GE2025 Dkt. Mwinyi: CCM itaendelea kulinda Amani na Umoja wa Zanzibar

GE2025 Dkt. Mwinyi: CCM itaendelea kulinda Amani na Umoja wa Zanzibar

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
354
Reaction score
395
Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema chama hicho kitaendelea kusimamia na kulinda misingi ya amani, umoja na mshikamano ambayo imeiwezesha Zanzibar kufikia mafanikio makubwa ya maendeleo katika miaka mitano iliyopita.

1760680643879.png
Akizungumza, Alhamisi Oktoba 16, 2025, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Paje, mkoa wa Kusini Unguja, Dkt. Mwinyi amesema sera kuu ya Chama Cha Mapinduzi imejikita katika kudumisha misingi hiyo mikuu ambayo ndiyo msingi wa maendeleo ya taifa.

Ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Zanzibar imepiga hatua kubwa za kimaendeleo kutokana na mazingira tulivu na maridhiano ya kisiasa yaliyopo nchini.

“Mpaka sasa hivi katika miaka mitano iliyopita tumekwenda vizuri, nchi yetu ina amani, ina umoja, mshikamano, na hata tuna maridhiano ya kisiasa. Hii imesababisha mambo mengi ya kimaendeleo kufanyika kwa sababu ya amani tuliyokuwa nayo,” amesema.

Dkt. Mwinyi amewaomba Wazanzibari wote kuendelea kulinda na kudumisha amani iliyopo, akisisitiza kuwa maendeleo hayawezi kupatikana katika mazingira ya mifarakano na ubaguzi.

Mbali na kuzungumzia masuala ya amani na umoja, Dkt. Mwinyi pia ameahidi kuendeleza miradi mikubwa ya maendeleo katika sekta ya miundombinu ya usafiri na usafirishaji, hasa katika Mkoa wa Kusini Unguja, ikiwemo ujenzi wa mradi mkubwa wa barabara ya njia nne kutoka Tunguu hadi Makunduchi akisema mradi huo utaufungua mkoa huo kiuchumi na kiutalii.

Ameongeza kuwa Serikali yake pia itahakikisha ujenzi wa madaraja mawili makubwa katika maeneo ya Kusini Unguja, yatakayorahisisha usafiri na kuongeza fursa za biashara na uwekezaji.
 
Hongera sana Dkt Mwinyi hakika Zanzibar chini ya huyu mwamba inapaa kimaendeleo
 
Back
Top Bottom