Dkt. Mpango: Rais amepanga safu ya ushindi wa uchaguzi wa mwaka 2024 & 2025. Tukafunge magoli ya uhakika sio kubahatisha

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,065
49,751
Hayo ndio maneno ya VP Mpango wakati akitoa neno la salamu kwenye uapisho.

Awali Rais Samia alisema mabadiliko aliyoyafanya sio adhabu Bali kuongeza Ufanisi kwani ni mabadiliko ya kawaida.

----
Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameona ni vema apange safu ya ushindi ambayo inaweza kufunga magoli zaidi ili kuanzia mwakani Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na mwaka 2025 Uchaguzi Mkuu yakafungwe magoli ya uhakika sio ya kubabaisha.

Akiongea mbele ya Rais Samia wakati wa kuwaapisha Viongozi Wateule Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar leo Sept 01,2023, Dkt. Mpango amesema “Nawapongeza Wateule wote katika nafasi mbalimbali, kama ambavyo Kocha yoyote anafanya Mh. Rais imempendeza amewaamini amebadilisha namba zenu za kucheza mpira, maana Mawaziri karibu wote sura zilezile lakini tumebadilisha nafasi na tukiacha mmoja na Manaibu Mawaziri tukiacha wachache”

“Nawaomba sana, Mh. Rais anataka tija zaidi katika utendaji kwahiyo muende mkashirikiane, mzingatie falsafa ya Mh.Rais ya zile R nne, nami natilia mkazo ile ya kusimamia mabadiliko (Reforms)”

“Mmemsikia Makamu Mwenyekiti (Mzee Kinana), ni muhimu sana muwe na masikio juu ya kero za Wananchi wetu Bara na Visiwani na kuzifanyia kazi, yapo maeneo kelele ni kubwa kila unapokwenda, nikimuangalia Jerry Silaa kwenye ardhi kero kubwa ukaongoze timu yako kuhakikisha kero upande wa ardhi zinashughulikiwa ipasavyo, pia upande wa Maliasili magomvi kati ya Wananchi na Hifadhi zetu ni makubwa Waziri ukashirikiane na mwenzako wa mifugo tunapoteza Watu n.k”

“Mheshimiwa Rais ameona ni vema apange safu ambayo inaweza kufunga magoli zaidi ili twende kuanzia mwakani Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na mwaka 2025 Uchaguzi Mkuu twende tukafunge magoli ya uhakika sio ya kubabaisha”

Chanzo: Millard Ayo
 
Usijitoe ufahamu, miaka 7 nyuma hapa kuna maeneo mtu usingekatiza na jezi la ccm. Ndiko mmerudi, jipangeni vinginevyo mwakani mtaambulia aibu.
Mbona saizi kesi zinavaliwa na watu wanakatiza? Ndio mnavyojidanganya?
 
Lengo kama ni kulenga chaguzi tu wananchi hawatendewi haki

Mabadiliko yalenge kubadilisha maisha ya wananchi walio wengi na utendaji uliotukuka maofisini na kwa wateuliwa

Nchi haiwezi endeshwa kwa kila wakati kiongozi anaota uchaguzi unafuata baada ya kuchaguliwa sio sahihi kabisa

Uchaguzi ukipita ni hapa kazi tu kama Magufuli alivyosema siasa za uchaguzi zinatakiwa kusubiri uchaguzi ukifika ndipo ziundwe hizo team za ushindi

Sikubaliani na makamu wa Raisi alichosema

Haiwezekani kila saa watendaji serikalini awe raisi,makanu waziri nk wanawaza chaguzi tu

Wafanye kazi waache porojo wa deliver mategemeo ya wananchi

Huo ujinga wa kuwaza chaguzi tu waache
 
Back
Top Bottom