SautiYaMnyonge
JF-Expert Member
- May 13, 2018
- 439
- 742
Wanajukwaa salaam,
Kwa muda sasa wa wiki mbili nipo jimbo la Vunjo ambapo nilikuja kuona uzalishaji wa zao la vanila ukanda wa Kirua,Kilema,Marangu,Mamba na Mwika. Hali ya hewa ni baridi sana ukizingatia nimezoea maisha ya jiji la kibiashara au jiji la Kune Boy (Abubakar Kunenge RC Dar)
Katika pitapita zangu stori zinazobamba kila kona ni uchaguzi mkuu hususani nafasi ya ubunge katika jimbo hili ambapo mbunge aliyekuwepo Ndg James Mbatia naye amejitosa kwa mara nyingine kutetea nafasi yake japo hali ya kisiasa sio nzuri hata kidogo.
Yupo mgombea wa chadema Ndugu Grace Kiwelu huyu hapewi nafasi kwani amekuwa mbunge wa viti maalum miaka kumi hajawahi kuwa msaada kwa wana vunjo, wasemavyo wananchi walio wengi.
Habari ya mjini sasa ipo kwa Dkt Charles Stephen Kimei (CSK kama wanavyomuita) ambaye wanasema wakati alipokuwa mkurugenzi mtendaji wa CRDB alisaidia mambo mengi ikiwemo kuanzishwa kwa tawi la benki hiyo jimboni humo, kujenga kituo cha polisi Marangu mtoni, kununua magari mawili mapya aina ya landcruiser kwa ajili ya vituo vya polisi vya Himo na Marangu Mtoni, ukarabati wa Tumaini Saccos iliyopo Mamba Kusini, kuchangia ujenzi wa madarasa Mboni Sekondari,Kuchangia ujenzi wa mabweni ya wasichana Muungano Sekondari, amechangia vigae vya sakafuni (tiles) kukamilisha jengo la ofisi Vicoba Vunjo yenye wanachama 7,000 ambapo walimteua kuwa mkurugenzi wao kwa sasa.
Kwa hayo machache wanasema ni mtu ambaye alionesha mapenzi makubwa kwa wanavunjo muda mrefu sasa ni vizuri wakamtuma kuwa mbunge wao ili akafanye kazi hii kwa uzuri zaidi. Wengine wanasema jimbo hili lina fursa nyingi za kiuchumi ila hazijaibuliwa hivyo Kimei anamudu kuzifungua kwani kama aliweza kuitoa benki ya CRDB kutoka benki iliyokuwa inafilisika mpaka kuwa benki kubwa, mashuhuri, inayotengeneza faida kuliko benki zote nchini na kushinda tuzo mbalimbali za kimataifa za benki bora Afrika!
Hakuna shaka yoyote kuwa Moshi mweupe utaonekana kwa bingwa huyu wa uchumi na masuala ya kifedha, Namtakia kila la heri!
Tukumbuke uchaguzi unapita,nchi inabaki tuitunze amani yetu.
Pichani akiwa na vijana jimboni humo.
NB: Suala la urais huku sio agenda maana wanasema Rais yupo ambaye ni Magufuli anayekataa huyo ni mbishi tu wa asili