Gody Mnazarayo
Member
- Feb 7, 2019
- 41
- 45
Dkt Mwigulu Nchemba ni mtu sahihi kwa wakati sahihi.
Nimesoma andiko la mwanajf mmoja humu, amemshutumu sana Dkt Mwigulu Nchemba bila hoja za msingi, kama kawaida ya wabongo bongolala. Hivi unawezaje kutuhumu PhD ya Dkt Mwigulu Lameck Nchemba kwasababu katoa speech ambayo haikipendezi chama unachokiamini?
Hivi unawezaje kumchukia mtu kwasababu tu akisimama jukwaani anaweka hadharani uzandiki wenu mnaofanya dhidi ya watanzania?
Bahati mbaya sana vyama vya upinzani vimezalisha vijana wa hovyo, wasioweza kujadili hoja, wametanguliza mbele hisia za kisiasa kuliko uhalisia wala hoja.
Dkt Mwigulu Lameck Nchemba amesema tuache kujipa kiherehere cha kuorodhesha matatizo ambayo hayapo na wakati mwingine Matatizo hayo tayari yanakuwa yameshachukuliwa hatua na Serikali, unakuta chama fulani kinakazana kujadili tatizo ambalo tayari limetatuliwa, na hii yote ni kutokana na kukosa ajenda za kuibana Serikali mnabaki mnaokoteza vihoja barabarani na kuja kuwalisha upepo wafuasi wenu ambao wamejawa na hisia za ujinga na uzwazwa.
Dkt Mwigulu Lameck Nchemba ni mtu sahihi kwa kipindi hiki kwasababu ni full package yaani Kiraka, ni mchumi wa daraja la juu pale benki ya dunia, ni strategist wa kupambana na mifumo ya bei, ni mwanasiasa nguli ukimletea za kisiasa anaenda na wewe mazimamazima unabaki kulialia.
Tuliataka kumhukumu kwa tozo lakini alikuwa sahihi kabisa Kwasababu Fedha hizo zilikuwa zije kufuta kabisa kadhia ya Ukosefu wa mikopo ya Elimu ya Juu, wote ni mashahidi leo wanafunzi wamekosa mikopo kwasababu tu tozo zimeondolewa baada ya wajuaji kujipa umuhimu wa kuleta makelele ya kijinga bila kuwaza kitatokea nini uko mbeleni.
Na Tozo ni maamuzi ya Serikali nzima unapokuja kumshambulia Dkt Mwigulu Nchemba tunakuona kama mjinga fulani tu, yaani kabisa unahisi Tozo zilitungwa nyumbani kwa Mwigulu na kuletwa directly kwa wananchi? utakuwa una Matatizo ya ubongo wewe.
kuhusu PhD ya Dkt Mwigulu Lameck Nchemba, ebu nenda wewe pale chamber UDSM ukapewe hiyo PhD tuone kama ni rahisi hivyo. Kwa wasiofahamu tu Dkt Mwigulu Lameck Nchemba alikuwa ni mwanzafunzi bora kati ya wanafunzi watatu waliohitimu mwaka wake wa shahada ya kwanza, ndipo BOT ikamuchukua akiwa anagombaniwa na taasisi kubwa ulimwenguni. Ni baraka kuwa na msomi kama Mwigulu hapa nchini, wengi wamekimbia hii nchi kwa sababu ya maneno maneno haya yasiyokuwa na kichwa wala miguu.
Wote ni mashahidi Dunia inapita kwenye anguko la uchumi, lakini Tanzania imebaki kuwa stable kwasababu ya Njia na Mipango ya Mwigulu, tunaigiza kama hatuoni jitihada zake kwasababu tu ni mbaya wetu wa kisiasa, tunaleta ushamba kwenye mambo muhimu. World Bank yenyewe imekiri tanzania imefanikiwa kubaki katika Hali nzuri pamoja na majanga ya vita na COVID. Hao wazungu wanaokaa na kina Lissu mavikao Kila siku ndio wamewaagiza mawaziri wa mataifa mbalimbali kwenda Kwa Dkt Mwigulu kujifunza namna alivyodhibiti mfumuko wa Bei na ku- stabilize uchumi wa Tanzania.
Dkt Mwigulu Lameck Nchemba Kapokea Wizara nyeti Kipindi ambacho Dunia imetususa, Dunia imetuweka katika Dustbin, Tumpongeze Mwigulu na sio kumuundia Propaganda za kijingajinga.
Mimi niendelee kuwasihi viongozi wa upinzani waliokomaa kuwafunda vijana wao namna ya kujenga hoja zao bila kuingiza hisia za kitoto.