Dkt. Bashiru adadavua umuhimu wa mkoa wa Tabora kihistoria

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
DKT. BASHIRU ADADAVUA UMUHIMU WA MKOA WA TABORA KIHISTORIA

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally ameeleza kwa undani umuhimu wa mkoa wa Tabora kihistoria, ikiwa ni pamoja na namna Mwalimu Nyerere alivyotoa machozi akipigania Uhuru wa Tanganyika mwaka 1958 akiwa mkoani humo.

Ameeleza hayo, leo tarehe 30 Januari, 2021 akiwa katika mkutano wa hadhara wa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.

"Mkutano wa TANU uliofanyika hapa Tabora ulimtoa machozi Hayati Baba Wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere baada ya kutoa kauli na kusema kuwa kama Waingereza watachelewesha Uhuru,Watanganyika tutawashitaki kwa Malkia wao. Wasimpomtii, tutawashitaki Umoja wa Mataifa Wasipotii tutawashitaki kwa Mwenyezi Mungu".

Katibu Mkuu ameeleza kwa undani namna ambavyo maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kutilia mkazo somo la historia itakavyosaida kukuza uzalendo wa vijana kwa taifa lao.

Imetolewa na;
Said Said Nguya
Afisa habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
 
Thamani ya mkoa wa Tabora
inbound7644694525095986922.jpg
 
Tangu Uhuru 1961 mkoa wa Tabora ulisahaulika saana... sema tu wanyamwezi kwa asili ni watu wavumilivu sana.
 
Back
Top Bottom