Dkt. Abbas, unapigwa changa la macho juu ya Makandarasi wa Maji

Kweli kabisa mkuu.
Halafu utafikiri haya matatizo wanasiasa hawayaoni.
Ndiyo maana tunaisfia Wizara ya Ujenzi na kuiponda hii ya Maji katika kutekeleza miradi kwa weledi.
 
Ukiona mwanasiasa anatafuta mchawi wa kumsukumia lawama kwa kushindwa mradi, eti ni mkandarasi, ujue kashindwa kazi!
Ni kweli, haya matatizo ya Sekta yanatengenezwa. Solution zipo lakini wameamua kukaa kimya.

Ni suala la kuita kikao na Makandarasi wa miradi ya Maji then wanakupa hints

Baadaye unaitisha kikao na Wataalamu wa Sekta watakupa changamoto zao

Mchawi wa miradi ya Maji anajulikana
 
Kweli kabisa mkuu.
Halafu utafikiri haya matatizo wanasiasa hawayaoni.
Ndiyo maana tunaisfia Wizara ya Ujenzi na kuiponda hii ya Maji katika kutekeleza miradi kwa weledi.
Ni kweli, walichoweza wa Ujenzi licha ya mazingira yao ya kazi kuboreshwa lakini pia wameweza sana kujitenga na Siasa.

Sekta ya Maji na Siasa ni kama Uji na Mgonjwa πŸ˜€
 
Ni kweli, walichoweza wa Ujenzi licha ya mazingira yao ya kazi kuboreshwa lakini pia wameweza sana kujitenga na Siasa.

Sekta ya Maji na Siasa ni kama Uji na Mgonjwa πŸ˜€
Ha ha ha!
I hope yule mtaalam wa kuwatua ndoo kina mama, Mh Juma Aweso-Waziri wa Maji, apitie hapa!
 
A good way forward.
 
Nakupe heko kwa maelezo yako. Ila ningeomba labda utumegee matatizo ya wizara, mashirika, na wandarasi katika hii sekta ya maji. Mimi nimeshuhudia miradi miongi ya maji kufa, na hii ni tangu wakati wa serkali ya hayati mwalimu. Miradi hii ilihujumiwa na viongozi wakishirikiana na viongozi, lakini hata raia nao walihusika katika kuhujumu miundo mbinu ya miradi. Mfano wangu ulikuwa sehemu fulani ambao wananchi walikuwa wanachimua mabomba kutengeza bangili za wakina mama. Kuna sehemu nyingi mkandarasi alipewa kuchimba lambo, lakini akaishia kuchimba shimo tu, akachukuwa pesa akaambaa (huenda alishirikiana na viongozi) na hadi leo hata shimo halipo.
 
Declare your interest tafadhali!
 
Thank you. Excellent analysis.
 
Nafikiri ni kweli ucheleweshaji wa malipo unaleteleza miradi kutokamilika au kutokamilika kwa wakati. Ucheleweshaji wa miradi pia huongeza gharama za miradi maana ukichelewa miezi sita kulipwa, utakapolipwa gharama zitakuwa zimepanda (bei kuongezeka).
 
Na hiyo ndiyo sababu Kuu
 
Dah labda 2010 maana 2015 hata taasisi ya Jakaya Kikwete ilikuwa ipo. Kuna mambo yalikosewa na yalipatiwa tusiwasingizie wastaafu wote.

Tukisema hivyo maana yake kila kitu kimefanyika kuanzia 2015 sio? Ni hii miradi michache tu isitufanye tudharau na makubwa yakiyokuwepo kabla.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…