DOKEZO Dodoma Area C ina miundombinu mibovu sana

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Jiji la Dodoma limekuwa na miundombinu mibovu ya mitaro na machemba haswa eneo la Area C.

Tunahitaji Serikali ishughulike na kurekebisha mitaro na machemba kumalizika haswa kabla janga la mvua kubwa kutukumba na kuadhirika kwa ukubwa kama Hanang Manyara.

Mitaro imechimbwa vibaya na haijamalizika imejaa uchafu na mchanga haipitishi maji mvua kidogo tu ikitokea huwezi jua ukingo wa barabara uko wapi kusababisha ajali na machemba yamechimbwa na kuachwa wazi bila kufukiwa kabisa mvua ikinyesha huwezi vumbua mashimo hayo.

Na kazi ilianza miaka mitatu Sasa imeshindwa kumalizika Bora warudi warudishe kama ilivyokuwaga.

Viongozi fungukeni mtupatie hali yetu
 
Back
Top Bottom