DNA watoto si wetu - Wanawake Mnatuambiaje hapa ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DNA watoto si wetu - Wanawake Mnatuambiaje hapa ?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mwiba, Jul 10, 2010.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  `Nusu ya waliopima DNA watoto si wao`
  Na Mwandishi wetu  9th July 2010  Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, imesema nusu ya watu waliokwenda kupima vinasaba (DNA) kutokana na kuwa na mashaka haya na yale, vipimo vimeonyesha kuwa si wazazi halisi wa watoto waliopimwa.
  Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Vifaa na Matengenezo wa ofisi hiyo, Emmanuel Gwae, wakati akizungumza katika maonyesho ya biashara yanayofanyika katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere.
  Alisema tangu huduma hiyo ianze kutolewa na taasisi hiyo mwaka 2005, watu zaidi ya 2,000 walifika kupata vipimo kujua uhalisia wa watoto wao.
  Alisema karibu nusu ya watu hao waliofika na kupimwa ilibainika kuwa watoto waliokuwa nao hawakuwa wa kwao.
  Alisema idadi ya watu wanaokwenda kupata vipimo imekuwa ikiongezeka kuliko miaka iliyopita.
  “Huduma hii ni kama imechelewa maana watu wanakuja kwa wingi sana kupima uhalisia wa watoto wao na wengi wanaopimwa wanakuta watoto si wao,” alisema.
  Alisema kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha matokeo hayo ikiwemo kubadilishana watoto wakati wa kujifungua.
  Alisema katika hospitali zenye mlundikano mkubwa wa wanawake wanaojifungua, baadhi ya wanawake kwa makusudi wanaweza kuwabadilishia wenzao watoto.
  Alisema hali hiyo pia inaweza kutokea hata bila kukusudia kutokana na mazingira ya hospitali.
  Alisema vipimo vya DNA hugharimu shilingi 300,000 na mhusika anaweza kupata majibu ndani ya wiki moja.
  Alisema kabla ya mhusika kwenda kupata vipimo lazima apeleke kwa mkemia barua kutoka mahakamani, kwa wakili au ofisi ya ustawi wa jamii na kueleza sababu ya kutaka kupima.
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Jul 10, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,194
  Trophy Points: 280
  Lazima ujue kwamba, mtu anayeenda kupima maana yake tayari ana shaka, kwa hiyo usitegemee kwamba matokeo haya yako reflective of the general population.

  Lakini hata baada ya kujua hilo, nusu ni figure iliyo very high. Ukimwi utaisha kweli ?
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Jul 11, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  mbona hii habari ni ya muda mrefu sana; inazungushwa zungushwa weee
   
 4. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #4
  Jul 11, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tatizo ni lipi tena? anyway--inaonekana uaminifu katika ndoa umekwazika kwa kiasi kikubwa--in brief, hakuna tena uaminifu ktk ndoa!! very unfotunate..
   
 5. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #5
  Jul 11, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Na ukihesabu na wanaume wanaopata watoto nje ya ndoa zao au kuwa na vimada lazima utambue kuwa Tanzania bila ukimwi haiwezikani
   
 6. Q

  Qadhi JF-Expert Member

  #6
  Jul 11, 2010
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 235
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama daktari(specialist) anaweza ku operate mguu badala ya kichwa na kichwa badala ya mguu...then uzembe wa nurses kubadilisha watoto utakuwa haulezeki...especially neither of the parents cares.Ni jambo dogo tu la kuhakikisha kuwa mtoto na mama wanawekwa tags immediately after delivery inakuwa ngumu sana ndani ya Bongo.
  Sometimes tunagundua kwamba one is NOT biologic father to a kid pale tunapohitaji blood transfusion na kuona ABO are completely un matching.....ukimfanya counselling mother kwa ahadi kuwa hutotoa siri anaweza kukueleza ukweli kwamba ali cheat na unfortunately kupata mtoto.

  Awesome
   
 7. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #7
  Jul 11, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Nami nahisi nina mbegu yangu kaya flani hapa dar
   
 8. katelero

  katelero JF-Expert Member

  #8
  Jul 11, 2010
  Joined: May 31, 2010
  Messages: 529
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0

  mmh
   
 9. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #9
  Jul 11, 2010
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Niliposoma hiyo kitu wazo la kwanza lilikuwa ni hii ni "Marketing Campaign" hawa jamaa wa kupima DNA, wanawatisha watu wapate wateja.
   
 10. roselyne1

  roselyne1 JF-Expert Member

  #10
  Jul 11, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  lol
   
Loading...