Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
Mwenyekiti wa Bodi (JUKATA), Dkt Ananilea Nkya anazungumzia mchakato wa zoezi la Uandikishaji na Uboreshaji Wapiga Kura linaloendelea Dar es Salaam.
Kuhusu mwitikio sijafanya utafiti lakini mahali ninapoishi, Mtaa wa Tabata Darajani, Ilala nimeona tangu Jumatatu zoezi la kuboresha daftari lilipoanza kituo kinaonekana kuwa na Wananchi waliokuja kujiandikisha.
Mfano Alhamisi Machi 20, 2025 kuanzia majira ya Saa Sita mchana hadi 12 Jioni kulikuwa na kundi la Wanafunzi ambapo nilipomhoji mmoja wao alisema wao ni Wanafunzi wa kidato cha Nne wa Shule ya Sekondari Kimanga walikuwa wamekuja kujiandikisha kupiga kura mwaka huu.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Kwa mtazamo wangu ni kwamba kama uhamasishaji wa Wanafunzi wa Sekondari waliofikisha umri miaka 18 kujiandikisha kupiga kura utakuwa umefanyika nchi nzima basi chaguzi zijazo nchini kwetu wapiga kura vijana watakuwa ni wengi jambo ambalo ni jema kwa maendeleo ya demokrasia nchini.
Hiyo itanoga zaidi kama maboresho madogo ya Katiba yatafanyika kabla ya uchaguzi wowote mwingine kufanyika nchini ili ziweze kutungwa Sheria zitakazowezesha uchaguzi huru na wa haki.