GE2025 Dkt. Charles Kimei atambulisha agenda kabambe za maendeleo Vunjo

GE2025 Dkt. Charles Kimei atambulisha agenda kabambe za maendeleo Vunjo

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

MTANZANIA620

Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
81
Reaction score
95
Katika mwendelezo wa harakati zake za kuwaletea maendeleo wananchi wa Vunjo, Mheshimiwa Dkt. Charles Stephen Kimei akiwa katika kata za Marangu Magharibi, Marangu Mashariki na Mamba Kusini ikiwa ni siku ya kwanza ya ratiba ya wagombea ubunge ndani ya CCM katika Jimbo hilo ametambulisha ajenda tatu kabambe zitakazotoa mchango mkubwa katika kuinua uchumi wa wananchi, kuboresha huduma za kijamii, na kuimarisha ushirikiano kati ya serikali, halmashauri na wananchi. Ajenda hizo zilizopewa msisitizo kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM 2025 - 2030.

1. Biashara ya Hewa ya Ukaa (Carbon Credit) Kupitia Misitu ya Vunjo

Dkt. Kimei amedhamiria kushirikiana na halmashauri ya wilaya ya Moshi pamoja na Serikali Kuu katika kuwezesha matumizi ya misitu ya Vunjo kutumika katika biashara ya hewa ya ukaa baada ya Serikali inayoongozwa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuandaa sera, sheria na kanuni zinazotoa muongozo wa biashara hiyo hapa nchini ili tuweze kuchangamkia fursa hiyo. Katika kufanikisha hilo zipo hatua za kufuata, hususani:-

Kuomba kibali cha matumizi ya Msitu wa Nusu Maili, uliopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro, kwa ajili ya biashara ya hewa ya ukaa.

Mpango huu utahusisha vijiji vinavyopakana na misitu na kuviwezesha kuvuna faida ya kimasoko kimataifa kupitia mikataba ya kaboni.

Mapato yatakayopatikana yataisaidia halmashauri, vijiji husika, na kuongeza mitaji ya uwezeshaji kwa wananchi kiuchumi.

2. Uhamasishaji wa Usajili wa Bima ya Afya kwa Wote

Akitambua changamoto ya upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wasio na uwezo, Dkt. Kimei ameeleza kuwa:-

Serikali ipo katika hatua za maandalizi ya kutunisha Mfuko wa Bima ya Afya kwa Wote, baada ya Bunge kupitisha sheria hiyo.

Katika kipindi kijacho, kampeni ya kutoa elimu na kuhamasisha usajili wa wananchi itaanzishwa, kwa lengo la kuhakikisha kila mwananchi anapata uhakika wa matibabu, wakiwemo wazee na watu wasiojiweza katika Jimbo la Vunjo.

3. Ushirikiano wa Sekta ya Malazi na Makampuni ya Utalii kwa Ajira na Uchumi

Kwa kutambua fursa ya kitalii iliyopo katika Jimbo la Vunjo, Dkt. Kimei amepanga:-

Kuanzisha mtandao wa ushirikiano kati ya wamiliki wa hotel, lodge, nyumba za malazi na tour operators.

Mpango huu utaleta uhakika wa biashara kwa waendesha huduma za malazi na usafiri, kuchochea ajira kwa vijana, na kuongeza kipato cha kaya na maeneo yanayozunguka vivutio vya kitalii.

Kwa ujumla, ajenda hizi tatu ni sehemu ya mkakati mpana wa Dkt. Kimei wa kuhakikisha maendeleo jumuishi, kwa kutumia rasilimali zilizopo Vunjo, kuimarisha huduma za kijamii, na kuchochea uchumi wa wananchi wa kawaida kupitia ubunifu na ushirikiano wa kimkakati.

IMG-20250730-WA0027.jpg
 
Back
Top Bottom