Dkt. Leonard Chamuriho atajwa na Rais kuwa ni mtaalam wa kufanya mazungumzo - "Negotiation Expert". Je, hawa watu tunao wangapi?

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,399
Raisi John Magufuli alitoa hotuba ya kuzungumzia utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mradi wa bwawa la kufua umeme wa Stiegler Gorge kwenye mto Rufiji.

Kwenye hafla hiyo Misri wamekuja na wajumbe zaidi ya 100 wakiongozwa na waziri mkuu wao pamoja na wawakilishi wa kampuni ya Arab Contractors ambao ndo watakaojenga bwawa la Stigler Gorge.

Kwa mujibu wa raisi John Magufuli mwenyewe, mazungumzo kati ya pande mbili za Tanzania na Misri yalikuwa ni mazito na yalochukua muda kuyamalza hadi kufikia makubaliano.

Kwenye mazungumzo hayo Tanzania ilikuwa ikiwakilishwa na ujumbe wa watu wasozidi 15 ambao ni raisi mwenyewe aliwachagua kwa kushirikiana na waziri wa ujenzi.

Mwenyekiti wa timu ya Tanzania ni Dr Leonard Chamuriho ambae ni katibu mkuu wa wizara ya mawasiliano na uchukuzi.

Ndani ya timu ya Tanzania kuna wajumbe kutoka TANROAD, Tanesco, Ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, Hazina, TRA. wizara ya nishati, Ofisi ya raisi (bwana H. Ubwa) na ofisi ya Mazingira.

Hawa ni wataalam wa ujenzi, wataalam wa nishati ya umeme, sheria, usalama, fedha na mazngira.

Lakini mwenyekiti wa timu hii bwana Leonard Chamuriho nde mtaalam wa kufanya mazungumzo yaani Negotiation Expert.

Jambo jingine lilillojenga udadisi ni kusikia kwamba Dr Chamuriho ndie alieshiriki kufanikisha ununuzi na uletwaji wa ndege mpya za ATCL nchini Tanzania.

Pia Dr Chamuriho ameshiriki kwenye mazungumzo ya kujenga reli ya umeme ya Standard Gauge Railways kama mtaalam wa kufanya mazungumzo yaani Negotiation Expert.

NI jambo la kujivunia kuona kwamba nchi yetu inao wataalam ambao wanaweza kufanikisha mambo mengi ya kuleta tija kwa taifa letu.

Ni vizuri nchi yetu inawatunza watu wa aina hii na kuwawezesha kuachia ujuzi wao kwa vizazi vijavyo ili kuiwezesha nchi yetu kufikia kwenye nchi khasa ya asali na maziwa.

Nini maana ya "Negotiation" yaani mazumgumzo baina ya pande mbili?

Hii ni njia ya kufanya nazungumzo maalum ambayo yanalenga kufikia makubaliano ili kuondoa tofauti.

Ni utaratibu ambapo makubaliano au muafaka unafikiwa huku migongano na kutoafikiana vikiondolewa na kisha kusaini makubaliano hayo kisheria mbele ya mashahidi.

Kama hakutakuwa na kukubaliana basi wahusika wa mazungumzo hayo huendelea kufanya vikao kwa malengo ya kufikia muafaka ambao unanufaisha pande zote mbili.

Cha msingi katika kufanya mazungumzo hayo ni kuwepo kwa usawa yaani fairness, kila mmoja kunufaika, na kuendeleza ushirikiano.

Hivyo Tanzania na Misri zitaendeleza ushirikiano baina yao na kuhakikisha ujenzi wa bwawa la Stigler Gorge linamalizwa kwa kuda ulokusudiwa.

Utaratibu wa kufanya mazungumzo yaani Process of negotiation.

1. Maandalizi
2. Majadiliano
3. Kutanabaisha malengo ya majadiliano.
4. Kuafikiana kuelekea kila mtu kushinda kwa upande wake yaani "win-win outcome"
5. Makubaliano yaani agreement
6. Utekelezaji wa hatua za makubaliano.

Kuna wakati majadiliano huwa ni aina mbili yaani formal na informal kwamba pande mbili zinaweza kuamu kuzungumzia mambo yanayojadiliwa nje ya vikao au ndani ya vikao au ikawa ni siri kabisa.

Ila inapotokea kunakuwa na kutokukubaliana (suala la Acacia) basi hatua hizo hapo juu katika utaratibu mzima wa mazungumzo zinaachwa pembeni na kunabakia kwenye namba 2 yaani majadiliano ambayi huwezi kuchukua muda mrefu.

Dr Leonard Chamuriho anao ujuzi wa kufanya mazungumzo yaani kwa kiingereza twasema "he has negotiation skills" ambazo ni adimu sana.

Kitendo cha raisi John Magufuli kumtaja bwana Leonard Chamuriho kwamba aliihusika na mazungumzo iya ununuzi wa ndege na pia ujenzi wa reli ya Standard gauge na sasa kuhusika na mazungumzoi ya ujenzi wa hili bwawa na Stigler Gauge, hilo ni jambo jema kwamba nchi yetu inao wataalam.

Ningependa kufahamu je wataalam kama hawa ambao mara nyingi ni wachache kuwa nao hupatikana wapi?

Je, Tanzania inao wataalam wa kutosha wa kufanya mazungumzo kuhusu miradi mikubwa ya serikali?

Je miaka yote hiyo wataalam hawa walikuwa wapi?

Na kama Dr Chamuriho ni katibu mkuu wa wizara kwanini asiwe na ofisi maalum na akawa ana wigo mpana zaidi ambao utamwezesha kuajiri vijana ambao wana utaalam wa kufanya mazungumzo?
 
Hatujaona makibaliano yao tunasikia tuu watu weshaingia kazini, hizi kazi wanazofanya ni mali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania wananchi tunahaki yakujua makubaliano yaliyofikiwa au wewe una copy ya mikataba waliyoingia.

NI wapi hapa duniani umeona wafanya hivyo yaani mwananchi wa kawaida apewa nakala ya mikataba baina ya serikali za nchi mbili?
 
Watu mnaonufaika moja kwa moja na utawala huu mnatupa tabu sana.

Mkuu . mimi ni mjasiriamali tu wa kawaida.

Ila nna interest sana na masuala mbalimbali ya kimaendeleo.

Mimi nipo kwenye michezo, diplomasia, siasa na mengi tu.
 
Kwa hiyo tuna mtaalamu mmoja tu, miradi yote anapitisha yeye. Ana uhusiano gani na rais. Stiegler ingeoaswa kuwa chini ya wizara ya Nishati ambayo ina katibu wake.
 
Back
Top Bottom