GE2025 Dkt. Mwinyi alivyopanda Jukwaani kucheza na Yammi

GE2025 Dkt. Mwinyi alivyopanda Jukwaani kucheza na Yammi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
354
Reaction score
395
Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Hussein Ali Mwinyi, aliibua shamrashamra za aina yake baada ya kuinuka na kucheza jukwaani pamoja na msanii maarufu wa muziki nchini Tanzania, Yammi .

Tukio hilo lilifanyika katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Bumbwini, Mkoa wa Kaskazini Unguja, na liliibua burudani kubwa kwa maelfu ya wananchi waliojitokeza kushiriki.

Mkutano huo ni sehemu ya muendelezo wa kampeni za Dkt. Mwinyi, ambapo mbali na hotuba na ahadi za maendeleo, wananchi walipata nafasi ya kushuhudia ukaribu na furaha kati ya kiongozi wao na wasanii wa kizazi kipya.

Hatua ya Dkt. Mwinyi kucheza na Yammy Yammi ilionekana kama ishara ya mshikamano na umoja kati ya viongozi na vijana, jambo lililoongeza hamasa na shangwe kubwa kwa hadhira.

Aidha, wananchi waliohudhuria walieleza kufurahishwa na namna kampeni hizo zinavyohusisha burudani, siasa na ujumbe wa maendeleo kwa pamoja. Walisema kitendo cha Dkt. Mwinyi kushirikiana na msanii maarufu jukwaani ni kielelezo cha kiongozi anayeijali furaha ya watu wake na kuthamini nafasi ya sanaa katika kuhamasisha jamii.

 
Back
Top Bottom