barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Leo magazeti mawili ya "IMAAN" na "AL-HUDA" yamekuja na vichwa vya habari vinavyomuhusu aliyekuwa DG wa NSSF Dkt.Ramadhan Dau kuwa anaonewa na kufitinshwa kwa kuondolewa kwenye sherika hilo la hifadhi ya Jamii wakati alikuwa amebakia miaka michache tu astaafu.
Gazeti hilo linasema licha ya uteuzi wa Dr Dau kuelezwa kuwa una tija kwa Taifa na kuimarisha uhusiano wa Tz na nchi za nje,lkn umedunisha uwakilishi wa Waislamu katika utendaji wa serikali hapa nchini.
"Tumezidi kuisha serikalini,wengine wanapelekwa nje ya nchi.Sisi ni wengi katika wale wanaoitwa majipu,lkn katika wanaoteuliwa kama si wachache basi hatumo kabisa,ukichunguza ni kama huu utumbuaji majipu unatulenga sisi" ..limeandika Gazeti la Al-Huds likimnukuu Bwana Haji mfanyakazi wa serikali.
"Dr Dau angemalizia tu kipindi chake,ameitoa mbali toka NPF iliyokuwa taabani mpaka NSSF yenye miradi lukuki,ilikuwa apewe shirika au taasisi nyingine ya kuongoza hapa nchini ili awajibike kama alivyowajibika NSSF".Gazeti hilo limedai kama kumtumia kidiplomasia basi angetumiwa baada ya kustaafu lkn sio kumuondoa sasa,nafasi ambayo itakuwa ngumu kwa mtu mwingine kuziba pengo la Dr Dau,gazeti linaendelea kusema kuwa teuzi hiyo ni chuki dhidi ya imani fulani na kuwepo na hali ya kuimarisha mfumo ili imani fulani iendelee kuwa katika sehemu ya maamuzi.
"Aliikuta NPF iliyotegemewa makato yasiyodaiwa ya "cane carters" ambao walikuwa wafanyakazi wa muda wa viwanda vya sukari vikiwemo vikampuni na taasisi za watu binafsi,chini ya Dr Dau shirika lilifanikiwa kuwa na miradi mikubwa kama daraja la kisasa la Kigamboni,mradi wa makazi katika eneo la Dege Beach huko Kigamboni,mradi wa nyumba za Kiluvya,mradi wa nyumba za makazi za Mtoni Kijichi,Mradi wa kituo cha Michezo kwa Ushirikiano na Club ya Real Madrid na pia NSSF ilishiriki ktk ujenzi wa Chuo Kikuu Dodoma.Kutokana na ufanisi huu Rais Mkapa aliwahi mtunuku cheti cha usimamizi na utendaji bora ktk kipindi cha uongozi wake wa shirika hilo