Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
Mdau wa JamiiForums alitaka ushauri kuhusu tabia yake ya kunywa soda mara nne kwa siku, ambapo anaona si hali ya kawaida na alitaka kujua jinsi anavyoweza kuacha matumizi hayo ya soda.
Soma zaidi: Msaada: Nimefikia hatua ya kunywa Pepsi 4 kwa siku, nifanyeje kuacha?
Kutokana na hilo, tumempata Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani na Figo kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili – Mlonganzila, Dkt. Anthony Gyunda, ambaye ametoa maelezo ya kitaalamu kuhusu athari za kiafya za tabia hiyo na ushauri wa nini kifanyike kubadili mwenendo huo.
Swali: Je, ni kweli kuwa unywaji wa soda kupita kiasi unaweza kusababisha ugonjwa wa kisukari?
Jibu: Ni kweli, unywaji wa soda na vitu vingine vya sukari ni risk (hatari) kwa kupata kisukari. Epuka vitu vya sukari nyingi kama soda, juices, energy drinks nk.
Swali: Kuna uwezekano mtu kuwa na uraibu wa vinywaji vyenye sukari nyingi kama soda na juisi? Kitaalamu, hili linaelewekaje?
Jibu: Sukari yenyewe inaleta uraibu, pia vinywaji vingine vya chupa na makopo huwa vinatunzwa kwa kuweka preservatives ambazo zingine zinaleta uraibu kama madawa ya kulevya tu.
Swali: Mtu anawezaje kuacha au kupunguza uraibu wa vinywaji vitamu? Kuna mbinu au ushauri wowote wa kiafya?
Jibu: Jinsi ya kuondokana na uraibu wa sukari ni sawa tu na uraibu mwingine kama wa madawa ya kulevya. Ushauri nasaha, maamuzi ya a muathirika mwenyewe na matumizi ya dawa za kukakata uraibu.