PreGE2025 Dkt. Doto Biteko: Wananchi msikubali kugawanyika Uchaguzi ujao

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,303
Reaction score
18,460
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewataka wananchi wa Tabora kutogawanyika kwa sababu yoyote ile kisa uchaguzi mkuu mwa mwaka 2025 huku akiwahimiza kumuunga mkono Rais Samia kutokana na juhudi zake za kuwaletea wananchi maendeleo.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Dkt. Biteko amesema hayo Mei 3, 2025 mkoani Tabora mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Kiwanda cha Kutengeneza Nguzo za Zege cha TCPM.

"Katika uchaguzi Mkuu ujao tusikubali kugawanywa wala kudanganywa kwa misingi yoyote ile, tukitanguliza tofauti zetu, matokeo yake yataishi kwa kipindi kifupi na madhara yake yatakuwa ya muda mrefu", amesema Dkt. Biteko.

Hawa wote ni wanafiki. Wanaongelea tu matokeo hawaongelei chanzo, ambacho ni udhulumaji wa haki.

Kama ana dhamira njema akionya ushetani unaoendelea ambao ndio utakaowagawa watanzania. Lakini kwa sababu hawa watu wamejaa unafiki, na tamaa ya kushibisha matumbo yao, hutasikia wakiongelea jinsi wananchi wanavyodhulumiwa haki zao na watawala.

Hata siku moja haitakuja kutokea, wanaouawa wakawa kitu kimoja na wauaji. Wanaotekwa hawawezi kuwa wamoja na watekaji.

Biteko aache unafiki, aache kuwa sehemu ya ushetani, apinge ushetani, wananchi tutamwelewa
 
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewataka wananchi wa Tabora kutogawanyika kwa sababu yoyote ile kisa uchaguzi mkuu mwa mwaka 2025 huku akiwahimiza kumuunga mkono Rais Samia kutokana na juhudi zake za kuwaletea wananchi maendeleo.

Dkt. Biteko amesema hayo Mei 3, 2025 mkoani Tabora mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Kiwanda cha Kutengeneza Nguzo za Zege cha TCPM.

"Katika uchaguzi Mkuu ujao tusikubali kugawanywa wala kudanganywa kwa misingi yoyote ile, tukitanguliza tofauti zetu, matokeo yake yataishi kwa kipindi kifupi na madhara yake yatakuwa ya muda mrefu", amesema Dkt. Biteko.
View attachment 3325013

Hawa MaCCM hawanaga akili. Hili tatizo halitakwisha kwa maneno maneno. Bila action na nia ya kweli wanajidanganya tu na kuahirisha matatizo.

Na pia kwa kuahirisha matatizo ndiyo watakuwa wanayafanya kuwa makubwa zaidi.
 
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewataka wananchi wa Tabora kutogawanyika kwa sababu yoyote ile kisa uchaguzi mkuu mwa mwaka 2025 huku akiwahimiza kumuunga mkono Rais Samia kutokana na juhudi zake za kuwaletea wananchi maendeleo.

Dkt. Biteko amesema hayo Mei 3, 2025 mkoani Tabora mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Kiwanda cha Kutengeneza Nguzo za Zege cha TCPM.

"Katika uchaguzi Mkuu ujao tusikubali kugawanywa wala kudanganywa kwa misingi yoyote ile, tukitanguliza tofauti zetu, matokeo yake yataishi kwa kipindi kifupi na madhara yake yatakuwa ya muda mrefu", amesema Dkt. Biteko.
View attachment 3325013
Sawa kabisa, sasa mbona mnaogopa kufanya uchaguzi uwe wa haki?
 
kumuunga mkono sa100 ni kuunga mkono
  • utekaji na kuuliwa kwa watu
  • kunyimwa uchaguzi huru na wa haki
 
Mbona tushakubaliana........No reform, No election
 
Misiba mingi inatokea kipindi cha uchaguzi, tunazika, tunapata mahabusu na wengine kubaki na ulemavu wa maisha. Tunahitaji mabadiliko katika mfumo wa uchaguzi.
 
Amepewa nafasi kimkakati
ili kuvuna kura za kanda ya ziwa
this time watz wamekuwa waelevu sana
hawashawishiki kihivyo!
Nae atulie sasa.
unaona Majaliwa ni kama shati tu lipo Ofisini
utadhani hayupo duniani.

CCM haitaki kujiharibia kanda ya ziwa ndiyo maana hadi Leo Mpina hagusiki
angekuwa anatokea hata Kisalawe tu
kwa hizo kauli na maswali yake
hadi sasa hana uanachama,
 
Back
Top Bottom