Dkt. Ashatu Kijaji atembelea TBS kujionea maendeleo ya ukaguzi wa gari la kutumia mfumo wa umeme lililobuniwa na Mtanzania Masoud Kipanya

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
Na Mwandishi wetu

WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Ashatu Kijaji ametembelea Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa ajili ya kujionea maendeleo ya ukaguzi wa gari la kutumia mfumo wa umeme lililobuniwa na Mtanzania, Masoud Kipanya.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kujionea maendeleo ya ukaguzi wa gari hilo makao makuu ya TBS, jijini Dar es Salaam, Waziri Dkt. Kijaji, alisema gari la Masoud tayari lipo TBS kwa ajili ya ukaguzi na anampongeza sana kwa kuonesha dhamira njema ambayo wamekuwa wakiitoa kuwataka vijana wawe wabunifu, hivyo na yeye (Masoud) ameibeba kwa vitendo.

"Ndio maana leo (jana) tupo hapa (TBS) kuona kipi ambacho amefanya na TBS wana jukumu la kuhakikisha kila bidhaa ambayo ipo ndani ya soko letu haina madhara kwa wananchi, watumiaji na ndiyo maana gari hilo lipo," alisema Dkt. Kijaji.

Alifafanua kwamba wamekuwa wakishirikiana na Masoud kama wizara ya Viwanda, Biasahara na Uwekezaji kupitia taasisi ya SIDO tangu alipoanza kazi ya kutengeneza gari hilo na sasa amefikia mwisho kama ilivyoonekana wiki mbili zilizopita alipolitoa nje gari hilo na Watanzania wakaliona.

"Kwa hiyo sisi kama Wizara tuna jukumu la kuhakikishia chombo chake kipo salama kwa ajili ya matumizi salama kule nje kwa wananchi," alisema Dkt. Kijaji na kuongeza;

"TBS wameishakagua gari hilo na wanasema ipo tayari kwa matumizi, lakini yapo mambo wanatakiwa kukaa naye na kuelekezana naye ili ayafanyie kazi."

Alisema mambo hayo akishayafanyiwa kazi gari hilo litaweza kuingia sokoni na kumuwezesha kuzalisha magari mengine zaidi na hilo jukumu la wizara na kama waziri mwenye dhamama ndiyo maana amefika TBS mwenyewe.

Hata hivyo, alisema miongoni mwa marekebisho yanayotakiwa kufanywa ni usukani, kwenye chesesi kuna vitu anatakiwa afanyie marekebisho, ambavyo atakaa na wataalam waelekezane ili gari hilo liweze kupita katika barabara za aina zote.

Alisema jinsi lilivyo kwa sasa linaweza ikapita kwenye barabara hizo, lakini likaumia ndani ya muda mfupi.

Kwa mujibu Waziri Dkt. Kijaji rekebisho lingine kwenye gari hilo ni upande wa dereva akiingia anatakiwa awe peke yake, lakini wao wanatamani watu watatu waweze kukaa kwenye gari hilo.

"Kwa hiyo tunataka tukae naye ili aweze kutengeneza chombo chenye kutumika kulingana na uhitaji wa soko letu lilivyo, ninyi ni Watanzania mnaona magari tunayoyatumia na tunatamani afike kwenye viwango hivyo ndiyo jukumu la TBS kushauri hilo na sisi kama wizara tunasimamia kuona anafikia viwango vizuri na sisi tuseme tuna gari letu, ndani ya Taifa letu," alisema.

Waziri alisema Masoud anatakiwa kuandika barua kwa Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) ili wawaandikie TBS kwa ajili ya kutoa cheti cha uthibitisho kama gari hilo lipo tayari na linaweza kwenda sokoni.

Alisema jana asubuhi alizungumza na Masoud na alimwambia tayari barua yake aliishaiandika kwenda SIDO, hivyo wao kama Serikali wanafanyia kazi suala hilo kupitia taasisi hizo mbili (TBS na SIDO) ili aweze kupata certification baada ya marekebisho ili gari hilo liende sokoni.

Kuhusu wagunduzi wengine, Waziri alisema wanawatambua wote waanze kufiki vijana wa Kitanzania kuanzia kwenye fikra zao ndiyo maana wameona Masoud amefikia hapo. Kama Wizara wanasema wamejipanga vizuri.

"Serikali ya Awamu ya Sita tunataka tusafiri na vijana hawa tuwalee kuanzia kwenye mawazo yao mpaka tuwajenge hatua kwa watua ili bidhaa zao ziweze kwenda sokoni na sio kurudi nyuma," alisema.

IMG-20220427-WA0356.jpg

IMG-20220427-WA0357.jpg

IMG-20220427-WA0354.jpg

IMG-20220427-WA0356.jpg
 
Lakini si kuna kampuni moja kule arusha inarekebisha magari ya watalii na kuwa ya umeme?

Sijawahi kusikia wanatembelewa hivyo.

Halafu pamoja na jitihada yake magari ya Kipanya hana kifaa chochote kilichoundwa au kutengenezwa Tanzania.

Ninachikiina hapo ni assembly si manufacturing.
 
Lakini si kuna kampuni moja kule arusha inarekebisha magari ya watalii na kuwa ya umeme? Sijawahi kusikia wanatembelewa hivyo...
Huo ni mwanzo mzuri. Hata Roma haikujengwa siku moja.

Tumtie moyo ndugu yetu Kipanya
 
Amtembelee na bm coach, bus lake miaka kumi tbs wanalikagua
 
Lakini si kuna kampuni moja kule arusha inarekebisha magari ya watalii na kuwa ya umeme? ...
hiyo assembling inatosha kumtambua na kumtia moyo Ili aweze kuunda kitu bora zaidi baadae hata hao walioendelea katika sayansi na ugunduzi walianza kama hivyo, wacha wivu wa husda kuwa na wivu wa maendeleo.
 
Tuwe wakweli hiyo gari bado sana.

Amejaza mavyuma badala ya fibers ambazo hutumika kutengeneza magari mengi siku hizi

Pia Masoud hatakiwi penga uza hiyo tololi bali anatakiwa arudi kwenye mchoro na aongeze kwh za hiyo gari na apunguze chaji time.

Aerodynamics za hiyo gari sio kabisa

Suspension system nayo mmmmh
 
Ukiangalia tu hiyo rear overhang yapickup load kutoka kwenye tairi la nyuma kuna uwalakini wa proportion and accepted length kwa gari ndogo.

Ni hivi ingekuwa vitu rahisi ivyo na hakuna vigezo vya usalama, adherence za mechanical engineering and so forth dunia ingejaa kila aina ya bidhaa.

Haya mambo yanawezekana kwenye nchi ambazo tunadhani ata body za mabasi ni kujichongea tu uwani kwako, gari likipata habari linachinja tu abiria kirahisi.
 
Lakini si kuna kampuni moja kule arusha inarekebisha magari ya watalii na kuwa ya umeme?

Sijawahi kusikia wanatembelewa hivyo.

Halafu pamoja na jitihada yake magari ya Kipanya hana kifaa chochote kilichoundwa au kutengenezwa Tanzania.

Ninachikiina hapo ni assembly si manufacturing.
Hizi ni siasa uchwara na inaonyesha watawala hawa wa hovyo kabisa hawana kazi ya kufanya ndiyo maana wanajiingiza kwenye mambo ya hovyo hovyo!
 
Assembly mchezo? Jaribu kuassemble na wewe tuone matokeo yako.
Hivi nchi yetu imekosa watu wenye akili kiasi hiki jamani mpaka kufikia kujishughulisha na ujinga kama huu? Haya si ni mambo yanayofanywa na watoto huko mitaani wakati wanacheza? Kweli kua uyaone!
 
hiyo assembling inatosha kumtambua na kumtia moyo Ili aweze kuunda kitu bora zaidi baadae hata hao walioendelea katika sayansi na ugunduzi walianza kama hivyo, wacha wivu wa husda kuwa na wivu wa maendeleo.
Husda kwenye hili kopo! Tanzania wote tunaonekana kama wendawazimu sasa kwa kuanza kusifia ujinga kama huu. Mimi nilidhani haya yangefanywa na watoto mitaani wakati wanacheza!
 
Back
Top Bottom