Dk. Wategere Kitoji: Rais John Magufuli bado anatafuta ‘krimu’ ambayo itaendana na kasi yake

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
428
368
1569059666701.png

MTAALAMU wa masuala ya Diplomasia kutoka Chuo cha Diplomasia Dar es Salaam, Dk. Wategere Kitoji amesema kuwa Rais John Magufuli bado anatafuta ‘krimu’ ambayo itaendana na kasi yake. Wategere alitoa kauli hiyo saa chache jana, baada ya Rais Magufuli kufanya uteuzi za viongozi mbalimblai, akiwemo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Lowate Sanare ambaye amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, kuchukua nafasi ya Dk Steven Kebwe.

Kebwe alitabiriwa kung’oka katika nafasi yake hiyo kutokana na ajali ya lori la mafuta Morogoro, iliyotokea Agosti 10 na kupoteza maisha ya watu 104 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuunda tume. “Ukiona Rais anafanya mabadiliko ujue kuna kitu amekiona, anatafuta watu ambao watatimiza malengo ambayo nchi itafikia, hivyo ni lazima angalie wale watakaoendana na kasi yake,”alisema Wategere.

Kwa upande wake, Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Pius Msekwa alisema kwa kifupi “Niseme tu Rais anafanya kazi kwa mujibu wa Katiba, uteuzi anafanya kwa namna anavyoona inafaa”. Mwenyekiti wa chama cha TLP, Augustine Mrema alisema bado rais ana kazi kubwa, kuunda serikali yake hasa kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu. “Nampongeza Rais Magufuli, kuna watu wapo wapo tu hawajui Rais anataka nini, yaani wao mpaka wasukumwesukumwe, aendelee hivyo hivyo kutengeneza safu yake, apate watu wanaojua nini anataka na wapi anataka kutufikisha kama nchi katika maendeleo kuelekea uchumi wa kati.

Kwa kweli mimi namwambia bado wapo wengi wanaotakiwa kutumbuliwa tu , asichoke wala asisite kufanya mabadiliko pale anapoona inabidi” alisema. Akitangaza uteuzi huo Ikulu Dar es Salaam, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi alisema pia Rais Magufuli ameteua mabalozi 12, wakisubiri kupangiwa vituo vyao vya kazi, baada ya waliopo katika nchi hizo kustaafu au kurejeshwa nyumbani kupangiwa kazi nyingine.

Walioteuliwa ni Dk Modestus Kipilimba ambaye ni Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa. Wengine ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dk Benson Bana, aliyekuwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali, Mohamed Mtonga, Jilli Maleko ambaye alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara na Meja Jenerali mstaafu, Anselm Bahati. Wengine ni Profesa Emmanuel Mbena aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha St John’s Dodoma, Katibu Mkuu mstaafu Ofisi ya Waziri Mkuu, Maimuna Tarishi, Meja Jenerali mstaafu Gaudence Milanzi, Ali Mwadili aliyekuwa Kansela Mkuu Ubalozi mdogo wa Dudai na Jestus Kinyamwanga, Mkurugenzi wa Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje.

Wengine ni Profesa Kennedy Gaston ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa taasisi ya kimataifa ya Asian African Legal Consultative Organization ambayo makao yake makuu yako New Delhi India na Aishi Amour, ambaye alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro. Dk Kijazi ataja vituo vya kazi vya mabalozi hao kuwa ni Abu Dhabi katika Falme za Kiarabu, Bujumbura (Burundi), Brussels (Ubelgiji), Pretoria (Afrika Kusini), Cairo (Misri), Harare (Zimbabwe), Kuwait City (Kuwait), Riadhi (Saudi Arabia), Tokyo (Japan), Umoja wa Mataifa (Uswisi), Umoja wa Mataifa (New York Marekani) na Abuja nchini Nigeria.

Pia Dk Kijazi alisema aliyekuwa Msaidizi wa Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mussa Masele ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro. Rais amefanya pia uhamisho wa wakuu wa wilaya wawili: Charles Kabeho aliyekuwa Tarime anakwenda Chato na aliyekuwa Chato, Msafiri Simeon anakwenda Tarime.

Aidha, Rais ameteua katibu mkuu mmoja, naibu makatibu wakuu watatu na naibu wakili mkuu wa Serikali mmoja. Tixon Nzunda aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi anayeshughulikia masuala ya elimu, amekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Bunge. Aliyekuwa Kamishna wa Bajeti katika Wizara ya Fedha, Mary Maganga ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu atakayeshughulikia utawala katika wizara hiyo.

Anthony Sanga aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira jijini Mwanza, ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji. Dk Ally Posi ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo. Dk Posi alikuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali na nafasi yake imechukuliwa na Gabriel Malata, aliyekuwa Kamishna wa Kazi katika ofisi ya Waziri Mkuu.

Rais pia amewahamisha naibu makatibu wakuu wawili; Nicholas Mkapa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye amekwenda Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuendelea na wadhifa huo ; na Mathias Kabunduguru aliyekuwa katika wadhifa huo katika wizara hiyo amepelekwa kuendelea na wadhifa huo wizara ya Tamisemi. Makatibu Tawala walioteuliwa na maeneo yao katika mabano ni Alphayo Kidata (Mtwara), Emmanuel Kalogero (Morogoro) na Dk Habib Kazungu (Kilimanjaro).

Rais amewapandisha vyeo maofisa watatu kuwa mabalozi, ambao ni Steven Mbungi ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulinzi, Siasa na Usalama Wizara ya Mambo ya Nje , Ally Bujiku na Dk Mussa Ulandala ambao ni wasaidizi wa Rais.
 
Anapanga safu hadi lini? 2020 Novemba akiongoka hiyo timu yake itakuwa imesha settle na kuwa nalakufanya?
Maana kabaki na mwaka mmoja na mwezi mmoja na kunaonekana itakuwa kuachiwa mzigo wa madeni na chronic shida.
 
Ataongoza miaka mitano mingine japo najua hutopenda lakini ndio uhalisia
 
Awateue vijana wengi kuwa Mabalozi wa Tz huko nje ya nchi, aachane NA utaratibu wa kuwateua wazee waliochoka mwili NA AKILI kwani wengi wao huwa wanakuwa na roho mbaya sana wawapo huko nje. Wanatusumbua sana sisi Watz tunaoishi nje ya nchi wakati tunapokwenda kwenye Of is I za Ubalozi wa Tz kufuata huduma. Wengi bado wana mawazo mabaya ya enzi za Ujima, wakimuona Mtanzania yupo nje ya nchi wao wanamhesabia kuwa ni Mzurulaji huko nje.

Rais awateue vijana wengi wenye mawazo NA fikra mpya za kisasa zinazoendana NA wakati wa sasa.
 
Huyo dr asubiri uteuzi mudawowote anaula kikubwa amesifu hatupatani nakosoaji
View attachment 1212764

Huyo dr uteuzi unamuhusu muda simrefu napenda wanaonisifu hatakama niwanafiki ilasipendi wakosoaji hata kama niwakweli nawaaminifu
 
Back
Top Bottom