Dkt. Nshala: Afunguka yaliojili kwenye kesi ya mgawanyo wa mali wa CHADEMA

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,436
Reaction score
5,234
Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Rugemeleza Nshala, akizungumza kwa niaba ya Jopo la Mawakili wa Chama hicho amesema kuwa Mahakama ya Rufaa imesikiliza na kupokea hoja zote za maombi ya marejeo ya mwenendo wa kesi ya mgawanyo wa mali za chama hicho, kesi iliyofunguliwa na Saidi Issa Mohamed na wenzake dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema na Katibu Mkuu wa chama.

Dkt. Nshala ameyasema hayo leo Machi 24, 2026 jijini Dodoma katika viunga vya Mahakama (Judiciary Square) ambapo amebainisha kuwa Mahakama imesikiliza shauri la mapitio manne, na kwamba waliweza kuwasilisha mbele ya majaji hoja zote walizodai kuwa ni uvunjifu wa taratibu uliofanywa na Jaji Mwanga wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo katika Mahakama Kuu, jambo ambalo kwa mujibu wao lilipelekea chama kutendewa uonevu.

Soma Pia: Pingamizi kesi ya mgawanyo wa mali CHADEMA latupiliwa mbali

Amesema baadhi ya amri za mahakama zilizotolewa awali zilikuwa “zinalenga kuiingiza mahakama katika aibu,” na hivyo kulazimisha Chadema kuomba marejeo ili taratibu za kisheria zipitiwe upya.

ila huyo mwanasheria wa chadema ni mwepesi mno kisheria, kwakweli ni mwanasheria wa mchongo
kamwe hata isaidia chadema kuchomoka katika kesi yoyote ile ya hicho kikundi cha wahaini,

yaana akina mnyika na mropokaji heche wanabwabwaja zaidi yake
 
Jaji mmoja tu, anatoa maamuzi yanayowagusa mamilioni ya watu; tena maamuzi yenyewe yakiwa ni batili waziwazi kabisa!

Hii ndiyo nchi tunayoishi sasa hivi.
 
Nimefuatilia hizo hoja mahakamani leo. Kiukweli safari bado ni ndefu, kama mtu mmoja anaweza kuamua kufungia chama kisifanye siasa, chenye wafuasi na wanachuana pamoja na mashabiku lukuki.
 
ila huyo mwanasheria wa chadema ni mwepesi mno kisheria, kwakweli ni mwanasheria wa mchongo
kamwe hata isaidia chadema kuchomoka katika kesi yoyote ile ya hicho kikundi cha wahaini,

yaana akina mnyika na mropokaji heche wanabwabwaja zaidi yake
Mwanasheria mwepesi wa mamako huko uvccm nonsense k kamlete mwanasheria kutoka Kwa mamako.
 
ila huyo mwanasheria wa chadema ni mwepesi mno kisheria, kwakweli ni mwanasheria wa mchongo
kamwe hata isaidia chadema kuchomoka katika kesi yoyote ile ya hicho kikundi cha wahaini,

yaana akina mnyika na mropokaji heche wanabwabwaja zaidi yake
🫵🌈🤫
 
Back
Top Bottom