Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,916
Wakuu habarini za wakati huu,
Kuna swali ambalo nimekuwa najiuliza sana na nimekosa jibu na hili nadhani naweza kupata jibu hapa kwenu wakuu maana hapa hakuna kinachoweza kuharibika.
Kimsingi nina maswali mawili...
1; Hili la kwanza ni kuhusu DNA [vinasaba]
Binadamu tunarithi vinasaba hivi kutoka kwa wazazi wetu na wazazi wetu nao hivyo hivyo pia,inaelezwa kuwa chanzo cha binadamu ni kimoja,yaani tuwe tuliumbwa au iwe ni kwa kupitia evolution bado haiondoi ukweli kuwa huko tulikotokea chanzo ni kimoja.
Sasa kama tuna chanzo kimoja na sisi tunarithi hivi vinasaba kutoka kwa wazazi na wazazi walirithi kutoka kwa wazazi wao, nao wazazi wa wazazi wetu walirithi hivyo hivyo na kuendelea, inakuwaje vinasaba hivi vinakuja kutofautiana kwa mtu mmoja hadi mwingine wakati chain yetu inatuelekeza kwenye chanzo kimoja?
2; Hili la pili ni kuhusu hobby
Ni kitu gani kinasababisha mtu anakuwa anapenda kitu fulani?
Kama ni malezi au wazazi, inakuwaje watoto wawili wanakulia kwenye mazingira yale yale na wanazaliwa na wazazi wale wale halafu wanakuja kuwa na hobby tofauti?
Unakuta mmoja hapendi kabisa chai ya maziwa na mwingine bila kuinywa bado anakuwa hajaiona siku, hili linasababishwa na kitu gani?
Karibuni kwa majibu.
CC: Monstgala Ishmael ......