Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango amelitaka jeshi la polisi nchini kuimarisha hali ya ulinzi na usalama katika uchaguzi mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Dkt.Mpango ametoa kauli hiyo leo Agosti 11, 2025 mjini Moshi mkoani Kilimanjaro wakati akifungua mkutano wa maafisa waandamizi wa jeshi la polisi nchini uliofanyika katika ukumbi wa shule ya polisi Moshi. Amesema uchaguzi huo unahusisha wadau wengine wakiwemo wananchi wenye itikadi mbalimbali za kisiasa, wagombea wa nafasi mbalimbali,Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi pamoja na viongozi wa dini na viongozi wa mila.
Aidha, Makamu wa Rais amesema ili kufanikisha mambo hayo, mikutano ya kampeni itafanyika kwenye maeneo yaliyoruhusiwa na ndani ya muda uliopangwa na kuzuia maadamano yasiyo na kibali ambayo yanaweza kusababisha vurugu.