Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,565
- 7,988
Salam wana JF.
Baada ya kukamilisha ziara ndefu na iliyojaa mafanikio katika mkoa wa Manyara, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni Kiongozi Mkuu wa upinzani nchini, kesho anatarajiwa kuzungumza na watanzania kupitia mkutano wa hadhara utakaofanyika katika viwanja vya Mbagala Zakhem jijini Dar es salaam.
Kabla ya mkutano huo wa hadhara Dkt. Slaa atapata fursa ya kukutana na timu inayoratibu kampeni za mgombea wetu wa udiwani katika kata ya Mianzini kamanda Cuthbert Saulo Ngwatta (almaarufu Mdudu) ambaye ndiye chaguo la wana mianzini.
Katika ziara hiyo Katibu mkuu katika kata ya Mianzini, ataambatana na viongozi wa kanda ya Pwani iliyo chini ya uenyekiti wa msomi na nguli Profesa Abdallah Safari.
Makamanda pamoja na wananchi waishio wilaya ya Temeke hasa maeneo ya jirani na Mbagala mnakaribishwa kumlaki na kumsikiliza kiongozi mahiri wa upinzani nchini kusikia atakuwa na ujumbe gani kwa watanzania hiyo kesho.
Nawasilisha. Peoples Power!