Dkt. Bashiru: Wana CCM hatuna muda wa malumbano

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
DKT. BASHIRU: WANA CCM HATUNA MUDA WA MALUMBANO.

8 Novemba, 2019

Leo Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally akiwa katika ziara ya siku moja Mkoa wa Morogoro wilayani Kilombero amewataka wanaCCM kuacha malumbano katika kipindi hiki cha uchaguzi na badala yake wajikite katika kusimamia na kutangaza utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015 - 2020.

Dkt. Bashiru ameyasema hayo katika mkutano wa ndani uliojumuisha wanachama wa CCM na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wakiongozwa na mwenyekiti wa mkoa ndg. Innocenti Karogoresi na Mbunge wa viti maalum Bi. Getrude Rwakatare.

Pamoja na mambo mengine, Katibu Mkuu ametumia fursa hiyo kupiga marufuku mashindano yoyote ya michezo yanayoandaliwa kwa kuyaita majina ya wanasiasa ama wanachama makada ambapo ameelekeza mashindano yoyote ya michezo yaitwe majina ya viongozi wastaafu na waasisi wa Chama chetu.

"Nimepiga marufuku kuanzia leo mashindano ya michezo nchi nzima kwenye chama chetu kuitwa majina ya wanasiasa, bali yatumike majina ya waasisi wetu, na kwa kuanza, Leo Rwakatare Cup itaitwa Kawawa Cup." Dkt. Bashiru amesisitiza.

Kabla ya mkutano huo, Dkt. Bashiru amesimikwa kuwa chifu wa kabila la wabena na pia amegawa viti vya kutembelea 30 kwa watu wenye ulemavu mbalimbali.

Katika mkutano huo, Bi. Rwakatare amemuhakikshia Katibu Mkuu, upepo wa "kisulisuli" umeumaliza upinzani katika wilaya ya Kilombero, hivyo kazi iliyobaki ni kufanya kazi kwa bidii na kuendelea kujenga taifa la haki na usawa.

Imetolewa na;
Katibu wa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

IMG-20191108-WA0016.jpeg
 
Back
Top Bottom