utaifakwanza
JF-Expert Member
- Feb 1, 2013
- 14,193
- 2,815
Watu wa mbagala watamchora tu
Salam wana JF.
Baada ya kukamilisha ziara ndefu na iliyojaa mafanikio katika mkoa wa Manyara, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni Kiongozi Mkuu wa upinzani nchini, kesho anatarajiwa kuzungumza na watanzania kupitia mkutano wa hadhara utakaofanyika katika viwanja vya Mbagala Zakhem jijini Dar es salaam.
Kabla ya mkutano huo wa hadhara Dkt. Slaa atapata fursa ya kukutana na timu inayoratibu kampeni za mgombea wetu wa udiwani katika kata ya Mianzini kamanda Cuthbert Saulo Ngwatta (almaarufu Mdudu) ambaye ndiye chaguo la wana mianzini.
Katika ziara hiyo Katibu mkuu katika kata ya Mianzini, ataambatana na viongozi wa kanda ya Pwani iliyo chini ya uenyekiti wa msomi na nguli Profesa Abdallah Safari.
Makamanda pamoja na wananchi waishio wilaya ya Temeke hasa maeneo ya jirani na Mbagala mnakaribishwa kumlaki na kumsikiliza kiongozi mahiri wa upinzani nchini kusikia atakuwa na ujumbe gani kwa watanzania hiyo kesho.
Nawasilisha. Peoples Power!
Kamanda Molemo hatujaonana muda mrefu sana bila shaka kesho tutakuwa pamoja.
ina maana dr slaa amefilisika sana kisiasa kiasi cha kuongoza kampeni za udiwani?
Kamanda molemo, ubarikiwe sana.popote kamanda molemo anapokuwa hapaharibiki kitu.tuko nyuma yako mkuu molemo.shukrani sana.
ina maana dr slaa amefilisika sana kisiasa kiasi cha kuongoza kampeni za udiwani?
ina maana dr slaa amefilisika sana kisiasa kiasi cha kuongoza kampeni za udiwani?
nyama yake mnampumulia
Watu wa mbagala watamchora tu
atatangazwa na nani na nani atamlinda wakati amewatukana vyombo vyote vya dola
atatangazwa na nani na nani atamlinda wakati amewatukana vyombo vyote vya dola
Rais ambaye hukutangazwa kutokana na tume chafu ya uchaguzi pole nakazi za chama karibu mianzini kuimarisha chama 2015 utatangazwa iam sure!!
Haya ya udiwani tuyaache , anataka kutumia jukwaa hilo kuongea na wananchi , yaani unataka Slaa awe Jangwani wakati kuna kampeni Mianzini ? Hebu Mswalie Mtume bhana !