Mmmh japo habari hii haina detail za kutosha ila kwa matukio ya karibuni nadhani tunakoelekea si kwema...huu mpishano wa wananchi kujichukulia sheria mkononi na polisi ku enforce sheria isivyotakiwa unatuelekeza kubaya!
Waziri wa mambo ya Ndani Mathias Chikawe amesema Bungeni sasa hivi kuwa polisi ameuawa leo mjini Dodoma wakati akijaribu kumuokoa mtoto ambaye alikuwa "anauawa" na mzazi wake! Anasema mtoto ameokolewa.
Hata hivyo, hakusema mtoto alitaka kuuawa kivipi na wala hajasema polisi kauawa vipi mbali na kuonya wananchi na chuki dhidi ya polisi!
Hoja hii ijadiliwe bungeni; ni hatari sana kwa usalama wa walinzi wa raia na mali zao.
Angeonya ccm kuwa na chuki kwa wananchi kupitia polisi.ameonya wananchi na chuki dhidi ya polisi? me nadhan angeonya polisi na chuki dhidi ya watanzania!
Waueni tu hila kama nao wengikuwa wauaji km mnavyodai sidhani km mmengukuwa mnaandika utumbo huo kwa amani labda niulize kuna askar aliuwa raia akabaki salama na kazi yake si wote wapo jela? ss mnaposhabikia binadamu mwenzio kuuliwa we unajiona uko salama kbs?
Hapo ni sawa na nyani kucheka wakt chaka linawaka moto wkt jion atakosa pa kulala. Ebu tukemee maovu bila kujali ni nani wala nani kila raia ana haki ya kuishi na mungu hapendi tuwe wanyama kiac hicho.
Alikuwa ameenda kamata mtuhumiwa. Wakamshambulia na kutenganisha kichwa na kiwiliwili.
Mytake: Askari wasipojirekebisha watauawa sana.
UPDATES: