Dodoma: Askari Polisi auliwa na raia

Dodoma: Askari Polisi auliwa na raia

KUNDULE

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2015
Posts
318
Reaction score
177
Alikuwa ameenda kamata mtuhumiwa. Wakamshambulia na kutenganisha kichwa na kiwiliwili.

Mytake: Askari wasipojirekebisha watauawa sana.

UPDATES:
Ni Hiv imetokea chang'ombe Dodoma askari alikuwa ameenda kumkata jamaa ambaye ni mtuhumiwa, ndipo hapo alipokutana na masaibu hayo kutoka kwa mtuhumiwa akishirikiana na masela.

Waziri wa mambo ya Ndani Mathias Chikawe amesema Bungeni sasa hivi kuwa polisi ameuawa leo mjini Dodoma wakati akijaribu kumuokoa mtoto ambaye alikuwa "anauawa" na mzazi wake! Anasema mtoto ameokolewa.

Hata hivyo, hakusema mtoto alitaka kuuawa kivipi na wala hajasema polisi kauawa vipi mbali na kuonya wananchi na chuki dhidi ya polisi!

rest in peace kamanda Joseph Isaack Swai my classmate na jirani yangu kitaani Arusha. wana PCB longido high school tutakukumbuka daima kwa ucheshi wako.. polisi jamii Dodoma imepoteza mtu makini sana. i will dearly miss you bro. pumzika kwa amani

==============================================
TAARIFA YA POLISI


Leo tarehe 04.02.2015 majira ya saa 11:00 limetokea tukio baya na la kusikitisha la kuuawa kwa askari wa Polisi Mkoa wa Dodoma namba G.7168 PC JOSEPH ISACK SWAI.

Chanzo cha kuuawa huyu askari ni kwamba alipigiwa simu na Mtendaji wa Mtaa wa chang'ombe juu hapa Dodoma Mjini akimjulisha kuwa amepokea taarifa ofisini kwake kutoka kwa OLIVER BALTAZARI, MIAKA 52, MKAZI WA CHANG'OMBE JUU

kuwa kijana wake aitwaye TISI S/O SIRILI MALYA ana mtesa motto wake mdogo wa miezi nane aitwaye VALERIAN TISI MALYA na anahisi labda ameshamuua kwani motto huyo halii tena.

Alichofanya mtendaji huyu ni kumpigia askari wetu huyo simu naye akaenda hadi katika Ofisi ya huyo Mtendaji wa Mtaa.

Waliongozana wote wakiwa pamoja na kijana mmoja hadi anakoishi huyo TISI SIRILI MALYA. Walipofika askari aligonga mlango akijitambulisha kuwa yeye ni askari hivyo atoke nje.

Alichofanya mtuhumiwa huyo ni kumnyanyua mtoto wake mdogo wa miezi nane kwa mkono mmoja miguu juu kichwa chini na kutaka kumkata kwa panga na kusema namkata shingo na sitaki kuona mtu.

Askari aliamua kumwokoa mtoto huyo na alipomrukia mtuhumiwa kwa bahati mbaya aliteleza na ndipo mtuhumiwa akamkata kichwani askari wetu na akadondoka chini kutokana na jeraha kubwa alilomsababishia.

Hata hivyo mtuhumiwa huyo aliendelea kumkatakata na Mtendaji na kijana waliyekuwa naye ambaye ni maratibu wa watoto wanaoishi katika mazingira magumu iliwabidi kukimbia huku wakipiga kelele kuomba msaada.

Mtuhumiwa baada ya kufanya kitendo hicho cha kinyama alikimbia huku nguo zake zikiwa zimetapakaa damu akiwa na panga mkononi.

Askari huyu muda mfupi kabla ya tukio hili alikuwa ametokea katika kituo cha Redio cha Dodoma FM kwa ajili ya kuandaa kipindi cha kuielimisha jamii juu ya ulinzi wa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) tunapoelekea kipindi cha uchaguzi, kwani mbali na kazi anazofanya mojawapo ni kushiriki katika vipindi vya kutoa elimu ya Polisi Jamii hapa mkoani Dodoma.

Msako bado unaendelea ili kuweza kumtia nguvuni mtuhumiwa huyu aliyesababisha kifo cha askari wetu wakati alipojitolea maisha ya ili kumwokoa huyo mtoto mdogo. Tuinazidi kuomba msaada wa wananchi popote pale watakapomuona TISI S/O SIRILI MALYA, MIAKA 29, MCHAGA

Ambaye ni maji ya kunde, mwembamba, siyo mrefu sana saizi ya kati alikuwa amevaa suruali rangi ya blue iliyopauka na T-Shirt rangi ya dark blue na kofia nyeupe yenye alama nyekundu ili tuweze kumkamata na kumfikisha mahakamani. Imetolewa na:

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi – Misime D.A (SACP)

Marehemu wakati wa uhai wake:
attachment.php

attachment.php

 
Tunaomba utueleze vizuri, mtuhumiwa wa kitu gani na alikuwa na uhusiano gnai na wananchi na nini kilichotokea hadi wananchi wakaanza kumfanya hivyo?

Ni jambo la huzuni sana. Ccm inatupeleka kubaya sana. Wananchi wanakuwa na uchungu na serikali kiasi cha kuwa na uadui n achuki kubwa namna hii? Nani aliwaamrisha wampige yule askari? Aliwakosea nini? Jamani ccm acheni upumbavu. Mnaua Tanzania Yetu.
 
Mmmh japo habari hii haina detail za kutosha ila kwa matukio ya karibuni nadhani tunakoelekea si kwema...huu mpishano wa wananchi kujichukulia sheria mkononi na polisi ku enforce sheria isivyotakiwa unatuelekeza kubaya!
 
alikuwa ameenda kamata mtuhumiwa.wakamshambulia na kutenganisha kichwa na kiwiliwili.mytake:askari wasipojirekebisha watauawa sana

Hata mie nimesikia, jamaa kampiga mapanga askari hii imetokea chang"ombe Dodoma, askari alitaka kumkamata jamaa baada ya kumpiga mtoto
 
Ni Hiv imetokea chang'ombe Dodoma askari alikuwa ameenda kumkata jamaa ambaye ni mtuhumiwa, ndipo hapo alipokutana na masaibu hayo kutoka kwa mtuhumiwa akishirikiana na masela.
 
Safi kabisa.. Hahaa, mh. Lipumba upo?
 
Alikuwa ameenda kamata mtuhumiwa. Wakamshambulia na kutenganisha kichwa na kiwiliwili.

Mytake: Askari wasipojirekebisha watauawa sana.


Habari nyingine huwa zinafanya jioni yaki kuwa nzuriiii na kukupa sababu ya kupiga hata beer mbili tatu za kusheherekea. Safi sana raia WEMA wa Dodoma. Safi mno.
 
Waziri wa mambo ya Ndani Mathias Chikawe amesema Bungeni sasa hivi kuwa polisi ameuawa leo mjini Dodoma wakati akijaribu kumuokoa mtoto ambaye alikuwa "anauawa" na mzazi wake! Anasema mtoto ameokolewa.

Hata hivyo, hakusema mtoto alitaka kuuawa kivipi na wala hajasema polisi kauawa vipi mbali na kuonya wananchi na chuki dhidi ya polisi!
 
Huyo aliyemuua ni dini gani? Maana watu wanashangilia sana askari kuuawa. Nijibuni kisha niwaambie mantiki.....
 
Kuna maeneo ni vitovu vya uhalifu kama niko sahihi na kumbukumbu zangu hilo eneo ni moja ya maeneo korofi sasa swali mpaka kunakuwa labelled kwa nini kuliachiwa.

Huyu askari alikuwa anapita njia au? Kama alitokea kituoni kwa nini alikuwa peke yake!? Kama ilikuwa ni lazima kwenda peke yake, usalama wake ulikuwa juu ya nani/ nini!?

Mchelea mwana kulia....
 
Angeonya ccm kuwatumia polisi kunyanyasa raia wasioikubali ccm. Chuki ya ccm dhidi ya upinzani kwa kutumia polisi ikomeshwe.
 
Back
Top Bottom