Dkt. John Magufuli amuapisha Balozi Eng. John Kijazi

Cicadulina

JF-Expert Member
Sep 8, 2015
974
2,366
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Balozi Eng. John William Herbert Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu jijini Dar es Salaam. Balozi Kijazi anachukua nafasi ya Balozi Ombeni Sefue ambaye atapangiwa kazi nyingine.
=====

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Balozi Mhandisi John William Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.

Hafla ya kuapishwa Balozi Kijazi imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa, Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Makatibu wakuu na Naibu Katibu Wakuu.

Balozi Kijaziambaye kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini ndia, anachukua nafasiya Balozi Ombeni Sefue ambaye atapangiwa kazi nyingine.

W akati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameagana na Mwakilishi wa Shirika Ia Umoja wa Mataifa Ia kuhudumia wakimbizi hapa nchini (UNHCR) anayemaliza muda wake Bi. Joyce Mends-Cole Ikulu Jijini Dar es salaam, ambapo pamoja na mambo mengine amemshukuru kwa kazi kubwa ya kuhudumia wakimbizi kwa kipindi chote alichokuwepo hapa nchini.

Kwa upande wake Bi. Joyce Mends-Co le amempongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri inayofanywa na Tanzania kuzisaidia nchi zenye matatizo, hususani migogoro ya kisiasa ambayo husababisha watu wake kuwa wakimbizi.

Pia amepongeza kuteuliwa kwa Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, kusaidia usuluhishi wa mgogoro wa Burundi ambao umesababisha idadi kubwa ya wakimbizi kukimbilia Tanzania.

Hata hivyo amesema idadi ya wa kimbizi wanao kimbilia Tanzania imepungua kutoka wakimbizi 3,000 waliokuwa wakiingia hapa nchini kwa wiki, wakati Mgogoro wa Burundi ulipoanza hadi kufikia wakimbizi takriban i 1,000 wanaingia hapa nchini kwa wiki hivi sasa.

Aidha, Bi. Joyce Mends-Cole amewas hukuru watanzania kwa ushirikiano alioupata kwa kipindi cha miaka mitatu aliyofanya kazi hapa nchini, na ameahid i kuwa Balozi wa kuitangaza vyema Tanzania.

GersonMsigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU Dar es salaam

07 Machi, 2016



1.jpg

3.jpg

4.jpg

5.jpg

6.jpg
 
O.S? Anabaki kuwa shujaa, Yaani na yeye alikuwepo kwenye hafla hiyo duuh jamaa ana roho ngumu sana, Na huyu barozi kaja na ndege ya saa ngapi kutoka India?
 
Naona OS anamalizia kazi Yake ya mwisho ongera sana umuhimu wako utaonekana katika taifa ulimwonyesha njia mkulu
 
Pombe katika ubora wake. Guys mimi naona haya ni mabadiliko ya kawaida. Lets not spin this thing! Kasema Sefue atapangiwa kazi nyingine. Inatosha!
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Eng. John William Herbert Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu jijini Dar es Salaam. Balozi Kijazi anachukua nafasi ya Balozi Ombeni Sefue ambaye atapangiwa kazi nyingine.
1.jpg




2.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Herbert Kijazi wa kwanza kushoto na Wa mwisho kulia ni aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.
 
Mabadiliko ni hatua muhimu katika maendeleo ya taasisi mtu au hata taifa pia, kazi ya Ombeni imeonekana na huyu pia anakuja na yakwake tunatumaini itaonekana yote ya yote ilani ya CCM inaendelea kutekelezwa na serikali ya kazi ya wamu ya 5, tuendelee na kazi.
 
ikitokea mabadiliko kama kazi bado unaipenda sijui utajisikiaje mwenzio akiapishwa kuja kuchukua nafasi yako.

kiukweli hizi nafasi za kuteuliwa pasua kichwa maana huna uhakika kesho utakuwa wapi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom