozi wabovu na ambao wanahatarisha hadhi na jina la CCM. Lakini zaidi wafanye hivyo kwa sababu wanaipenda nchi yao na wana maslahi na hatima ya nchi hiyo. Wakisimama kuitetea Tanzania wananchi watawakumbuka.

Hata hivyo wakiendelea ambavyo wamekuwa wakifanya kwa miaka mingi sasa basi wajue kuwa Watanzania hawatawasamehe na watakumbuka jinsi wabunge hao walivyokuwa wakimya. Ndiyo maana bado naamini kuwa bado wakati wa kuiamini CCM kujisafisha haujafika bado.

Ni kwa sababu hiyo naendelea kutoa wito kuwa wananchi wa Kiteto waikatae CCM na mgombea wake kwani hadi hivi sasa CCM haistahili kiti kingine cha uchaguzi. Hatua zozote watakazochukua kwa sababu ya sakata la Richmond zionekane ni kujaribu kujisafisha. Hata hivyo, kujaribu kujisafisha mbele ya uchaguzi itaonekana ni kampeni tu za uchaguzi.

Wananchi wa Kiteto wataliona hilo na hawatazugwa na mazingaombwe hayo. Ni kwa sababu hiyo naamini kuwa mgombea wa CHADEMA Victor Kimesera ataibuka na ushindi mnono wiki chache zijazo. Ushindi utakaotokana na hamu ya wananchi kutoa onyo na fundisho kwa CCM kuwa ufisadi hauzawadiwi, na uongozi mbovu haurejeshewi fadhila.

CCM haina budi kujisafisha. Hata hivyo, kujisafisha huko lazima kutoke ndani ya mioyo ya viongozi na wanachama wake. Ni lazima kufanywe kwa sababu ya kulipenda Taifa zaidi na kutaka kukirithisha kizazi kijacho Taifa lililo bora, la kisasa na lenye kuheshimu utawala wa sheria. Wakifanya hivyo, CCM itakuwa ni vigumu kuwashinda.
 
CCM kujisafisha wanahitaji ile dawa fulani ya kuharisha inaitwa chumvi ya haluli, wabugie kwa wingi waharishe weeeeee, uozo wote utaisha. Dawa ni nzuri lakini mtu asipokuwa makini inaweza kusababisha kifo cha mtumiaji
 
CCM kujisafisha wanahitaji ile dawa fulani ya kuharisha inaitwa chumvi ya haluli, wabugie kwa wingi waharishe weeeeee, uozo wote utaisha. Dawa ni nzuri lakini mtu asipokuwa makini inaweza kusababisha kifo cha mtumiaji

Jitihada za CCM kujisafisha hazitafanikiwa ikiwa fisadi Mkapa hatawekwa kiti moto na kama kuna ushahidi kwamba alivunja sheria za nchi kujipatia mali kwa njia za haramu basi afikishwe mahakamani.

Dodoma CCM itaweza kujisafisha?

Lula wa Ndali-Mwananzela Februari 6, 2008
Raia Mwema

KAMA kuna wakati ambao Chama cha Mapinduzi (CCM) kinatakiwa kionyeshe uwezo wa uongozi basi ni wakati huu.

Kama kuna saa na dakika ambayo wananchi wanaangalia kwa karibu kila hatua inayochukuliwa na CCM basi wakati huo ni sasa.

Macho ya wengi yameelekezwa kwa CCM kuona kama dhidi ya kashfa kubwa ya Benki Kuu (BoT) na nyingine zilizotangulia, chama hicho kinaweza kuyakata mawimbi ya bahari waliyoichafua wana CCM wenyewe.

Ni matumaini yangu kuwa nchi yetu imefikia kilele cha ufisadi na ya kuwa kila kitendo cha kifisadi ambacho tungeweza kukiona tutakuwa tumeshakiona hadi hivi sasa.

Tumeona: Viongozi kutumia madaraka vibaya; upotevu wa mabilioni ya fedha ambayo Serikali ikaamua kuyafuta tu kinyemela tumeona; ununuzi wa ndege kubwa na watu kuapishwa kula majani ili ndege hiyo inunuliwe tumeona; na Ikulu kugeuzwa genge la biashara na kutumiwa mtu kupata mkopo, hilo nalo tumeliona.

Sijui ni kitu gani kingine ambacho kinaweza kutushtua tena. Je, Watanzania watashtuka wakisikia kiongozi amemtwanga mtu risasi mtaani kisa ati “kamtukana”? Je watashtuka wakisikia kuwa waziri fulani na raia walianzisha kampuni wakiwa madarakani na wakitumia ofisi zao? Je tutashtuka huko mbele tukisikia kuwa Gavana wa Benki Kuu hakuwa mwajiriwa wa serikali bali aliingia mkataba (msiniulize na nani na kwa nini) kusimamia idara nyeti kama Benki Kuu halafu leo tunashangaa hakuwa na uchungu nayo?

Ama kweli sabuni ambayo CCM wanataka kutumia kujiosha lazima iwe ni ya aina yake, vinginevyo wasije kuwa wanapojisafisha ndivyo wanavyojichafua. Kwani, hukushangaa pale Spika wa Bunge tukufu anayevalia Joho lililofumwa toka Uingereza aliposema Naibu wake “Asikurupuke” kujadili mambo yenye umuhimu kwa Taifa kwa vile yeye “mwenyewe” hayupo? Au ulielewaje pale ambapo Kigogo huyo wa CCM alipoamua kuweka mijadala ya Bunge kiporo ili aende kwenye ziara ambayo yeye ndiye alialikwa binafsi na si mtu mwingine?

Baada ya watu kupiga kelele na kushangazwa jinsi gani Spika Samuel Sitta anaujasiri wa kuliteka Taifa zima kwa vile tu yeye ni Spika na Katiba inampa nguvu hizo akaamua kuahirisha safari yenyewe!

Kilichonitiba mimi ni kuwa Spika alikuwa anamaanisha kwamba Naibu Spika yuko pale kama picha tu na haruhusiwi kusimamia masuala nyeti na magumu kwa Taifa. Kwa maneno mengine, kusipokuwapo na kashfa kama ya Richmond na BoT Bunge letu linajadili vitu vya kawaida tu na visivyo na umuhimu kwa Taifa.

Binafsi natoa hoja kuwa Spika Sitta ambaye amekuwa akisahihisha watu wengine kwa kutumia lugha mbaya bungeni, awaombe radhi wabunge na Taifa kwa ujumla kwa kumshushia hadhi Naibu Spika (Asisahau kumuomba radhi na Bi. Makinda) hasa kwa kutumia neno “kukurupuka”.

Kauli yake ya “Naibu Spika asije kukurupuka” ni kauli ya kibabe, isiyo na chembe ya uungwana na nikiangalia kwa mbali imejaa unyanyasaji wa mfumo dume. Aombe radhi bila kukawia, vinginevyo tutaanza kumuweka kwenye kundi la mafisadi wanaotumia madaraka yao vibaya.

Hata hivyo, tukiacha hilo la Spika Sitta, ni wazi kuwa kama kuna wakati mgumu kisiasa kwa CCM basi ni wakati huu. Inaonekana Rais Jakaya Kikwete ameanza kuona dalili mbaya, na kama si yeye tu bila ya shaka hata viongozi wengine wa ngazi za juu wa chama hicho. Vitendo vya viongozi wa CCM kuzomewa na kupokewa kwa mabango, bila ya shaka, ilikuwa ni kama wito wa kuwaamsha toka usingizini.

Je, hatua ya Rais Kikwete kutangaza “makusudio” ya kuanzisha utaratibu wa kuhakikisha kuwa viongozi wabunge hawajishughulishi na biashara ndiyo hatua muafaka ya CCM kuanza kujisafisha? Je, kuwachukulia hatua za kinidhamu au za kisheria waliohusika na mikataba ya BoT na Richmond na wadogo zao, ndio mwanzo wa kujisafisha?

Naamini kuwa kuna mambo ambayo Serikali ya CCM haina budi kuyafanya kwa sababu ni wajibu wake na ni ya lazima. Lakini kama kweli inataka kujisafisha kuna mambo ya msingi ambayo ni lazima iyasimamie na kuanza kuyatenda ili wananchi warudishe imani kwake. Haitoshi kutoa maneno matamu au ahadi nzuri, ni vitendo tu vinavyoangaliwa. Si ahadi za wakati wa uchaguzi bali ni vitendo baada ya uchaguzi.

Kuhusu ufisadi nchini CCM lazima ikae chini na kusema “imetosha”. Wao wawe wa kwanza kuuchukia ufisadi na wasikubali kuwa marafiki na ufisadi. Yaani waukatae ufisadi kama ukoma. Na watafanya hivyo si kwa kukemea majukwaani au bungeni. Haitoshi kuukana ufisadi mbele ya waandishi wa habari.

CCM lazima itengeneze mazingira yatakayofunua ufisadi. Kuna mabadiliko kadhaa ya kisheria ambayo Serikali ya CCM haina budi kuyaangalia kwani ni ya msingi. La kwanza, ni kwenye manunuzi ya Serikali. Hadi sasa mtu anayepoteza shilingi laki moja wizarani na kukosa maelezo yuko sawa na aliyepoteza shilingi milioni moja na akakosa maelezo. Hivi majuzi kwenye kikao cha Bunge tumeambiwa kuwa Serikali imesamehe deni la zaidi ya shilingi bilioni nne ambazo zimepotea kinyemela.

Sasa hatuwezi kuendesha Serikali na utumishi wa umma namna hiyo. Bunge litunge sheria ambayo italazimisha kiongozi au mtumishi wa umma asimamishwe kazi mara moja pindi kiasi fulani kinapopotea au kukosa maelezo na ndani ya siku kadhaa baada ya kufuatia uchunguzi kama hakuna maelezo basi mtu huyo anafikishwa mahakamani kwa ubadhirifu.

Mtindo huu upo kwenye nchi zilizoendelea na ambazo hazina mzaha na fedha za walipa kodi wao. Mtumishi wa umma ambaye anapoteza hata dola moja na haina maelezo anachukuliwa hatua za kinidhamu. Ukifanya kazi kwenye vihoteli vya MacDonald mwisho wa siku droo yako ya fedha haitakiwi kupungua dola mbili. Ukipoteza mara ya kwanza unapewa onyo la mdomo, mara ya pili la maandishi na mara ya tatu mtu anatimuliwa.

Kwenye fedha za Watanzania kusiwe na mswalia Mtume. Afisa wa Serikali ambaye ni mkuu wa idara au kitengo na anawajibika kusimamia fedha, akishindwa kutoa maelezo ya ziliko shilingi elfu 10 za wananchi, hakuna kubembelezana, atakiwa arudishe ndani ya siku kadhaa na anapewa onyo la maandishi. Akipoteza tena anatimuliwa. Yule ambaye chini yake shilingi zaidi ya milioni moja zinatoweka hapewi onyo la maandishi, anatimuliwa kazi.

Ambaye anapoteza zaidi ya shilingi milioni tano zilizokuwa chini yake huyo siyo tu anatimuliwa bali pia anafikishwa mahakamani kwa wizi wa mali ya umma, matumizi mabaya ya ofisi, na ubadhirifu. Hili litakuwa fundisho na onyo kwa watu kuchezea fedha za Watanzania. Sasa hivi wanaotafuna fedha za Watanzania hawana wasiwasi kwani hakuna jinsi ya kuwawajibisha mara moja na badala yake kuna mchakato usio wa lazima wa kuwawajibisha.

La pili na kubwa pia ni kuwa Serikali ya CCM kwa kutumia wabunge wake lazima isimame kweli kuisimamia Serikali. Matatizo mengi kwenye vyombo vingi vya Serikali yanatokana na wabunge wa CCM kutokuwa makini na kuwa goi goi na kusubiri hadi waambiwe nini cha kufanya. Wengi wanaogopa au hawapendi kuonekana wako “kimbelembele” na hivyo wengi wanasubiri kuona nani atakuwa wa kwanza kunyosha kidole.

Imekuwaje leo ATC inanunua ndege mbovu na kutumia zaidi ya shilingi milioni 400 kuifanyika matengenezo na hilo lionekane jambo la kawaida na hakuna mbunge anayepiga kelele? Inakuwaje viongozi wa shirika hilo wajipongeze kwa magari ya kifahahari na hakuna anayesema “imekuwaje”?

Wabunge wa CCM ambao ndio wengi bungeni wangeweza kuliepusha Taifa katika kashfa na viongozi wengi wabovu. Ni ukimya wao na woga wao ndio umeligharimu Taifa. Hata hivyo, kama habari za siku hizi mbili tatu zina ukweli wowote basi kuna mwanga walau kidogo mbele.

Wakati umefika kwa wabunge wa CCM watumie nafasi yao kuanza kukisafisha chama chao kwa kuwatosa viongozi wabovu na ambao wanahatarisha hadhi na jina la CCM. Lakini zaidi wafanye hivyo kwa sababu wanaipenda nchi yao na wana maslahi na hatima ya nchi hiyo. Wakisimama kuitetea Tanzania wananchi watawakumbuka.

Hata hivyo wakiendelea ambavyo wamekuwa wakifanya kwa miaka mingi sasa basi wajue kuwa Watanzania hawatawasamehe na watakumbuka jinsi wabunge hao walivyokuwa wakimya. Ndiyo maana bado naamini kuwa bado wakati wa kuiamini CCM kujisafisha haujafika bado.

Ni kwa sababu hiyo naendelea kutoa wito kuwa wananchi wa Kiteto waikatae CCM na mgombea wake kwani hadi hivi sasa CCM haistahili kiti kingine cha uchaguzi. Hatua zozote watakazochukua kwa sababu ya sakata la Richmond zionekane ni kujaribu kujisafisha. Hata hivyo, kujaribu kujisafisha mbele ya uchaguzi itaonekana ni kampeni tu za uchaguzi.

Wananchi wa Kiteto wataliona hilo na hawatazugwa na mazingaombwe hayo. Ni kwa sababu hiyo naamini kuwa mgombea wa CHADEMA Victor Kimesera ataibuka na ushindi mnono wiki chache zijazo. Ushindi utakaotokana na hamu ya wananchi kutoa onyo na fundisho kwa CCM kuwa ufisadi hauzawadiwi, na uongozi mbovu haurejeshewi fadhila.

CCM haina budi kujisafisha. Hata hivyo, kujisafisha huko lazima kutoke ndani ya mioyo ya viongozi na wanachama wake. Ni lazima kufanywe kwa sababu ya kulipenda Taifa zaidi na kutaka kukirithisha kizazi kijacho Taifa lililo bora, la kisasa na lenye kuheshimu utawala wa sheria. Wakifanya hivyo, CCM itakuwa ni vigumu kuwashinda.

Nadhani kwa yaliyotokea Bungeni jana yanatosha kupata jibu. Nimefurahishwa jinsi wabunge wa CCM walivyotoa hoja zao bila woga na kwa uchungu wa nchi yao, haya ni mabadiliko yanayotakiwa kwa hivi sasa, maana hii ndio demokrasia ya kweli. Mwelekeo tunauona. Kwa hali hiyo usafi utakuwepo bila shaka kwani kila atakaepewa majukumu ataogopa kurudia haya. Tusubiri.
 
Back
Top Bottom