Dkt Mwigulu Mchumi First Class

Mudawote

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2013
Posts
11,570
Reaction score
16,017
GTs,

Napenda kuzungumza na Dkt Mwigulu kupitia jukwaa hili. Sitaki kumuita Waziri Mkuu kwa sababu mpaka sasa uhalali wa serikali ya Dkt Samia kikatiba haupo na yeye anajua kabisa alichokifanya kufanya figisu kubalagaza upinzani hiyo ni ticket ya kuondolewa madarakani kwa njia yeyote na ndicho kinachokuja, hivyo Dkt Mwigulu kwangu siyo Waziri Mkuu na Dkt Samia bado siyo Rais bali ni mg’ang’anizi kwenye ofisi ya rais.

Nije kwenye jambo letu. Dkt Mwigulu wewe ni mwema sana na umetusaidia watu wengi sana including mimi mwenyewe ni mfaidika wa ukarimu wako.

Unachokifanya sasa kinakuua kisiasa kwa sababu kauli zako zote ni za kishenzi na hazi aksi matakwa ya watanzania.

Yaani watu wameuawa kwa maelfu wewe unaenda kuzungumzia polisi waliouawa na wenzao, hivi na raia gani alikuwa na silaha? Ya kuua polisi??

Yaani badala ya kujitengenezea political future ya baadaye wewe unajiangamiza na Dkt Samia ambaye alishanyang’anywa kibali cha urais na Mungu toka kipindi kile.

Dkt Mwigulu mpaka sasa unachukiwa sana, ukitaka kujua soma comments za JF na Facebook na mitandao mingine. Usidhani ni wachache wanaokuchukia, unachukiwa sana tena sana.

Sijui utajikwamuaje
 
Hao wote ni wajinga, CCM ya sasa ingekua na watu wenye akili wangeweza kuitawala tanzania kirahisi sana na wakaendelea kujichotea kirahisi kabisa,
Na hii ni kwa sababu watanzania bado wengi wajinga kutokana na elimu duni wanayoitoa
Ila wameamua kutumia nguvu badala ya akili matokeo yake hata wao wanaishi kwa hofu na ikipigwa lockdown wote tunaathirika
 
Kukaa kimya sio Ujinga vijana Wakitanzania sio wajinga mazee..
 
Badilisha headline isomeke MCHUMIATUMBO FIRST CLASS.
 
Msomi daktari asiyeamini kwenye utafiti na takwimu sijui philosophy yake ni ya nini? Ushirikina?
 
😂😂😂😂 huu ni mkakati kamwaga mihela aongelewe kila kona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…