Uchaguzi 2020 Dkt. Bashiru aliwahi kusema CCM haitatumia tena wasanii. TOT na Vijana Jazz wanatosha. Je, amebadili gia angani? CCM wametishwa na "Ni-Yeye"?

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,441
55,018
Nini kimeifanya CCM iachane na idea ya Dr.Bashiru ya kutokutumia wasanii?

Tena alidai ujumbe katika nyimbo za kina Diamond, Harmonize, Ali Kiba, Zuchu, Dula Makabila, etc haziwachomi MABEBERU.

Hebu msikilizeni alichokisema hapa.


 
..Nimeambiwa Tundu Lissu / "Ni-Yeye" anajiamini uwezo wake wa kujenga hoja.

..ati hahitaji washereheshaji na wasanii wa kuchangamsha jukwaa.
 
Bila wingi wa makundi ya wasanii atapunguza ushawishi.Japo wapo watu wanafuata burudani za wasanii hawafuati siasa za mtayarishaji.
 
Bila wingi wa makundi ya wasanii atapunguza ushawishi.Japo wapo watu wanafuata burudani za wasanii hawafuati siasa za mtayarishaji.

..uwezo wa Jpm kujenga hoja ni mdogo sana.

..ndiyo maana ktk mikutano yake kunakuwa na wazungumzaji lukuki.

..kingine anachopenda ni kugawa fedha ili akubalike.
 
Tatizo ni kwamba Dr Bashiru ni mgeni katika siasa za ccm hali iliyopelekea kutokujua kwamba ccm haimo tena mioyoni mwa watu. Lakini Wakongwe ndani ya chama wanajua kwamba ccm ikienda kimya kimya watajikuta yupo mgombea na waandaaji wa mkutano tu.

Ndio maana wanawatumia wasanii kukusanya watu, kwa sababu wengi wanafuata sherehe pamoja nakuwaona wasanii live tena bure bila kiingilio.
 
Yaani mwanaccm anasimama anatoa kauli na wewe unamsikiliza na kumuamini, broo haujitendei haki nakwambia.

Maccm sio mijitu ya kuaminiwa hata kidogo, mtu kama Baahiru au Polepole akikwambia usiku mwema, toka nje ukahakikishe kama kweli ni usiku.
 
CCM wakifanya mkutano bila kina Diamond watajikuta wapo wawili tu mkutanoni.
Bashiru hakulijua hilo tokea mwanzo ndio maana alikurupuka tu kukataa wasanii kwenye kampeni. Sasa angalia nguvu itakayo tumika mwaka huu kuwawezesha wasanii kufika adi vijijini kuhamasisha watu kuhudhuria mikutano ya ccm.
 
Back
Top Bottom