Dkt. Shein aipongeza China kwa kusaidia maendeleo Zanzibar

Jul 10, 2017
22
33
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha miradi ya maendeleo sambamba na kukuza uhusiano uliopo.

Dk. Shein amesema hayo alipokuwa na mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Watu wa China Cai Defeng, aliopo nchini Tanzania kwa ziara ya siku sita kufuatia mwaliko wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Yustino Ndugai.

Katika mazungumzo hayo, Rais Dk. Shein alitoa shukurani kwa Serikali ya Watu wa China kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzbar katika kuendeleza miradi mbali mbali ya maendeleo ambayo imekuwa chachu katika kukuza uchumi wa Zanzibar. Rais Dk. Shein alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamini uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliopo kati yake na Jamhuri ya Watu wa China ambapo ujio wa kiongozi huyo unathibitisha ukweli huo.

Sambamba na hayo, Rais Dk. Shein ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar alipongeza uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya (CCM) na chama cha Kikomunisti cha China (CPC) chini ya uongozi wa Rais Xi Jinping wanchi hiyo.

Dk. Shein alizipongeza hatua za Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kuunga mkono jitihada za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo afya, elimu, kilimo, maji safi na salama, miundombinu, viwanda na mengineyo Dk. Shein alipongeza juhudi kubwa zinazochukuliwa na nchi hiyo katika kutoa nafasi za masomo kwa wanafunzi kutoka Zanzibar sambamba na mashirikiano yaliopo kutoka Jimbo la Jangsu katika kuimarisha sekta ya afya.

SHEIN.jpeg
 
Sijui waafrika nani katuloga??Ivi kupata msaada ni kitu cha kufurahisha kweli? yani ni sawa na baba afurahi mke wake kununuliwa nguo na mwanaume mwingine!!

Wakasome kitabu cha Dead Aid by Dumbisa Moyo!
 
Ni sifa kubwa sana kwa mkuu wa nchi masikini kuwa na uwezo wa kushawishi wawekezaji wa kimataifa au kupewa mikopo na nchi zenye uchumi mkubwa ambazo mara nyingi husita kutoa mikopo kwa sababu za kuhofia kutumiwa vibaya na vi nchi hivi masikini..

Kupongeza hadharani ni kutangaza kwamba serikali chini ya uongozi wake ina uwezo wa kushawishi taifa kubwa kama China kutoa msaada kwa nchi yake.
 
Sambamba na hayo, Rais Dk. Shein ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar alipongeza uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya (CCM) na chama cha Kikomunisti cha China (CPC) chini ya uongozi wa Rais Xi Jinping wanchi hiyo.

Duh!!!! kumbe kuna haya Mimi nilikua hata siyaelewi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom