Dkt Bashiru: Waliotaka kutuchonganisha wameshindwa na kulegea

Kinuju

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
2,390
5,310
Katibu mkuu msitaafu wa CCM na mbunge wa kuteuliwa Dk Bashiru Kakurwa wakati akichangia hoja kwenye mjadala wa wizara ya kilimo amesema nchi yetu imepitia kipindi kigumu baada ya kuondokewa na aliyekuwa rais wa tano wa nchi yetu hayati Dk Magufuli.

Dk Bashiru amesema kutokana na hali hiyo kuna kundi la watu walijipanga kuwachonganisha watanzania kwa kutunga uongo na kusambaza mtandaoni lakini watu hao wameshindwa na kulegea.

=======

Mbunge wa kuteuliwa, Dk Bashiru Ally amesema majaribio yaliyolenga kuwagombanisha Watanzania yameshindwa na kulegea.

Dodoma. Mbunge wa kuteuliwa, Dk Bashiru Ally amesema majaribio yaliyolenga kuwagombanisha Watanzania yameshindwa na kulegea.

“Nchi yetu imepita katika kipindi kigumu cha kihistoria ambacho hatujawahi kuipitia kutokana na msiba mkubwa uliotukumba, kulikuwepo majaribio ya kutuchonganisha na wakati mwingine kudhalilisha watu na kutunga maneno ya uongo ili nchi itikisike, lakini wameshindwa na wamelegea,” amesema katibu mkuu huyo wa zamani wa CCM.

Dk Bashiru ameeleza hayo bungeni mjini Dodoma leo Jumanne Mei 25, 2021 katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Kilimo ikiwa ni mara yake ya kwanza kuzungumza bungeni tangu alipoteuliwa na Rais Samia Suhulu Hassan Machi 31, 2021.

Bila ya kutaja ni maeneo gani na watu gani waliokuwa wakiwagombanisha Watanzania na kuwazushia uongo, amemshukuru Mungu kwa kuwa Rais Samia na makamu wake, Dk Philip Mpango wameonyesha dira na matumaini ya Tanzania kwa siku za usoni.

Dk Bashiru aliteuliwa kuwa mbunge akiwa amedumu kwa wiki tano katika wadhifa wa katibu mkuu kiongozi baada ya kuteuliwa na Hayati John Magufuli Februari 26, 2021.

Nyoka ya uteuzi kwa Dk Bashiru ilianzia Mei 2018 alipoteuliwa kuwa katibu mkuu wa CCM baada ya kufanya vizuri katika kamati ya kuchunguza mali za chama hicho tawala nchini Tanzania.

Leo katika mchango wake Spika Job Ndugai alimuweka kuwa mchangiaji wa mwisho na kumpa dakika 10 wakati wabunge wengine walikuwa wakipewa dakika tano.

“Mimi ni mteuliwa kati ya nafasi za rais na hadi sasa tupo wanane, nataka nimuahidi rais kuwa sitamuangusha katika nafasi hii aliyoniamini,” amesema huku akiendelea kuchangia kuhusu masuala ya kilimo.

Chanzo: Mwananchi
View attachment 1798472
 
Cdm na bashiri WAP na WAP??yeye aseme tu alipita kipindi kigumu baada ya kutolewa katibu mkuu kiongozi hadi mbunge wa kuteuliwa akaulize maswali ya nyongeza kama halima mdee
Ameonyesha yuko imara sana
 
CDM ni wimbo fulani hivi kama wa taifa hivi. Kuna watu wasipokitaja siku haiendi. CDM si imekufa jama? Mbona kuna watu wanaweweseka nayo hivi. CDM imekufa kama mwendazake. Endeleeni na maisha bila CDM kama maisha yanavoendelea bila mwendazake
 
CDM ni wimbo fulani hivi kama wa taifa hivi. Kuna watu wasipokitaja siku haiendi. CDM si imekufa jama? Mbona kuna watu wanaweweseka nayo hivi. CDM imekufa kama mwendazake. Endeleeni na maisha bila CDM kama maisha yanavoendelea bila mwendazake
Nani ametaja chadema
 
Mfa maji haishi kutapatapa.
Leo hii huyu Ni Kama mzee Halima tu.
Alinyanyasa sana watu na kutuletea wsgombea wasio na sifa za kua wabunge halafu alipoingia ikulu ndio alitegemea kuabudiwa Kama mwendazake lkn mipango haikua na Majaliwa.
Sasa hivi yeye na mzee Halima level moja
 
Back
Top Bottom